Rais Magufuli awaomba wanawake Tanzania kutopanga uzazi

Women and children Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kwa kawaida mwanamke nchini Tanzania huwa na watato zaidi ya watano

Rais wa Tanzania John Magufuli amewashauri wanawake waache kutumia dawa za kupanga uzazi akisema kuwa nchi inahitaji watu zaidi.

"Wanawake sasa wanaweza kuacha kutumia dawa za kupanga uzazi," Rais wa Magufuli alisema.

Mbunge wa upinzani Cecil Mwambe amekosoa matamshi hayo akisema yanakwenda kinyume na sera za afya za nchi hiyo.

Tanzania ina takriban watu milioni 53, wakati asilimia 49 ya watu wanaishi kwa chini ya dola mbili kwa siku.

Kwa kawaida mwanamke nchini Tanzania huwa na watato zaidi ya watano, ikiwa ni kati ya viwango vya juu zaidi duniani.

Siku moja baada ya matamshi hayo ya Magufuli, spika wa bunge Job Ndugai aliwapiga wanawake wabunge marufuku ya kuvaa kucha bandia bungeni.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kwa kawaida mwanamke nchini Tanzania huwa na watato zaidi ya watano

Bwa Ndugai aliiambia BBC kuwa marufuku hiyo ni kwa sababu za kiafya bila kueleza zaidi.

Marufuku hiyo pia inawauzuia wanawake kuvaa nguo fupi. Wageni wa kike wanaozuru bunge pia na watafuata maagizo hayo.

'Wanawake watupe dawa za kupanga uzazi'

Magufuli alitoa matamshi hayo wakati wa mkutano siku ya Jumapili kwenye mkoa wa kaskazini wa Meatu, akisema watu wanaotumia dawa za kupanga uzazi ni wavivu.

Hawataki kufanya kazi kwa bidii kulisha familia kubwa. Ndiyo sababu watu huamua kutumia njia za kupanga uzazi na kumalizia na mtoto mmoja au wawili," alisema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Magufuli amependekeza sera kadhaa zenye utata tangu aingie madarakani mwaka 2015

"Nimesafiri Ulaya na kwingineko na nimeona athari za kupanga uzazi. Nchi zingine sasa zinakumbwa na upungufu kwa watu."

Bi Mwambe alisema kuwa ikiwa Rais Magufuli anataka matamshi yake yatiliwe maanani, kwanza abadilishe sheria za bima kuwahudumia watoto 10 kinyume na watoto wanne kwa sasa kwa kila familia.

Gazeti la Citizen limesema kuwa hakuna dalili kuwa sera kuhusu idadi ya watu nchini humo zitabadilika kufuatia matamshi hayo.

Rais Magufuli alitoa matamshi kama hayo mwaka 2016, Baada ya kuzinduliwa mfumo wa elimu ya bure ya shule ya sekondari: "Wanawake sasa wanaweza kutupa dawa zao za kupanga uzazi. Elimu ni bure."

Magufuli amependekeza sera kadhaa zenye utata tangu aingie madarakani mwaka 2015.

Mwaka uliopita alipendekeza kuwa wasichana wa shule wanaokuwa waja wazito wazuiwe kuendelea na elimu baada ya kujifungua.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii