Obama ashutumu upuzi unaotoka kwa ikulu ya Whitehouse ya rais Donald Trump

Rais Donald Trump na mtangulizi wake Barrack Obama

Aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama amemshutumu mrithi wake Donald Trump na mambo ya 'kipuuzi yanayotoka' katika ikulu ya Whitehouse.

''Hii sio kawaida huu ni wakati usio wa kawaida na ni wakati hatari'', Obama aliwaambia wanafunzi katika chuo kikuu cha Illinois.

Alitaka kurejeshwa kwa uaminifu na heshima na sheria kufuatwa katika serikali.

Rais huyo wa zamani amekuwa akifanya mambo yake kwa siri tangu alipoondoka mamlakani 2017.

Bwana Obama aliambia sherehe hiyo ya kuwatuza wanafunzi mjini Urbana jimbo la Illinois kwamba amekuwa akitaka kufuata utamaduni wa marais wa zamani kupitia kuondoka katika ulingo wa kisiasa.

Badala yake aliushutumu utawala uliopo wa Republican.

Akimjibu, rais Trump alisema katika mkutano wa mchango wa Republican huko fargo kaskazini mwa Dakota siku ya Ijumaa kwamba aliitazama hotuba ya mtangulizi wake ,''lakini nililala''.

''Bwana Obama alijaribu kujipatia sifa ya mambo mazuri yanayoendelea nchini'', aliongezea.

'Vita vimetangazwa'

Wanachama wa Democrats - ambao wamekasirishwa wamekuwa wakisuburi kujitokeza kwa Barack Obama kwa muda mrefu

Chama hicho kimekuwa na wasiwasi kuvunja utamaduni unaosema kuwa marais wa zamani hawafai kuingilia siasa za nchi wakiwa nje.

Pia kumekuwa na swala la kuandika kitabu mbali na kutafuta fedha za kufadhili wakfu wake.

Lakini sasa anaonekana kwamba amejiandaa kujitosa katika kampeni za miaka ya katikati katika muda wa wiki nane ujao.

Huku ajenda ya hotuba yake ikiangazia ukosoajia wa rais aliyepo madarakani, kulikuwa na ujumbe mwingi uliolenga chama chake. Kujenga miungano-ya kijamii na kiuchumi.

Ndio mbinu iliomuhakikishia ushindi wa awamu mbili na ni ujumbe wake kwa chama hicho huku kikijaribu kuchukua udhibiti wa bunge la Congress.

Lakini kuna tatizo kubwa hapa, kwa Barrack Obama na kwa chama chake. Hakuna wasiwasi kwamba ana uwezo wa kuwapatia motisha wanachama wa chama hicho.

Lakini hatari yake ni kuimarisha umoja wa chama cha Republican. Kitu kimoja ambacho tuna hakika nacho ni kwamba Donald Trump atahisi kwamba amepata kitu kulenga wakati wa kampeni.

Katika hotuba yake , bwana Obama alionya kwamba demokrasia ya Marekani inategemea raia wake wanaojitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa Novemba wa bunge la Congress.

''Sasa wengine wenu wanasema ninatilia chumvi ninaposema kwamba uchaguzi huu ni muhimu zaidi ya wowote ule katika maisha yangu'', alisema mwanachamna huyo wa Democrat.

Lakini vichwa vya habri vya hivi majuzi vimeonyesha wazi kwamba wakati huu ni tofauti.

Obama alizungumzia kuhusu kichwa cha habari cha gazeti la The New York times kilichomkasirisha rais Trump.

''Mwandishi asiyejulikana aliandika kwamba afisa mmoja mkuu katika utawala wa rais Trump alidaiwa kushirikiana na wenzake ili kulinda taifa hili dhidi ya mporomoko mbaya wa uongozi wa rais wa sasa''.

Bwana Obama alisema: Hawatusaidii kwa kukuza asilimia 90 ya upuuzi unaotoka katika Ikulu ya Whitehouse na baadaye kusema, musijali.

Tunalinda asilimia 10 iliosalia. Lakini pia aliuambia umati mkubwa kwamba bwana Trump ni dalili na sio sababu ya mgawanyiko uliopo nchini Marekani.

Alikashifu wito wa Trump kwa idara ya haki kuchunguza wapinzani wake wa kisiasa.

''Haifai kusema kuwa tutatumia idara ya haki ama FBI kuwaadhibu wapinzani wetu wa kisiasa''.