Basila Mwanukuzi asema wanaokosoa Miss Tanzania wamejaa chuki
Huwezi kusikiliza tena

Wakosoaji wanadai zawadi ya gari iliyotolewa haiendani na hadhi ya taji la Miss Tanzania.

Muandaaji wa mashindano ya ulimbwende ya Miss Tanzania Basila Mwanukuzi ameiambia BBC kuwa wale wote wanaotoa kasoro mashindano ya mwaka huu, wanachuki na hawapendi maendeleo.

Mashindano hayo yamekuwa yakiyumba kwa miaka kadhaa lakini mwaka huu kumekuwa na mwamko wa kipekee.

Kilele cha mashindano hayo kilikuwa siku ya Jumamosi ambapo mlimbwende Queenelizabeth Makune aliibuka mshindi. Pamoja na vitu vingine, mlimbwende huyo alizawadiwa gari na waandaaji wa shindano hilo.