Afcon 2019: Kenya yailaza Ghana, Tanzania yaizuia Uganda

Chanzo cha picha, Getty Images
Goli la kujifunga la Nicholas Opoku katika kipindi cha kwanza liliisaidia timu ya nyumbani Harambee Stars yenye wachezaji kumi kuvunja bahati mbaya ambayo imekuwa nayo ya miaka 15 dhidi ya Black Stars ya Ghana baada ya kuilaza 1-0 katika mechi ya kufuzu kwa kombe la bara Afrika 2019 kundi F katika uwanja wa kasarani .
Krosi ya Eric Johanna kutoka upande wa kulia ilimgonga beki Opuku na kuingia katika wavu hivyobasi kuifanya Kenya kuchukua uongozi dakika tatu kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Beki wa Gor Mahia Joash Onyango alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea visivyo mshambuliaji wa Ghana Majeed Waris.
Wakati huohuo Uganda Cranes ilishindwa kujizolea alama tatu dhidi ya Taifa Stars ya tanzania nyumbani.
Hatahivyo timu hiyo ambayo haijashinda mechi kubwa chini ya ukufunzi wa Sebastien Desabre bado inaongoza katika kundi L baada ya mechi mbili ikiwa na pointi nne.
Hatahivyo fursa hiyo itategemea siku ya Jumapili wakati ambapo makundi mengine yanacheza, lesotho na cape verde zitakabilia katika mechi ya raundi ya pili.
Iwapo Lesotho itailaza Cape Verde kwa zaidi ya bao moja ,basi itapanda hadi kilele cha kundi hilo huku Uganda ikiwa ya pili.