Usingizi wa pono: Kulala bila nguo kuna hatari zozote?

usingizi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kila mtu huwa ana namna yake ya kulala ambayo anajiona kuwa yuko huru

Takwimu zinaonesha kwamba idadi kubwa ya vijana, na hasa Ulaya, huwa hawavai nguo ya aina yoyote ile wanapolala.

Je, kuna madhara au manufaa? Unafaa kulala bila nguo?

Mtaalam wa usingizi Dkt Nerina Ramlakhan ameambia BBC kwamba kuna faida ambazo mtu anaweza kuzipata akivaa nguo za kulalia wakati anapolala.

"Kila mtu ana upekee wake na kila mtu ana namna yake ya kulala ambayo anaona huwa inampa uhuru au raha. Kuna baadhi ya watu hawapendi kulala bila nguo huku wengine huwa hawajali kabisa," Dkt Ramlakhan.

Anaongeza kwamba kila mtu huwa anahitaji kiwango cha joto ambacho kwake kinamfanya aweze kulala vizuri, na kwa kawaida huwa chini kidogo ya kiwango cha joto mwilini.

Anashauri kuwa kama unavaa nguo wakati wa kulala au huvai ni vyema kutumia kitanda chenye godoro zuri, na vilevile vazi zuri la kulalia ni lile la nguo nyepesi.

Je, kuna ubaya wa kulala bila nguo?

Dkt. Ramlakhan anasema kwamba hawezi kufikiria sababu yoyote mbaya inayohusisha mtu kulala bila nguo… 'kama mtu unajisikia vizuri kulala bila nguo basi ni vyema kufanya hivyo'.

Ukilala bila nguo unaweza kujihisi huru zaidi.

Hata hivyo, changamoto hutokea ukiwa ugenini.

Ni vyema kuzingatia kama unaweza kuwakwaza watu wengine ambao labda umelala nao, kwa mfano iwapo utalazimika kuamka kwa dharura usiku.

Unaweza pia kuwa makini kwa kuamka mapema kabla ya watu wengine kuamka, iwapo kwa mfano umelala eneo la wazi ambapo wenyeji wako pia wanatumia.

Haki miliki ya picha THINKSTOCK

Mambo 5 yanayoweza kukufanya ulale vizuri

  1. Kupata kiamsha kinywa ndani ya nusu saa au saa moja baada ya kuamka, haswa kama unajisikia uchovu. Ni muhimu kula kitu ili kutuliza mzunguko wa damu na sukari.
  2. Punguza unywaji wa kahawa au vinywaji vingine vyenye kafeini kwa kula chakula kama mbadala wake.
  3. Kunywa maji kwa wingi; Maji katika mwili huchukua asiliia 60 hivyo ni vyema unywe lita mbili za maji kila siku. Maji ya matunda(juice) pia ni mazuri lakini sio chai au kahawa.
  4. Jitenge na matumizi ya simu wakati wote mchana, pumzisha macho kiasi. Usilale na simu yako karibu au kuiwasha simu kuwa ndio kitu cha kwanza unafanya asubuhi.
  5. Lala mapema mara tatu au nne kwa wiki. Si lazima ulale moja kwa moja, unaweza kusoma kitabu au kufikiria jinsi siku yako ilivyokuwa.

Unaweza kusoma pia:

Mada zinazohusiana