Yawezekana kuwa na serikali zinazoendeshwa na wanawake pekee?

Wanaume wameondolewa kwenye serikali na wanawake wakawekwa wachukue hatamu. Huo ni muktadha mkuu kwenye mchezo unaotarajiwa kuzinduliwa siku ya Alhamisi ambao umeandikwa kwa ushirikiano na kundi la wanawake walio kwenye mamlaka ya juu ya utawala. Je, wadhani inawezekana kuwa na serikali iliyo na wanawake pekee? Tupe maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Facebook, BBCswahili.