Kimbunga Florence: Kimbunga hatari chatua North Carolina

Mhudumu ambeba mtoto Haki miliki ya picha Getty Images

Kimbunga Florence kinachoandamana na upepo mkali na mvua kubwa hatimaye kimetua katika pwani ya mashariki ya Marekani. Onyo limetolewa kwamba mvua hiyo huenda ikasababisha mafuriko makubwa.

Ufukwe wa Wrightsville umekumbwa na upepo mkali unaovuma kwa kasi ya kilomita 150 kwa saa.

Mamia ya watu katika mji New Bern wanasubiri kuokolewa.

Zaidi ya watu milioni moja wetakiwa kuondoka katika makazi yao kuelekea maalumu yaliyotengwa.

Kwa mujibu wa shirika la kutoa huduma za dharura karibu nusu ya miundo mbinu ya umeme imeharibiwa na kimbunga hicho katika maeneo kadhaa ya Carolina.

Maafisa wameonya kwamba huenda mawimbi makubwa ya kutoka baharini na mvua kubwa ikaathiri maeneo ya North na South Carolina, huku kimbunga hicho kikielekea maeneo ya bara.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gavana wa North Carolina Roy Cooper amesema kimbunga hicho ni cha "kihistoria"

Upepo wa kimbunga hicho unavuma kwa kasi ya maili 100 kwa saa (155 km/h).

Nyumba takriban 100,000 tayari hazina huduma ya umeme huku hali ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi.

Maafisa wa serikali wametahadharisha kwamba kimbunga hicho kinaweza "kuwaua watu wengi sana" huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea mafuriko "mabaya sana".

Watu zaidi ya milioni moja katika maeneo ya pwani North Carolina, South Carolina na Virginia walikuwa wametakiwa kuyahama makazi yao.

Maelfu walitafuta hifadhi katika vituo vya muda vya huduma za dharura Alhamisi usiku.

Hali kwa sasa ikoje?

Hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi Alhamisi huku upepo ukiongeza nguvu kiasi katika maeneo ya pwani.

Katika baadhi ya maeneo ya North Carolina mvua ya kina cha futi moja ilinyesha katika kipindi cha saa kadha, na picha zilionyesha maji yakijaa baharini na kufunika maeneo ya ufukweni.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu wanaokimbia makwao wakitafuta hifadhi Wilmington, North Carolina

Sasa Kimbunga Florence ni cha kiwango cha pili na hakujakuwa na dalili zozote za kupunguza nguvu kwenye kitovu chake kabla ya kufika maeneo ya bara Ijumaa asubuhi.

Watabiri wa hali ya hewa wametahadharisha kwamba maji ya mafuriko huenda yakafikia kina cha futi 13 (mita 4) na katika baadhi ya maeneo, huenda upepo mkali ukasababisha maji ya mito kuanza kurudi nyuma.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wakifunga madirisha ya nyumba zao Wrightsville Beach wakijiandaa kuhama

Safari 1,400 za ndege zimefutwa kwa mujibu wa FlightAware.com, kwani viwanja vingi vya ndege maeneo ya pwani vitaathiriwa.

Kuna kimbunga kingine?

Maafisa katika jimbo la Hawaii wamewatahadharisha wakazi kuhusu kimbunga kingine kwa jina Olivia.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema Olivia - kimbunga chenye upepo unaovuma kwa kasi ya maili 65 kwa saa, kitafikia maeneo ya bara Jumatano asubuhi na kusababisha mvua kubwa.

Mada zinazohusiana