Afrika kusini yaidhinisha lugha ya kiswahili kufunzwa shuleni

Afrika kusini imeidhinisha lugha ya kiswahili kufunzwa shuleni kuanzia 2020 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Afrika kusini imeidhinisha lugha ya kiswahili kufunzwa shuleni kuanzia 2020

Kiswahili kitaanza kufunzwa katika shule nchini Afrika kusini kuanzia mwaka 2020.

Waziri wa elimu msingi, Angie Motshekga siku ya Jumatatu amesema kuwa Kiswahili kitafunzwa kama lugha mbadala kwa wanafunzi nchini humo.

Tanzania inashikilia nafasi ya ngapi kwa utajiri Afrika?

Kwa mujibu wa taarifa kwenye vyombo vya habari nchini humo, Motshekga ameeleza kwamba uamuzi huo umeidhinishwa na baraza la mawaziri kuhusu masuala ya elimu na kwamba Kiswahili kitafunzwa katika shule za umma za kibinafsi na za kujitegemea.

Haki miliki ya picha @DBE_SA
Image caption Waziri wa elimu msingi Afrika kusini Angie Motshekga

"Kiswahili kina nguvu kupanuka katika nchi ambazo hazijawahi kukizungumza na kina nguvu ya kuliunganisha bara la Afrika," Motshekga amesema.

Kiswahili ndiyo itakuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika inayotoka nje ya Afrika kusini, kufunzwa katika nchi hiyo.

Kifaransa, Kijerumani na hata Mandarin ndio miongoni mwa lugha za nje zinazofunzwa kama lugha mbadala katika shule Afrika kusini.

Bi Motshekga amesema Kiswahili ndio lugha inayozungumzwa pakubwa barani Afrika, baada ya kiingereza na kiaarabu.

"Ni mojawapo ya lugha rasmi za Muungano wa Afrika.

Tanzania kati ya nchi raia hawana furaha duniani

Bia husaidia watu 'kufungua roho'

Tuna imani kuwa kutoa mafunzo ya kiswahili Afrika kusini kutasaidia kuleta uwiano wa jamii na Waafrika wenzetu," Bi Motshekga ameongeza.

Mwezi uliopita, kiongozi wa upinzani nchini humo Julius Malema alisema Kiswahili kinasathili kuendelezwa kiwe kinatumika katika mabara yote, kama sehemu ya 'kuondosha utawala wa ukoloni' Afrika.

"Ni lazima tuwe na lugha inayotuunganisha Waafrika... Tuache kuzungumzishana kiingereza," alisema.

Kiswahili nilugha ya Kibantu iliyo fananan na lugha nyingine nyingi zinazozungumzwa barani Afrika.

Mnamo Mei mwaka huu, mtandao mkubwa wa kijamii Twitter ulitambua rasmi Kiswahili kama lugha, na kukifanya kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutambuliwa kwa heshima hiyo.

Kampeni kwa kutumia #TwitterRecognizeSwahili ilishinikizwa na wakenya kadhaa kwa muda mrefu , kuitaka Twitter iitambue lugha hiyo rasmi.

Kiswahili kinavyopenya mipaka Afrika

Zaidi ya watu milioni 15 hutumia lugha hiyo kama lugha ya kwanza huku nchi nyengine wakitumia Kiswahili kama lugha ya pili au ya tatu.Ni lugha rasmi ya muungano wa Afrika.

Haki miliki ya picha YASUYOSHI CHIBA

KENYA

Kiswahili nchini Kenya ni lugha rasmi na pia ni lugha ya Taifa. Rais wa kwanza wa taifa la Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta alitoa kauli kwamba Kiswahili kinafaa kutumika kama lugha rasmi ya Kenya mwaka 1969.Mwaka 1975 kiswahili kilianza kutumika bungeni.

Serikali ya Kenya ilianzisha somo la Kiswahili katika Idara ya Lugha za Kiafrika na Isimu ya Chuo Kikuu cha Nairobi.

Huwezi kusikiliza tena
Kiswahili chakaribia kuwa lugha rasmi Rwanda

TANZANIA

Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzania na inatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa.

Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu.

Vyombo mbalimbali vimeubuniwa kama Bakita, Bakiza, Takiluki, Taasisi ya Elimu, Uwavita na Ukuta. Pia vyuo vikuu mbalimbali vya Bara na Visiwani vilianza kusomesha Kiswahili kuanzia shahada ya kwanza, ya uzamili na uzamivu.

RWANDA

Kiswahili ni lugha rasmi nchini Rwanda. Kabla mwaka 1994 , wakati wa mauaji ya kimbari lugha ya kiswahili ilizungumzwa kwenye mji tofauti .

Lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19.

Mwaka wa 1976 -1977 lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa katika shule za upili na chuo Kikuu Cha Rwanda.

Haki miliki ya picha FREDERIC DE LA MURE

UGANDA

Mwaka 1960, Serikali ya Uganda iliruhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini humo; Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima.

Lugha ya maandishi ya Kiswahili yalianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro, hata kabla ya ukoloni (1862). Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila.

Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Lakini Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi

Wikendi hii Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, Keneth Cimara imeipongeza serikali ya Uganda kwa juhudi ya kuendeleza Kiswahili tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Huwezi kusikiliza tena
Mwanamuziki anayevumisha Reggae ya Kiswahili

Katika warsha ya siku mbili iliyokamilika mwishoni mwa juma katika hoteli ya Imperial Royal mjini Kamapla iliyowajumuisha walimu wa vyuo vikuu, shule za upili na taasisi mbalimbali nchini Uganda.

Keneth Cimara amesema miaka ya themani raia wengi wa Uganda walikiona Kiswahili kama lugha ya wahalifu ikitumiwa na askari kuwanyanganya mali zao, aidha kuwatendea uhalifu.

Haki miliki ya picha AFP

Cimara ameongeza kwamba sasa Serikali ya Uganda ni miongoni mwa mataifa ya Jumuia ya Afrika mashariki ambayo yameweka mikakati ya kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahi kama anavyosema tena Katibu mtendaji.

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Kiswahili kiliingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuanzia karne ya 19.Kiswahili kilianza kuenea kutoka Mashariki mwa nchi hiyo ,kuelekea kandokando ya mto Kongo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii