Maswali mengi yazuka kuhusu begi alilosafiri nalo Bobi Wine kurudi Uganda

Bobi Wine akiondoka Marekani Haki miliki ya picha BOBI WINE/ TWITTER
Image caption Bobi Wine akiondoka Marekani

Bobi amewasili Uganda kutoka Marekani, alikokuwa amekwenda kupokea matibabu. Lakini hilo sio kubwa kwa baadhi kuhusu safari ya mwanasiasa huyo wa upinzani, lakini badala yake kuna kitu kilichoteka hisia zao.

Kumezuka mjadala kuhusu begi alilosafiri nalo mbunge huyo wa Kyadondo.

Katika mojawapo ya picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Bobi Wine anaonekana akiwa katika uwanja wa ndege akisubiri kuabiri ndege.

Macho yameelekezwa kwenye begi lililokuwa karibu naye ambalo ni la nembo ya bidhaa za kifahari - Luis Vuitton.

Begi hilo limezusha mgawanyiko wa hisia miongoni mwa walio wafuasi na wasio wafuasi wa Wine.

Image caption Bobi Wine akielekea Entebbe kutoka uwanja mkuu wa ndege JKIA mjini Nairobi

Swali kubwa lililoulizwa ni je, iwapo Museveni anawakandamiza Waganda wasiendelee, ni vipi basi Bobi Wine anavyojipatia mali nyingi kiasi cha kumuwezesha kuishi katika kasri, kuendesha magari ya kifahari na kubeba mabegi yenye thamani, kama hili la Luis Vuitton?

Halikupokewa vyema upande wa pili na walio wafuasi wake kiongozi huyo wa upinzani.

Baadhi walikuwa wepesi kuusahihisha ujumbe katika mtandao wa Twitter uliokuwa unasambaa, wengine angalau kwa kejeli.

LV nembo ya ufahari

Lakini je begi lenyewe, ni LV halisi au ni muigo wake?

Louis Vuitton Malletier, ambao kwa umaarufu hufahamika kama Louis Vuitton au kifupi LV, ni kampuni ya mitindo ya kifahari kutoka nchini Ufaransa, na yenye matawi katika mataifa tofauti duniani.

Kwenye mtandao mabegi ya safari ya LV bei yake ni kati ya $ 1200 hadi $ 3000.

Wapo wanaonunua bidhaa za moja kwa moja zenye thamani hiyo kutoka kwenye maduka ya kifahari kama LV na kadhalika.

Lakini pia kuna biashara ya bidhaa ghushi zilizoundwa kwa mfano wa za kama LV zinzoingizwa katika mataifa sanasana kutoka soko kuu nchini China.

Utafiti unaashiria takriban wateja milioni tatu kila mwaka wananunua bidhaa ghushi zenye nembo za kifahari kama LV, Yves Saint Laurent, Burberry au hata Gucci.

Haki miliki ya picha Marc Piasecki
Image caption Mabegi ya safari ya LV yana thamani ya kati ya $ 1200 hadi $ 3000.

Kuonekana kwa kiongozi huyo akiwa amesimama karibu na sehemu ya watu mashuhuri au matajiri kupandia ndege, kulimponza.

Baadhi walichukulia kuwa hilo linaashiria kuwa Wine anaelekea kupanda na kukaa katika kitengo cha abiria wenye hadhi, yaani Business class.

Mwingine huyo akatumia fursa kusahihisha kwamba Bobi Wine alikaa sehemu ya ndege ya abiria wa kawaida tu kinyume na ilivyodaiwa. Kwa alikuwa amesimama tu kwenye eneo la kuwahudumia 'abiria wa hadhi' akiwa njiani kuelekea eneo la abiria wa kawaida.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii