Bangi: Kauli kinzani zatolewa baada ya bangi kuhalalishwa Afrika kusini

Wanaharakati wanaounga mkono itumiaji wa bangi walionekana wakisheherekea uamuzi huo wa mahakama Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanaharakati wanaounga mkono itumiaji wa bangi walionekana wakisheherekea uamuzi huo wa mahakama

Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika kusini imehalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi wamesheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''.

Akitoa hukumu hiyo Naibu jaji Mkuu, wa Afrika Kusini, Raymond Zondo, amesema sheria inayopiga marufuku watu wazima kutumia bangi ilikuwa kinyume cha katiba.

Serikali ya Afrika kusini bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na na uamuzi huo.

Watumiaji watatu wa bangi walikuwa wanakabiliwa na mashtaka walijitetea mbele ya mahakama hiyo wakisema '' mashataka dhidi yao yaliingilia uhuru wao''

Naibu jaji mkuu Raymond Zondo alisema: "Sio hatia kwa mtu mzima kutumia au kugusa bangi akiwa katika eneo la faraghani hasa ikiwa anafanya hivyo kwa maatumizi yake ya kibinafsi''

Licha ya uamuzi huo, ni hatia kwa mtu kuvuta au kuuza bangi hadharani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bunge litatatoa uamuzi ni kiwango gani cha bangi watu wanastahili kuwa nacho

Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini limeunga mkono uamuzi wa mahahakama dhidi ya matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.

Jeremy Acton, kiongozi wa chama cha Dagga, ambacho kinaendesha kampaini ya kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi pia kimepongeza uamuzi huo wa mahakama ya katiba kimesema uamuzi huo pia ungelijumuisha kuhalalisha ubebaji wa bangi hadharani.

Bangi hutambuliwa kama "dagga"nchini Afrika Kusini.

Je unazifahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa?

Lesotho

Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.

Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini

Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa.

Tangu mwezi machi mwaka 2017, baada ya mahakama kuu ya Western Cape kuhalalisha matumizi ya bangi majumbani bado matumizi yake ni kinyume cha sheria, mpaka pale sheria itakapobadilishwa kuruhusu wafanyabiashara walime na kuwekeza kwenye kilimo cha bangi, vivyo hivyo kwa makampuni kutengeneza bidhaa zitokanazo na bangi na mawakala kusambaza bidhaa.

katika kipindi cha miezi kadhaa nyuma, wale walioonyesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha bangi wameleta maendeleo makubwa kufungua milango katika uzalishaji wa bangi kwa ajili ya dawa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi

Ghana

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .

kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.

pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.

Korea Kaskazini

Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii