Airgate Centre: Hatimaye serikali imeanza kulibomoa jumba kubwa lililojengwa katika ardhi ya barabara Kenya

Ubomozi wa jumba la Nakumatt Ukay mjini Nairobi

Jumba la Airgate Centre ambalo likijulikana kuwa Taj Mall,limeanza kubomolewa mapema juma mosi asubuhi.

Shughuli hiyo ya ubomozi ni sehemu ya juhudi ya seriklai ya Kenya kutwaa sehemu uliyotengewa ujenzi wa barabara na yaliyo kwenye kingo za mito na chemchemi.

Mmiliki wa jumba hilo ,Ramesh Gorassia alikuwa amepewa muda wa siku 14 kulibomoa mwenyewe lakini alikataa kufanya hivyo akisisitiza kuwa alifuata taratibu zote za kisheria.

Maafisa wa usalama wameimarisha doria kuhakikisha shughuli hiyo iliyoanza mwendo wa saa kumi na mbili unusu asubuhi haitatizwi na yeyote.

Maafisa hao pia walilazimika kutumia gesi ya machozi kuwatawanya watu waliyojaribu kubeba vitu kuto eneo la ubomozi huo.

Siku chache zilizopita, Mwenyekiti wa jopo maalum la kushughulikia ubomoaji huo, Moses Nyakiongora na Afisa wa Kaunti ya Nairobi, Julius Wanjau, walisema shughuli ya kulibomoa jengo hilo ambalo limejengwa eneo lililotengewa barabara ingeanza baada ya kukamilisha kabisa ubomoaji wa majumba mengine kama vile Southend Mall.

Jumba la Southend Mall lilibomolewa Agosti 9 baada ya kubainika kuwa mto Ngong ulikuwa unapita kati ya jumba hilo na jengo lingine ambalo halikuwa na watu.

Wamiliki wa jumba hilo walikuwa wamejenga eneo la kuegesha magari juu ya mto huo.

Serikali iilikuwa imesema wamiliki wa majumba hayo watagharamia ubomozi huo

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii