Mtu mwenye ulemavu wa akili apatikana na vijiko na kalamu tumboni baada ya upasuaji Tanzania

Mtu mwenye ulemavu wa akili apatikana na vijiko na kalamu tumboni baada ya upasuaji Tanzania

Huko nchini Tanzania mtu anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili amesababisha hali ya taharuki, baada ya kufanyiwa upasuaji na kupatwa na vitu visivyo vya kawaida tumboni mwake katika hospitali ya Mugana mkoani Kagera Kaskazini Magharibi mwa Tanzania. Jambo hilo limezua mjadala mkubwa na baadhi ya watu tulihusisha na Imani za kishirikina.

Mwandishi wa BBC Leonard Mubali amezungumza na Mganga mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dkt Marko Mbata na kwanza anaeleza sababu ya kupelekwa hospitalini kwa mgonjwa huyo.