Cardi B na Nicki Minaj wapigana katika sherehe mjini New York

Nicki Minaj na Cardi B

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Cardi B (kulia) anadaiwa kumfuata Nicki Minaj (kushoto} kabla ya vita hivyo kuzuka

Uhasama ulioibuka kati ya Cardi B na Nicki Minaj ulibadilika na kuwa vita katika sherehe ya tamasha la New York Fashion Week siku ya Ijumaa jioni.

''Mgogoro huo ulizuka baada ya rapa Cardi kumfuata Minaj kuhusiana na uongo uliokuwa ukisambaa'' , tovuti ya watu maarufu ya TMZ ilisema.

Alipigwa kisukusuku katika uso na walinzi wa usalama kabla ya kumrushia kiatu Minaj ambaye alionekana kutoshangazwa na kitendo hicho.

Baada ya Cardi B kutolewa nje bila viatu na kupata uvimbe juu ya jicho lake , nyota wote wawili waliingia katika mitandao ya kijamii na kuendeleza vita hivyo.

Walioshuhudia waliambia vyombo vya habari nchini Marekani kwamba mzozo huo ulifanyika katika ghorofa ya kwanza ya jumba la Harper Bazaar wakati wa onyesho la Christina Aguilera.

Minaj, ambaye hivi majuzi alitoa albamu yake ya nne kwa jina Queen, baadaye alisamabaza picha ya yeye akisimama akiwa amevalia nguo yenye madoadoa ya chui.

Rapa huyo ambaye amepata ufanisi mkubwa mwaka uliopita kupitia nyimbo kama vile Boda yellow na I Like it alisema kuwa amewacha mambo mengi kupita.

Cardi hakumtaja Minaj kwa jina lakini alisema: Nimekuwacha unitukane, nimekuwacha useme uwongo juu yangu .Pia alimshutumu Minaj mwenye umri wa miaka 34 kwa kuwatishia wasanii wengine , akisema kwamba iwapo watashirikiana na Cardi B atavunja uhusiano wake nao.

Cardi baadaye alielezea : Unapozungumzia mwanangu unapopenda kupenda matamshi yangu kama mama, na kusema kuhusu uwezo wangu kuhusu kumuangalia mwanangu hapo ndipo siwezi kukubali.

Alimaliza kwa kusema alifanya bidii sana kufika katika kiwango hicho na hatokubali mtu yeyote kumuaribia ufanisi wake. Cardi B ambaye jina lake kamili ni Belcalis Almanzar , alijifungua mwanawe wa kwanza wa kile Kulture mwezi Julai.

Chanzo cha picha, Kevin Mazur/Getty

Maelezo ya picha,

Nicki Minaj na Cardi B walionekana kuwa na uhusiano mmzuri katika tamasha la Met Gala mwezi Mei 2018