Mgogoro katika muziki: Cardi B, Nicki Minaj na wanamuziki wengine wanaozozana

Cardi B na Nicki Minaj Haki miliki ya picha Reuters/Getty

Anapenda fedha , anapenda almasi, anapenda kuwarushia viatu vyenye visigino virefu watu asiowapenda sana.

Mgogoro kati ya Cardi B na Nicki Minaj uligeuka na kuwa vita wikendi iliopita huku wawili hao wakipigana katika tamasha la New York fashion week.

Video iliochapishwa katika jarida la TMZ nchini Marekani ilionyesha wawili hao wakirushiana cheche za maneno huku Cardi B baadaye akilazimika kumrushia kiatu chenye kisigino Minaj baada ya kupigwa kisukusuku cha uso na mlinzi mmoja wa kuweka usalama.

Hatahivyo Minaj alionekana kana kwamba hana habari! Wawili hao waliendeleza vita vyao katika mitandao ya kijamii hususan instagram ambapo walirushiana cheche kali za maneno.

Sio mgogoro wa kwanza katika sekta hiyo ya muziki. Na sio hata wa kwanza kati ya Nicki Minaj na mwanamuziki wa kike katika historia. Kuna wengine.

1. Lady Gaga v Madonna

Haki miliki ya picha Reuters/EPA

Wakati Lady Gaga alipotoa kibao kwa jina Born This Way mwaka 2011, ni watu wachache walifikiria kwamba ni wimbo unaojulikana, mmoja wao akiwa Madonna, ambaye aliona kwamba wimbo huo unafanana na ule wake wa 1989 kwa jina Express Yourself ambapo alioucheza aliweka nyimbo hizo pamoja katika ziara moja.

''Wakati ambao nilimkosoa Lady Gaga ni ule ambapo nilihisi kwamba ameimba wimbo kama wangu'', madonna alisema 2015.

''Sio kana kwamba anachukua nafasi yangu ama anachukua taji langi. Anaimba nyimbo zake. Sidhani kwamba ana kipaji kikubwa cha uimbaji ama mtunzi. Ni kisa hicho kimoja pekee''.

Mgogoro huo mmoja hatahivyo ulisababisha bifu ya miaka kadhaa.

Gaga ambaye kwa jina lake ni Stefani Germanotta- katika makala yake ya Five Foot Two, yaliotolewa mwaka uliopita , alisema kuwa hakufurahia kwamba Madonna hakuzungumza naye moja kwa moja.

''Licha ya heshima ninayompa sikudhania kwamba anaweza kusema kitu bila kukutana nami na kuniambia makosa yangu'', alisema.

3. Kanye West v Taylor Swift

Haki miliki ya picha Getty Images

Bifu kati ya Taylor Swift na Kanye West inaanzia 2009 - na hususan wakati wa tuzo za mwaka huo za MTV .

Kanye hakufurahishwa na ushindi wa Taylor wa kanda ya video ya mwaka kwa jina for You Belong With Me. Alidhani badala yake ni Beyonce aliyefaa kuibuka mshindi kupitia kanda yake kwa jina Single Ladies.

Na kama tunavyojua, Kanye sio mtu anayeficha hisia zake. Rapa huyo alipanda jukwani wakati wa hotuba ya Taylor ya kukubali ushindi huo, akachukua kipaza sauti na kiusema: Taylor nafurahi sana na nitakuwacha umalize lakini Beyonce alikuwa na kanda nzuri sana ya video katika historia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kim Kardashian West amemtetea mumewe wakati wa mgogoro na Taylor.

Wawili hao baadaye walikutana na kupatana, lakini miaka michache baadaye , West alidai katika kibao chake kwamba hatua aliyochukua ilimsaidia sana Taylor shift katika kazi yake.

Taylor alidai kwamba hakuyapatia baraka maneno ya wimbo wa West kabla utoke, lakini mkewe rapa huyo Kim Kardashian alichapisha ujumbe katika snapchat ambao ulioonekana ukimuonyesha Taylor akiubariki wimbo huo.

''Katika tuzo za Grammy , Swift alijibu: Nataka kuwaambia wasichana wote -kutakuwa na watu katika kazi yenu ambao watajaribu kukuvurugia ufanisi wenu ama hata kujisifu kwa manufaa yako ama hata umaarufu, aliwashauri: Endeleeni kufanya kazi zenu bila mtu kuwaingilia kati ili kuwavunja motisha.

Taylor baadaye alimkejeli Kanye katika wimbo wake Look What You made me do.

''Sipendelei jukwaa lako lililojuu chini, na jukumu ulilochukua'', aliimba.

4. Zayn v Naughty Boy

Haki miliki ya picha Getty Images

Mwaka 2015 , Zayn Malik alianza kufanya kazi na Naughty Boy - mtayarishaji ambaye ni maarufu kwa kwazi yake na Emeli Sande na Sam Smith.

Lakini ni vyema kusema kuwa yeye na Zayn hawakufanikiwa kufanya mazuki pamoja.

"Naughty Boy una mzaha sana wacha kujidai kwamba wewe ni rafiki yangu hakuna mtu anayekujua, Zayn alichapisha ujumbe wa Twitter baada ya kukosana wakati wa kurekodi.

Boy baadaye aliambia gazet la The Guardian kwamba kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 anatupatupa maneno na kwamba walikuwa wamekosana kutokana na ushawishi kutoka nje.

5. Azealia Banks v Iggy Azalea

Haki miliki ya picha Getty Images

Idadi ya nyota ambao Azealia Banks (kushoto) amekosana nao ni kubwa mno hali ya kwamba inaweza kuandika orodha.

Lakini mtu ambaye alikosolewa sana na mwimbaji huyo ni msanii Iggy Azalea.

Kwa wasanii wawili ambao walikuwa maarufu wakati mmoja na walikaribia kuwa na jina moja, walikuwa na tofauti kubwa na hawakuweza kulinganishwa kivyovyote.

Bifu yao ilianza wakati jarida la XXL lilipomuweka Iggy katika ukurasa wake wa kwanza wa jarida lao la kila mwaka ambalo linawaangazia wasanii wapya katika muziki kila mwaka.

Banks hakupendelea sana uamuzi uliochukuliwa na mhariri wa jarida hilo. Alisema kuwa jarida hilo lilikuwa limekosea kumweka Iggy na kuendelea kumshutumu kwa kukiuka tamaduni ya weusi.

Iggy Azelea alijibu kwa ksema: Huwezi kuzuia baraka zangu, leo nasherehekea, elewa ama jipange.

Mgogoro wao uliendelea kwa miaka kadhaa , huku Iggy akidai kwamba mwaka 2014 ufanisi wake mkubwa 2014 ndio sababu ya Banks kutaka kujipatia umaarufu.

6. Benzino v Eminem

Haki miliki ya picha Getty Images

Hakukukosa mgogoro wa Rap mapema miaka ya 2000. Nas na Jay Z. DMX na Ja Rule. 50 Cent dhidi ya marapa wengine wote.

Lakini mgogoro mkubwa kabisa ulihusisha majina makubwa katika sanaa ya muziki wakati huo na mwanamuziki mwingine ambaye hakuwa maarufu kwa jina Benzino - Mwanzilishi mwenza wa gazeti la mtindo wa hiphop la The Source.

Benzino aliachilia muziki uliomdhalilisha Eminem kwa jina Pull Your Skirt Up, ambao ulimtaja Eminem kuwa Vanilla Ice ya 2003 na kumlinganisha na mwanamke.

Eminem alijibu kupitia kibao chake Nail in the Coffin, ambapo alisema hakuna mtu anayetaka kumsikiliza babu yake akirap.

7. Lil' Kim v Nicki Minaj

Haki miliki ya picha Getty Images

Iwapo Rappa yeyote mpya ambaye ni mwanamke atawasili katika sanaa ya muziki huo na Lil Kim [juu[ hajaanza vita naye-basi hajawahi kuonekana.

Kim ana historia na Eve, Foxy Brown, Remy Ma na wengine wengi. Lakini hao walikuwa watu wadogo ikilinganishwa na Nicki Minaj kama ilivyoonekana.

Albamu ya Nicki kwa jina Pink Friday ilipata ufanisi mkubwa wakati ilipotolewa 2010 , lakini Lil Kim hakufurahia

Katika wimbo aliouweka katika mitandao ya kijamii kwa jina Black Friday, Kim alimtaja Nicki kuwa mtu amabaye anataka kuwa kama Lil Kim kwa kuwa anamuigiza

Minaj, alijibu kwa kumuita 'kahaba mjinga'.

8. Rihanna v Ciara

Haki miliki ya picha Getty Images

Cha kumalizia ni kwamba RiRi na CiCi, wote walianza muziki mwaka 2005 huku Ciara akipanda katika chati za muziki na wimbo wake Goodies ,Rihana naye akiwa katika nafasi ya pili na wimbo wake Pon De Replay.

Walikuwa wasichana wadogo waliokuwa na matumaini makubwa ya muziki wa R&B na pia walikuwa wakienda kujivinjari pamoja . lakini miaka michache baadaye mambo yalibadilika na kuwa mabaya

"Nilikutana naye hivi majuzi na hakuwa mzuri,"Ciara alisema 2011. "haukuwa mgongano mzuri." Baadaye walianza kujibizana katika mtandao wa Twitter.

Rihanna: "Ciana, je nilisahau kukupa ushauri.?"

Ciara: "Kweli Rihanna usingependelea kukutana nami mahala popote ama katika jukwaa.."

Rihanna: " We gangsta huh?... kila la kheri katika jukwaa unalozungumzia."

Lakini haikuchukua muda kabla ya Rihanna kurudi nyuma na kuandika: "Ciara baby, nakupenda! Ulinikosea sana katika runinga. Pole sana!"

Ciara alijibu: 'Rhi, unajua tumekuwa tukipendana tangu siku ya kwanza! Ulinikosea sana katika sherehe ile! msamaha wako umekubaliwa. Tuzungumze ana kwa ana."

Huoni kama huo ni upendo tuwe marafiki


Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii