Sokwe wapewa majina katika sherehe ya kufana nchini Rwanda

Sherehe za kuwapatia sokwe majina zafanyika Rwanda

Nchini Rwanda zimefanyika sherehe za kuwapa majina watoto wa sokwe 23 katika eneo la milimani kaskazini mwa nchi hiyo.

Sekta ya utalii ni ya kwanza kuingizia Rwanda fedha nyingi.

Ni mwaka mmoja tangu serikali ya nchi hiyo kupandisha mara dufu bei ya kutalii sokwe hao.

Baadhi ya wadau wa sekta hiyo wanasema wameathirika kutokana na uwamuzi huo huku serikali ikisema pato linazidi kuongezeka

Majina haya hutolewa na baadhi ya watu mashuhuri duniani.

Sherehe za leo walikuwepo Rais Wa zamani Wa Nigeria Olusegun Obasanjo mama Graca Mashel mke Wa marehemu Nelson Mandela , wafanyabiasha wakubwa duninia na baadhi ya wachezaji wa zamani Wa Arsenal, wanamuziki kama Akon miongoni mwa wengine.

Hata hivyo siyo kila mtu anayeweza kutalii sokwe hao tangu serikali kuongeza bei toka dolla 750 hadi elfu 1500…..Baadhi ya wadau wa utalii wanasema waliathirika kwa njia moja ama nyingine

Kutokana na shughuli za utalii mji huu na hata kando kando mwa mbuga inayohifadhi sokwe kunasheheni migahawa na mahoteli ya kiajabu baadhi ya wamiliki wanasema mambo ni shwari

Maelezo ya video,

Sherehe za kuwapatia majina sokwe zafanyika nchini Rwanda

Wengine wananuna kuzungumzia swala hili wakisema tu kwamba watalii wengi wa kizungu waliahirisha ziara zao za kutalii mbuga hii.

Serikali haijawa wazi kuhusu kupungua ama kuongezeka kwa watalii baada ya ongezeko la bei ya kuzuru sokwe kwa mujibu wa ,Prosper Uwingeri ambaye ni mkuu wa mbuga ya Volcano

Mamlaka ya hifadhi ya mbuga ya volcano inasema kutokana na pato kubwa la utalii wa sokwe ilamua kuongeza toka asilimia 5 hadi 10 fedha za mgao kwa jamii inayoishi karibu na mbuga ya volcano.

Pesa hizo hasa hasa hugawiwa mashirika ya watu ambao zamani walikuwa wawindaji haramu wa sokwe

Mbuga hii ya Volcano inahifadhi jumla ya sokwe 281.

Rwanda inasema kila mwaka sekta ya utalii huingiza dolla milioni Zaidi ya 400 na lengo likiwa kuingiza milioni 800.