Tetesi za soka Ulaya Jumapili 16.09.2018: Mourinho, Messi, Paulo Dybala, David Luiz, Aleksandar Mitrovic

avid Beckham na timu yake mpya ya Marekani Inter Miami
Image caption David Beckham na timu yake mpya ya Marekani Inter Miami inamtaka mchezaji wa FC Barcelona

Mchezaji David Beckham na timu yake mpya ya Marekani Inter Miami inamtaka mchezaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi mwenye umri wa miaka 31 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Marekani Major League Soccer mwaka 2020. ( Mail Jumapili)

Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anapanga mwezi January kupata saini ya mchezaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil mwenye umri wa miaka 29. (Sunday Express).

Klabu ya Juventus ya Italia imepanga kumtoa mshambuliaji wake raia wa Argentina Paulo Dybala akajiunge na klabu ya Manchester United kwa kubadilishana na mchezaji wake wa zamani Paul Pogba katika makubaliano yanayoweza kufikia paundi milioni 150. (Sunday Mirror).

Katika hatua nyingine Paul Pogba ameonesha nia ya kuongeza mkataba wake katika klabu hiyo ikiwa tu kocha Jose Mourinho atatimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na mfaransa Zinedine Zidane. (CaughtOffside).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Luiz anaweza kuongezewa mkataba

Klabu ya Chelsea imefungua milango ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili beki wa kati wa Kibrazili mwenye umri wa miaka 31 David Luiz, ambaye mkataba wake wa sasa unaisha wakati wa kipindi cha majira ya joto. (Sun on Sunday).

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola atakuwa anawatazama kwa karibu wachezaji wawili wa klaby ya Lyon ya Ufarabsa Luca Tousart na Tanguy Ndombele wakati timu hiyo itakaposafiri kwenda Etihad siku ya Jumatano. Wachezaji hawa wawili kinda wa Ufaransa wote wenye umri wa miaka 21 imeripotiwa wamekuwa wakifuatiliwa na vilabu kadhaa vya Ulaya. (Star on Sunday).

Klabu ya Juventus imetoa kiasi paundi milioni 53.4 kwa klabu ya Fiorentina ili kupata saini ya mchezahi Federico Chiesa wakati wa majira ya joto. Mshambuliaji huyu mwenye umri wa maiaka 20 raia wa Italia amekuwa akihusishwa pia na klabu ya Manchester United na Chelsea. (Calciomercato).

Chelsea pia imeriptiwa kuwa inampango wa mshambuliaji wa Fulham mwenye umri wa miaka 23 Aleksandar Mitrovic. Mchezaji huyu wa kimataifa wa Serbia amewavutia tangu ajiunge na klabu hiyo kutokea Newcastle kwa dau la paundi milioni 22. (Sunday Mirror).

Klabu ya Barcelona inamuwinda mchezaji Frank de Jong mwenye umri wa miaka 21 ambaye ameonesha nia ya kujiunga na miamba hiyo ya Uhispania, kiungo huyu wa Ajax ya Uholanzi akikiri kuwa angependa kucheza pamoja na Leonel Mess. (Sunday Mirror).

Klabu ya Inter Milan ya Italia inajiandaa kumuomba mshambuliaji kinda wa Manchester United Anthony Martial kwa mkopo mwezi January, ingawa uhamisho huu huenda ukaifanya klabu ya United kumtaka winga raia wa Croatia Ivan Perisic kwa kubadilishana. (Star on Sunday)

Image caption Kiungo wa kidachi anayechezea klabu ya Liverpool Georginio Wijnaldum

Kiungo wa kidachi anayechezea klabu ya Liverpool Georginio Wijnaldum mwenye umri wa miaka 27 amesema alikataa ofa kutoka kwa klabu ya Tottenham na kuamua kujiunga na Liverpool akitokea Newcastle mwaka 2016. (Metro).

Kiungo wa Chelsea N'Golo Kante mwenye umri wa miaka 27 wamesema kuna mawasiliano na klaby ya PSG ya Ufaransa kwenye majira haya lakini kiungo huyu wa Ufaransa amesema anafuraha kusalia kwenye klabu yake ya sasa. (ESPN).

Mchezaji wa zamani wa klabi ya Everton Wyne Rooney amesema kuwa anaamini mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshir alikuwa hataki aendelee kubaki klabuni hapo hali iliyochangia aende kujiunga na klabu ya Marekan ya DC United. (Mail on Sunday)

Rooney pia ameripotiwa anataka kumfuata mchezani mwenzake wa zamani wa Uingereza Steven Gerrard mwenye umri wa miaka 38 na Frank Lampard mwenye umri wa miaka 40 kwenye kazi ya kufundisha wakati atakapoamua kutundika daruga. (Sunday Times - Subscription required).

Kocha wa zamani wa West Ham David Moyes amesema alisikitishwa kwa kutopewa nafasi ya kubakia kwenye klabu hiyo baada ya kufanikiwa kuwabakisha kwenye ligi kuu msimu uliopita, lakini bado anaamini kuwa yeye ni miongoni mwa makocha bora. (Sun on Sunday).

Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Chelsea Eden Hazard anaweza kuwa mchezaji bora wa Ulaya katika kipindi cha miaka miwili, kocha wake Maurizio Sarri amesema baada ya mchezaji huyu wa kimataifa wa Ubelgiji kufunga mabao matatu katika mchezo wa timu yake dhidi ya Cardiff. (Sky sport)

Kocha wa Chelsea Rafael Benitez amesema hataki kujipa presha baada ya timu yake ya Newcastle kupata kipigo cha tatu kwenye uwanja wake wa nyumbani. (Newcastle Chronicle).

Image caption Kocha wa Aston Villa Steve Bruce

Kocha wa Aston Villa Steve Bruce amesema anaweza kuelewa lawama ambazo anatupiwa na mashabiki wa timu hiyo ambao wanataka afutwe kazi baada ya timu yake kutoka sare na Blackburn. (Birmingham Mail).

Mchezaji mkongwe wa klabu ya Roma na Italia Daniele de Rossi mwenye umri wa miaka 35 amesema anafikiria kuhama na kwenda kucheza ligi kuu ya Marekani MLS. (Goal.com).

Beki wa kushoto wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza Kieran Trippier mwenye umri wa miaka 27 amesema hatua ya kuruhusiwa na klabu yake ya Manchester City kuondoka ilikuwa na athari kwake lakini kujiunga na klabu ya Burnely ulikuwa ni uamuzi sahihi aliowahi kuufanya. (Mail on Sunday).

Kocha wa klabu ya Brighton Chris Hughton amekiri kuwa huenda akafanya kampeni mbaya, hata ikiwa na maana kuwa ni kupambana ili kubaki kwenye ligi kuu. (Argus).

Mada zinazohusiana