Afisa wa Trump asema yeye ni miongoni mwa wanaomuhujumu rais wa Marekani

US President Donald Trump responds to a journalist at the White House

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Trump akizungumza na waandishi wa habari White House

Rais Donald Trump wa Marekani amelihimiza jarida la New York Times kumfichua afisa mkuu wa serikali yake, aliyeandika makala ya gazeti hilo, akidai baadhi ya wafanyikazi serikalini walikuwa wakifanya kila wawezalo, ili kutatiza ajenda yake ya maendeleo.

Trump amemtaja mwandishi wa makala hiyo, ambaye jina lake limefichwa, kama mchochezi, na kuashiria kuwa uchapishaji wenyewe wa makala hiyo ni kosa la jinai.

Mwandishi huyo asiyetajwa amesifu ufanisi kidogo wa utawala wake, lakini akasema baadhi ya maamuzi ya Bwana Trump yamekuwa yasiyofikiriwa na ya kipuuzi.

Msemaji wa jarida la New York Times amesema gazeti hilo linajivunia kuwa lilichapisha makala hayo, ambayo amesema yamesaidia raia kuelewa kile kinachoendelea katika uongozi wa Rais Trump.

Chanzo cha picha, Getty Images/NYT

Maelezo ya picha,

Picha ya Trump kenye jarida la New York Times

White House imejibu kwa njia gani?

Tayarai kumekuw na shinikizohuko White House za kumtafuta na kumtambua afisa aliyetoa taarifa hizo.

Rais alisema makala hiyo ni hujuma na afisa wa mawasiliano wa White House Sarah Huckabee Sanders alituma jibu lenye maneno makali.

"Mtu ambaye aliandika makala haya amechagua kumhujumu badala ya kumuunga rais wa Marekani aliyechaguliwa," aliandika. Haweki mbele nchi bali maslahi yake ndiyo ameyaweka mbela badala ya watu wa Marekani.

Bi Sanders na Bw Trump wote wamelikosa jarida la The New York Times kwa kuchapisha makaa hiyo, huku Trump akisema kuwa makampuni yote ya habari yatakosa biashara mara atakapoondoka ofisini kwa kuwa hayatakuwa na kitu cha kuandika.

Hueda kukawa na wito wa kutaka afisa huyo kujifichua.