Drake na Meek Mill wazika uhasama wao wa miaka mitatu

Drake
Maelezo ya picha,

Drake

Drake ameelezea kumalizika uhasama wa muda mrefu na Meek Mill kama wakati bora zaidi kwenye taaluma yake.

Baada ya miaka kadha ya kuzozana mitandaoni na kupitia kwa miziki yao, wanamuziki hao wawili walionekana jukwaani pamoja huko Boston.

Wawili hao wamekuwa wakizozana tangu mwaka 2015 wakati Meek Mill alimlaumu Drake kwa kutoandika nyimbo zake mwenyewe.

Kwa sasa Drake yuko katika tamasha inayojulikana kama Aubrey & The Three Migos

Maelezo ya picha,

Meek Mill alikuwa mgeni wa ghafla kwenye tamasha la Drake huko Boston

Nyota huyo raia wa Canada aliwashangaza mashabiki huko Boston wakati alimuita Meek Mill jukwaani kuimba wimbo wa Dreams and Nightmares

Drake alisambaza picha ya wanaume hao wawili wakiwa jukwaani ambapo aliandika, "kwa kweli hii imenipa utulivu wa akili usiku wa leo."

Uamuzi wao wa kumaliza uhasama ulipongezwa na watu wengi mashuhuri akiwemo mchekeshaji Kevin Hart.

Tofauti za Drake na Meek Mill kilikuwa kitu kilichowashangaza mashabiki. Wanamuziki hao wawili mara kwa mara wameonekana kwenye video pamoja na pia walikuwa na uhusiano mzuri nje ya muziki.

Maelezo ya picha,

Nicki Minaj na Meek Mill walikuwa wapenzi kwa miaka miwili kabla ya kutengana mwaka 2017

Lakini ujumbe alioandika Meek Mill kwenye mtandao wa Twitter Julai mwaka 2015, ulifichua tofauti kati yao.

Meek alimlaumu Drake kwa kujiita rapa licha ya kuandikiwa nyimbo zake.

Ujumbe huo ulisema: "Wacheni kunilinganisha na Drake. Haandiki nyimbo zake!

Kile kilichofuatia vilikuwa ni vita vya maneno, vitisho na nyimbo za kujibizana.

Uhasama kati ya Drake na Meek Mill ulionekana kuwa wa aina yake kwa kuwa wakati huo, Meek alikuwa mpenzi wa Nicki Minaj ambaye naye alikuwa rafiki wa karibu wa Drake.

Maelezo ya picha,

Drake

Uamuzi wa wanaume hao kuonekana jukwaani pamoja unoenyesha kuwa wameweka kando tofauti zao.

Mapema mwaka huu Drake alito ishara nyingine kuwa walikuwa na uhusiano mzuri wakati alionekana jukwaani akiwa amevaa shati lenye maaneno "Free Meek Mill"

Meek Mill alihukumiwa hadi miaka minne jela kwa kukiuka sheria za kifungo cha nje kufuatia kesi iliyohusu mihadarati na silaha cha mwaka 2008.

Kufuatia rufaa aliachiliwa baada ya kutumikia kifungo cha miezi mitano.

Meek Mill alikuwa na waungaji mkono maarufu wakiwemo Jay-Z, mchekeshaji Kevin Hart na tajiri Michael Rubin.