Wadau wa tenisi wasema Serena Williams alibaguliwa kijinsia

Serena Williams

Chanzo cha picha, Getty Images

Chama cha mpira wa tenisi cha wanawa(WTA) kimeunga mkono madai ya nyota wa mchezo huo Serena Williams kuwa amebaguliwa kijinsia.

Afisa Mtendaji Mkuu wa WTA Steve Simon amedai kuwa muamuzi wa fainali ya Jumamosi ameonesha kiwango kidogo cha ustahimilivu katika mzozo wake na Williams kuliko vile ambavyo angefanya laiti angellikwaruzana na mchezaji wa kiume.

Serena ameadhibiwa kwa kukiuka kanuni ya ukufunzi,kutoa matamshi ya matusi na kumuita muamuzi ''mwizi''baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya Mashindano ya Wazi ya Marekani (US Open) dhidi ya Naomi Osaka wa Japan.

"WTA inaamini kuwa hakuna tofauti katika viwango vya uvumilivu vinavyostahili kuelekezwa kwa hisia zinazotolewa na mchezaji mwanamume au mwanamke,'' amesema Bw Simon katika taarifa yake na kuongeza kuwa haamini suala hilo lilizingatiwa katika uamuzi uliyofikiwa dhidi ya Williams.

Simmon pia metoa wito kwa wakufunzi kupewa nafasi katikati ya mchezo kuzungumza na wachezaji.

Mwamuzi Carlos Ramos alimuadhibu Williams baada ya kumuona mkufunzi wake Patrick Mouratoglou,akionyesha ishara ya mkono. Baadaye mkufunzi huyo raia wa Ufaransa alikiri kuwa alijaribu kumuelekeza mchezaji wake.

Mkuu wa shirikisho la mchezo wa Tennisi nchini Marekani (USTA) ,Katrina Adams ,amesema "Wachezaji wakiume wamekuwa wakiwakaripia waamuzi wakati wa kubadilishana upande kuchezea na hatuoni chochote kikitokea.".

Maoni hayo yanaungwa mkono na mwandishi wa mchezo wa Tennis wa BBC, Sue Barker, ambaye amesema: "Nimekaa mara kadha pembeni ya uwanja na kuwaona wachezaji wakiume wakirusha maneno makali kwa waamuzi na hawakuchukuliwa hatua zozote.''

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kocha wa Serena Williams, Patrick Mouratoglou amekiri kuwa alijaribu kumuelekeza mchezaji wake katikati ya mchezo.

Williams, 36, ametozwa faini ya dola $17,000 sawa na euro(£13,100) kwa kukiuka kanuni za mchezo wa Tennis ikiwa ni pamoja na kumuita refa Ramos a "mwongo" na "mwizi". Hata hivyo mchezaji huyo amejishindia dola $1.85m sawia na euro (£1.43m) kwa kufuzu kuingia fainali ya shindano la US Open.

Mizozo iloyopita ya US Open dhidi ya Williams

  • 2009-Nusu-finali ya US Open: Akiwa bado na onyo la kumtusi refa katika mechi ya awali, Williams alimkaripia kwa hasira mwamuzi wa pembeni baada ya kupatikana na hatia ya mguu wake kukanyaga nje ya laini hatua ambayo ilimpatia mpinzani wake Kim Clijsters pointi mbili. Kosa hilo lilimsababishia adhabu iliyomkosesha pointi iliyomwezesha Clijsters kushinda mechi hiyo. Williams aliwekewa vikwazo vya muda kwa kipindi cha miaka milili na kupigwa faini ya dola $175,000 sawa na euro (£135,000), iliyopunguzwa hadi dola $82,500 sawa na euro (£63,750) if endapo hatarudia kufanya kosa lingine kubwa hadi mwaka 2011.
  • 2011 Finali ya US Open: Williams alipiga mayoe akisema "come on" wakati Sam Stosur alipojaribu kurudisha mpira hatua ambayo ilimsababishia kupoteza pointi moja dhidi ya muaustralia huyo. Williams baadaye alimtukana refa(umpere) Eva Asderak hatua iliyomfanya kupigwa faini ya dola $2,000 sawa na euro (£1,265).

Mwamuzi hakutakiwa 'kumsukuma' Williams - Djokovic

Alipoulizwa maoni yake kuhusu mwenendo wa Williams,Novak Djokovic,mshindi mara tatu wa taji la wanaume la US Open siku ya jumapili baada ya kumshinda Juan Martin del Potro, alisema, hatua ya mwamuzi Ramos kuingilia mambo bila sababu za msingi ilibadili mkondo wa mechi."Kwa mtazamo wangu nahis imwenyekiti alimkera Serena kiasi cha yeye kushindwa kustahamili hasa ikizingatiwa ni fainali ya Grand Slam''.

Djokovic, ambaye pia ni mshindi mara 14 wa Grand Slam pia amesema anatofautiana na msimamo wa mkuu wa WTA Bw Simon,akiongeza kuwa hakuyaelewa matamshi yake (kuwa Serena kabaguliwa kijinsia) huku akielezea utata huo ni kama hali ngumu kwa muamuzi na kwamba anaungana na muamuzi huyo kipindi hiki kigumu.