Tajiri mmiliki wa Alibaba Jack Ma kustaafu ili awe mwalimu

Jack Ma speaks during a news conference in Hong Kong, China, June 25, 2018

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Jack Ma ana utajiri wa dola bilioni 40

Mmoja wa watu matajiri zaidi nchini China Jack Ma, atajiuzulu wadhifa wake kama mwenyekiti mkuu wa kampuni ya bishara ya mtandaoni Alibaba mwakani, kampuni hiyo imethibitisha.

Taarifa hii inajiri kufuatia nyingine za kutatanisha kuhusu muda atakaojiuzulu, baadhi wakitaja leo.

Hata hivyo atabaki kwenye bodi ya wakurugenzi lakini atakuwa sasa anaangazia masuala ya utoaji misaada na elimu, kwa mujibu wa gazeti la New York Times.

Bw Ma alianzisha kampuni ya Alibaba mwaka 1999 na ameiongoza hadi kufikia kuwa moja ya kampuni kubwa zaidi duniani.

Ikiwa na thamani ya dola bilioni 400 Alibaba uhusika na mambo yakiwemo uuzaji ya bidhaa mitandano, uzalishaji wa filamu na kuhifadhi nyaraka.

Mwalimu huyo wa zamani wa lugha ya kiingereza anasema kustaafu sio mwisho wa mambo bali sasa ndio mwanzo, akiongeza kuwa "ninapenda elimu".

Bw Ma ambaye atafikisha umri wa miaka 54 siku ya Jumatatu, ana utajiri wa dola bilioni 40 na kumfanya kuwa mtu wa tatu tajiri zaidi nchini China.

Mapema wiki hii Bw Ma alikiambia kituo cha Bloomberg kuwa anataka kuanzisha wakfu kufuata nyayo za tajiri wa Microsoft, Bill Gates.

"Kuna vitu ninaweza kujifunza kutoka kwa Bill Gates," alisema

"Sitaweza kuwa tajiri kama yeye, lakini kitu kimoja ambacho nitaweza kufanya ni kustaafua mapema. Nafikiri siku moja nitarudi kuwa mwalimu. Hiki ni kitu ninaamini nitafanya bora zaidi kuliko kuwa mkurugenzi wa Alibaba."

Bwana Ma alianzia taaluma ya ualimu akifunza luhgha ya kiingerza katika chuo kikuu huko Hangzhou mashariki mwa mkoa wa Zhejiang. Alanzisha kampuni ya ya Alibaba kutoka nyumbani kwake huko Hangzhou.