Chloride Exide: Sababu ya wanaume hawa kuvalia kama wanawake

Wafanyakazi wa kampuni Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Ukizitazama picha hizi picha unaweza ukadhani unawatazama wanamitindo, au ukadhani kuna wanawake kwenye picha hii.

Lakini wote ni wanaume, na si wanamitindo pia. Ni wafanyakazi wa kampuni moja nchini Kenya walioamua kuvalia kama wanawake kazini kama sehemu ya maadhimisho ya kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya kiafya ya wanawake, na zaidi saratani Oktoba ukiwa mwezi wa kuhamasisha kuhusu saratani ya matiti.

Picha zao zimesambazwa sana mtandaoni Kenya, baadhi wakiwapongeza na wengine kukosoa hatua hiyo.

Walioshiriki walikuwa wafanyakazi wa kiume wenye vyeo mbalimbali katika kampuni hiyo, akiwemo afisa mkuu mtendaji Guy Jack.

Meneja mkurugenzi wa kampuni hiyo Guy Jack Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE
Image caption Meneja mkurugenzi wa kampuni hiyo Guy Jack

Meneja wa huduma kwa wateja Stella Kamau ameambia BBC kwamba wazo la wanaume kuvalia mavazi ya kike kazini liliibuka katika moja ya vikao vilivyokuwa vikijadili shughuli ya kupamba wiki ya huduma kwa wateja, ambayo mwaka huu imeadhimishwa kuanzia kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa wiki hii.

Wazo lilitolewa mwanzoni mwa Septemba, ambapo kibarua kilianza cha kuwashawishi wanaume kushiriki.

Wafanyakazi wa kampuni Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

"Baadhi walisema 'Haiwezekani!'. Walishangaa ni vipi wake zao na watoto wangelipokea wazo hilo. Ilikuwa ni karibu wote walikuwa na wasiwasi," anasema Bi Kamau.

Lakini baada ya muda, pole pole walilikubali wazo hilo.

Ikawa basi ni kupanga na kusubiri siku yenyewe.

Mavazi yalitoka wapi? Wafanyakazi wa kike ndio waliojitolea kuwapa wanaume hao mavazi, nguo, viatu na hata vibegi.

Kabati lilijaa mavazi ya kila aina.

Mfanyakazi Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Wanaume walifika wakiwa wamevalia mavazi ya kawaida, lakini wakabadilisha na kuvalia mavazi hayo ya kike. Walipodolewa na kupambwa na wenzao kuhakikisha wanapendeza kwa kweli.

Bi Kamau anasema hilo lilipoanza kutendeka, furaha na vicheko vilitawala afisini.

"Imekuwa ni wiki ya huduma kwa wateja na kando na mtazamo wa nje kuboresha huduma kwa wateja, ni muhimu kuhakikisha kwamba kazini ni pahali pa furaha, wafanyakazi kuwa na furaha," anasema.

Mbwembwe hizo zilidumu kwa saa kadha lakini kwa baadhi kazi haingetendeka bila mavazi yao ya kawaida, na hivyo walibadilisha baada ya saa kadha.

Lakini kuna wengine waliofurahia sana na kuvalia hivyo kwa kipindi kirefu.

Mfanyakazi Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Ingawa shughuli kuu ilifanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la viwandani, Nairobi, wafanyakazi katika matawi mengine walishiriki.

"Afisini palipendeza sana jana. Hata tuna wazo la kuanzisha kundi la mambo ya kufurahisha ambalo litakuwa linatoa mapendekezo ya kipekee ya kufurahisha," anasema Bi Kamau.

Kampuni ya Chloride Exide ni sehemu ya kamapuni kubwa ya Associated Battery Manufacturers (ABM) ambao ina matawi Kenya, Uganda, Tanzania na Zambia na ina kampuni nyingine zinazoangazia sekta yakawi kama vile Solinc, na kampuni ya plastiki ya Precision Plastics. Wafanyakazi wa kampuni hizo Kenya walishiriki.

Mfanyakazi Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Na wanawake wakavalia kama wanaume na kwenda kazini?

"Hilo halitafurahisha zaidi kama wanaume wakivalia kama wanawake. Isitoshe, mpango wetu si mavazi pekee na usawa, tunahamasisha kuhusu matatizo ya kiafya wanayokumbana nao wanawake," anasema Bi Kamau.

Watu wanasemaje?

Irene Muriuki, mmoja wa waliochangia maoni anatania kuhusu aliye hapa chini: "Ndiye dada ambaye kila mtu angependa kuwa naye ... anajali sana na ana sifa za mama ... mpelekee matatizo yako yote na utapata ushauri wa busara."

Mfanyakazi Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Ndiye huyu pia

Mfanyakazi Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Hawa ni Guy Jack na meneja wa ukaguzi wa hesabu Charles Ngare.

Guy Jack akiwa na meneja wa ukaguzi wa hesabu Charles Ngare Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Fuchaka Edel aliandika: "Njia nzuri sana ya kuwaungamkono wanawake. Nawahakikishia kwambawakati wowote nikihitaji betri ya gari, nitawakumbuka hawa 'slayqueens'".

Wafanyakazi wa kampuni Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Min LC alisema aliyetoa wazo hilo anafaa kuongezewa mshahara.

Guy Jack na wachezaji wengine Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Brenda Nekesa Muliro alisema: "Wiki yangu imekuwa haiendi sawa hadi nilipoiona hii. Inachekesha sana na nawashukuru kwa kuvalia viatu vya wanawake.

"Yule mwanamume mwenye rinda la jeusi na viatu vyenye kwato ndefu amependeza kweli."

Mfanyakazi Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Hodiah Hourldar Chepchirchir, "Haha day made. Aki nitanunua battery hata kama sina gari".

Mfanyakazi Haki miliki ya picha CHLORIDE EXIDE

Unaweza kusoma pia:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii