'Mchoro jadi unaofahamika' umepatikana kwenye kipande cha mawe Afrika Kusini

The oldest-known drawing, painted in ochre pigment on a small stone Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchoro huu ni wa tangu miaka 73,000 iliyopita

Wanasayansi wanasema kuwa wamevumbua mchoro wa kale katika kipande cha mawe nchini Afrika Kusini.Mchoro huo ambao unasadikiwa kuwa na karibu miaka elfu sabini na tatu unaonyesha mistari iliyochorwa kwa rangi nyekundu ambayo imejificha katika vigaya vya ndani ya kipande hicho cha mawe.

Baadhi ya wanasayansi wanasema kipande hicho cha mawe kilicho na mchoro unaofanana na alama ya reli kimepatikana katika pango la Blombos katika pwani ya kusini mwa kusini.

Ripoti mpya kuhusiana na utafiti huo uliyochapishwa katika toleo la Jumatano la Journal nature inasema uvumbuzi huo ni ''kiashiria cha kwanza cha ufahamu wa ki sasa '' kwa binaadamu.

Japo wanasayansi washawahi kupata mchoro aina nyingine duniani, utambuzi huu wa sasa unatajwa kuwa wa kipekee katika historia.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanasayansi wamepata kipande cha mawe ndani ya pango la Blombos,kilomita 300 (maili 185) mashariki mwa mji wa Cape Town

Binadamu wametumia mabaki ya mawe hayo kwa karibu miaka 285,000.

Mtaalamu wa vitu vya kale,Christopher Henshilwood ameiambia shirika la habari la Reuters kwama mchoro huo huenda ulikuwa mgumu sana kuchora.

Mungo Man: Mabaki ya kale zaidi ya binadamu yapelekwa nyumbani Australia

"Kukomeshwa ghafla kwa mistari yote kwenye sehemu za mviringo inaonyesha kuwa mchoro huo ulikuwa undelezwa katika sehemu kubwa ," he said.

Bwana Henshilwood ambaye anafanya kazi katika chuo kikuu cha Bergen nchini Norway pamoja na chuo kikuu cha Witwatersrand, nchini Afrika Kusini ambaye aliyewaongoza wanasayansi wenzake katika utambuzi wa mchoro huu amesema hawezi kuuita usanii kwa sababu sehemu ya kazi yenyewe inatoa maana ya kimaumbile yanayotokana na Mungu.

Kumekuwa na vitu vingine vya kale ambavyo vimepatikana ndani ya pango la Blombos, kilomita 300 sawa na maili 185 mashariki mwa mji wa Cape Town, ikiwa ni pamoja na shanga zilizofunikwa kwa mchanga mwenkundu uliyokuwa umejikusanya katikati ya mawe pamoja na kifurushi cha kutengeneza rangia mbacho kunasadikiwa kuwa mahali hapo kwa zaidi ya miaka 100,000.

Binadamu wa kisasa ambaye hufahamika kama 'homo sapiens' inaaminika alianza kuwepo duniani zaidi ya miaka 315,000 ambayo sasa ni Afrika.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii