Korea Kaskazini yaandaa gwaride la jeshi bila makombora ya masafa marefu

Korean People's Army (KPA) soldiers stand atop armoured vehicles during a military parade Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakiwa juu ya magari ya kivita

Korea Kaskazini haikuonyesha makombora ya masafa marefu kwenye gwaride ya jeshi kuadhimisha miaka 70 ya taifa hilo.

Pia haijulikani ikiwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alitoa hotuba kwenye warsha hiyo.

Waride hilo linafuatiliwa kufahamu kuhusu silaha za Korea Kaskazini na iwapo imejitolea kuharibu zana zake za nyuklia.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Kim Jong-un (katikati) alionekana akiwa na mwanasiasa kutoka China Li Zhanshu

Baadhi ya wachambuzi walikuwa wametabiri kuwa Bw Kim angepunguza maonyesho ya silaha kufuatia mkutano na rais wa Marekani Donald Trump.

Maonyesho makubwa ya makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kufika nchini Marekani na yaliyo na uwezo wa kubeba bomu la nyuklia yanaonekana kama uchokozi.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wanajeshi wa Korea wakitembea eneo la Kim Il Sung square mjini Pyongyang

Mwezi Juni Bw Kim na Trump walisaini makubaliano kufanya kazi katika kumaliza silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea lakini hakukuwa na mpangilio wa kufanya hivyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya wanajeshi walishiriki waride hiyo

Mazungumzo ya kiwango cha juu yameendelea lakini ziara ya hivi majuzi ambayo ingefanywa na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Mike Pompeo, ilifutwa dakika za mwisho huku pande zote zikilaumiwa kwa kukwama mazungumzo hayo.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Walioshiriki walipeperusha maaua wakipita mbele ya Kim

Korea Kaskazini pia ilitarajiwa kufanya mazoezi makubwa ya kijeshi kwa miaka mitano.

Uchunguzi wa kutumia satelaiti kutoka wiki mbili zilizopita unaonyesha kuwa maonyesho hayo ya mwaka huu yataendelea hadi mwezi wote wa Septemba yatakuwa makubwa.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wanajeshi wakipiga saluti wakitizama waride
Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Ndege zikipita angani kuadhimisha miaka 70
Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakipita kwenye waride

Mada zinazohusiana