Yusaku Maezawa: Bilionea wa Japan kuzuru kwenye mwezi

Yusaku Maezawa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bilionea wa Kijapani Yusaku Maezawa

Bilionea wa Kijapani Yusaku Maezawa alionekana kwa mara ya kwanza katika umma kama mpiga ngoma wa bendi ambaye hakuwa na mvuto wowote .

Maezawa ameweza kutengeneza fursa za utajiri wake kupitia shughuli za mitindo mtandaoni,na ameweza kujulikana zaidi nje ya Japan kwa kuweka rekodi ya kutumia mamilioni ya Dolla.

Kwa sasa bwana Maezawa anatamani kuwa abiria wa kwanza kusafiri kwenye mwezi na hii ikiwa ni sehemu ya matarajio yake katika mpango alionao na Elon Musk's SpaceX.

Nyota huyo wa kijapan amepanga kuongozana na kundi la wanamuziki katika safari yake ya mwezini itakayofanyika mwaka 2023 anataka kuongozana na kundi la wasanii.

Maezawa, mwenye umri wa miaka 42,hajafahamu bado ni kiasi gani cha fedha anapaswa kukilipa kwa safari hiyo ambayo itawaunganisha pamoja na mabilionea wengine wawili ambao hawajulikani sana duniani.

Mjapani huyo aliyeanza kama mjasiriamali wa kuuza CD kwa ajili ya kurekodia ambazo zilikuwa adimu kupitia kampuni aliyoianzisha mwaka 1998 ikijulikana kama Start Today.

''Nilikuwa rais wa kampuni yangu wakati nikifanya ziara ya kuzunguka nchi nzima pamoja na kundi langu'' ,alililambia gazeti la Japan Times mapema mwaka huu na inapokuja suala la kuchagua nilichagua kampuni yangu wakati huo nikiwa na umri wa takribani miaka 25 au 26.

Haki miliki ya picha yusaku2020
Image caption Yusaku Maezawa aliweka picha hiyo katika kurasa yake ya Instagram na kuandika "mzimu wa Jean-Michel Basquiat unakuja Japan"

Maezawa alizindua mitindo kwa ajili ya mauzo ya rejareja katika mji wa Zozo mwaka 2004 wakati huo akiwa na umri wa katikati ya miaka 30

Jarida maarufu la Forbes limemuorodhesha kama mtu tajiri namba 18 nchinni Japani akiwa utajiri binafsi wa dola za kimarekani bilioni 2.9.

Kampuni yake kwa sasa imekuwa ikigonga vichwa vya habari baada ya kubuni shati la kubana(bodysuit ) ambayo wateja wanaweza kuweka vipimo vyao halisi wakati wakifanya manunuzi katika mtandao

Maezawa amefanikiwa kufanya ubunifu wa kipekee wa kisasa na wenye ngazi ya hali ya juu kwenye mnada aliolipia kiasi cha dola milioni 110.5 kununua mchoro wa msanii wa Kimarekani Jean-Michel Basquiat na kuiweka katika makumbusho ya Chiba katika mji wake alipozaliwa.

Mwaka 2016 ,Maezawa alilipa kiasi cha Dola milioni 57.3 kwa ajili ya kazi nyingine za sanaa,

Pamoja na kuwa na utajiri au mauzo yake kuwa ya juu,Maezawa anasema amekuwa akisukumwa na kazi nzuri za sanaa ambayo imekuwa ikitumika lakini pia ujuzi wa wasanii na namna ya maisha yao yalivyokuwa yanaendelea.

Watatakiwa kubuni kitu mara tu baada ya kurudi kutoka mwezini, kitu ambacho kitakachowahamasisha watu wengine wenye ndoto kufanya hivyo kwa siku zijazo,Mtaalam mmoja wa masuala ya anga aliwaambia waandishi wa habari.

Maezawa amekubali kulipa gharama zote za tiketi kwa ajili ya safari hiyo kiasi ambacho hakikuwekwa wazi kwa sasa, huku bado kukiwa na wasiwasi kuwa iwapo kama Maezawa na kundi lake wataweza kufanikiwa juu ya azima hiyo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii