Mfanyibiashara anayekuza wavumbuzi wa siku zijazo nchini Ghana

Children at home using the science kit to help them do their homework
Image caption Watoto kutoka kote Ghana wana uwezo wa kutimiza ndoto zao za kisayansi

''Bwana, bwana, bwana'', waliita zaidi ya watoto 30 kwa msisimuko, wakitoka katika viti vyao vya mbao walivyokuwa wamekalia darasani mwisho wa bonde lililojaa nyasi

Shindano limeanza katika shule ya upili ya Berekuso Junior viungani mwa mji mkuu wa Accra Ghana, kuona ni nani atakayeunganisha msururu wa nyaya na transista ili kufanya kengele ndogo kupiga kelele.

Na baada ya sekunde chache chumba hicho kinatoa milio mingi. Watoto wanafurahia. Ni vigumu kusema ni nani aliyeibuka mshindi.

Mwaka mmoja uliopita, vijana hawa walikuwa wakifunzwa somo la elektroniki kupitia ubao mweusi ,chaki na vitabu kadhaa. Na sasa wana kila wanachohitaji mbele yao ili kuunda mzunguko wa stima.

Uvumbuzi wa kitabu cha maandishi

Charles Pfori Antipem, 25, ndiye anaongoza uvumbuzi huo.

Alivumbua kitabu cha maandishi , kijisanduku kidogo cheusi chenye ukubwa na bei ya dola kumi na tano {$15} ya kitabu cha maandishi kilichopo na umeme.

''Nilipoweza kuweka kitabu hicho mbele la dawati la wanafunzi hao na kuona furaha iliokuwa katika macho yao wakati walipotengeza kengele ya kwanza yaelektriki'', anasema. ''Hicho ndicho kinachotufanya sisi kuendelea''.

Charles alibuni teknolojia hiyo ya Dext katika kampuni yake miezi 18 iliopita.Kwa sasa ana wafanyikazi tisa, na kufikia sasa ameuza zaidi ya vitabu 5000 kwa serikali na shule za kibinafsi nchini Ghana.

Wazo hilo lilianza na mwenzake , Michal Asante Afrifa katika bweni lao katika chuo kikuu.wanataka kila mtoto nchini Ghana kumiliki kitabu kimoja katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

''Kupata elimu kutoka katika kitabu hicho ni kitu kimoja lakini kuweza kukijaribu na wanaokifanyia majaribio ndio kitu muhimu'', anasema.

Image caption Charles alibuni teknolojia hiyo ya Dext katika kampuni yake miezi 18 iliopita

Inatarajiwa kwamba miaka ya 2020 itakuwa muongo ambao watu watakuwa wakipata kazi kutokana na mafunzo ya somo la sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu.Hakuna anayejua ni idadi gani ya kazi duniani zitahitaji uzoefu wa masomo hayo , lakini inakadiriwa itakuwa takriban asilimia 80.

Lakini Afrika ya jangwa la sahara bado inasalia nyuma katika uwekezaji wa elimu ya masomo ya STEM na mafunzo yake. Kama jimbo la kivyake , Umoja wa mataifa unasema kuwa litahitaji wahandisi milioni 2.5 pekee ili kuafikia malengo yake ya maendeleo SDG kuimarisha uwepo wa maji safi na usafi.

Daktari Thomas Tagoe ,mwanachama wa muungano wa wanasayansi wa Ghana unasema kuwa kuwafanya watoto kupenda masomo ya sayansi ni muhimu kwa kuwa taifa hilo halina wahandisi wa kutosha na wataalamu wa teknolojia.

''Ni mwaka wa kidijitali na tunahitaji watu wanaoweza kutumia fursa hiyo'', anasema. 'Inamaanisha kwamba tunaweza kuondoka katika wimbi la taifa linaloendelea hadi katika kiwango kisichojulikana katika utalamu wa kisayansi'.

Sheria za sayansi

Charles alilelewa katika nyumba ambapo sayansi ilikuwa kila kitu.Babake aliyefariki miaka michache iliopita alikuwa mwalimu wa sayansi katika shule ya eneo walilokuwa wakiishi.

Kila mara alikuwa akitutaka kujifunza kila aina ya elimu tuliyopata hususan vitu vilivyohusika na sayansi.

Lakini Charles hakuwa na uwezo kupata mtandao ama sayansi ya msingi na vifaa vya kiteknolojia alipokuwa shule. 'Vifaa nilivyokuwa navyo ni mikono yangu', anasema akiongezea anataka kubadilisha hilo miongoni mwa wanafunzi wa sasa.

Image caption Kifaa hiki kinagharimu dola $15 tu

Nahisi kwamba kazi yangu ni kufanya niwezalo kuviwezesha vizazi vijavyo zaidi ya nilivyowezeshwa na babangu, ili kukabiliana na changamoto kubwa zinazotarajiwa siku za usoni

Saa sita kaskazini magharibi mwa Berekuso, katika karakana moja ndogo ya teknolojia mjini Kumasi, kundi la Charles linaendelea kutengeneza vitabu hivyo vya sayansi.

Wanaunganisha maelfu ya nyaya ndogo katika transista.

'Sasa, hivi ndivyo ilivyo', anasema Charles kwa majivuno akibeba kijisanduku hicho cheusi. Anatuonyesha mwongozo, vifaa vya kielektroniki , kisanduku hicho , vioo na katikati yake ni betri zinazotumika kukiwasha.

Charles anatarajia simu kutoka kwa mteja muhimu ambaye anataka kuzindua vitabu hivyo vya kiteknolojia katika shule zilizopo katika eneo la mashamba ya Cocoa katika taifa jirani la Ivory Coast

Ni muuzaji anayependa kazi yake, akijibu maswali kwa urahisi.Huku akikatiza simu hiyo anaonekana anatabasamu. 'Ilikuwa simu nzuri', akilezea kwamba wamekubaliana kununua vibau vichache vya majaribio . 'Hatua hiyo inaweza kuvutia maagizo zaidi ya vitabu hivi ama uwkezaji zaidi wa vitabu hivi vya sayansi', anasema.

Tukirudi mjini Berekuso katika barabara iliojaa vumbi kilomita chache kutoka shule, Princess makafui mwenye urmi wa miaka 15 ameketi na marafikize wa shule wakifanya kazi ya shule.

Image caption Princess Makafui na wenzake walishinda wakitimia kifaa hicho

Familia yake ni maskwota katika nyumba ambayo hakimalizwa kujengwa .haina kuta zote mbali na umeme.Jua limeanza kutua na sasa wanalazimika kufanya kazi kwa kutumia taa moja iliowekwa katikati ya meza ambayo walivumbua wenyewe.

'Ni taa ya mshumaa', Princess anasema kwa majivuno. 'Inamaanisha kwamba tunaweza kutumia upande mmoja wa mshumaa huo kufanya kazi zetu za shule'. Prinecss na kundi lake la wasichana 12 waliibuka washindi wa shindano la sayansi kwa uvumbuzi wao. Waliunda kwa kutumia kijitabu cha sayansi.

'Kabla ya vitabu hivyo vya kisayansi, somo letu la sayansi lilikuwa linakera kwa kuwa kila kitu kilikuwa kikifanyika kupitia kusoma', anasema.

Kwa Charles, wazo hilo kwamba analea vizazi vijavyo vya uvumbuzi ni kitu ambacho alitumai kufanya.

'Kwa kuwaona wanafunzi wakivumbua kwa kutumia vitabu vyao vya sayansi ni kitu ambacho tumejaribu kuthibitisha.'

'Unapowapatia wanafunzi vifaa, wataanza kutafuta suluhu kwa matatizo yanayowakabili kwa kutumia teknolojia hiyo'.

'Mvumbuzi anayewakuza wavumbuzi?' Anatabasamu.'Ikiwa babangu angekuwa hapa angejivunia sana'.

Makala hii ya BBC imetayarishwa na wakfu wa Bill & Melinda gates