Diane Rwigara na mamake waachiliwa huru na mahakama Rwanda

Rwigara na mamake Haki miliki ya picha Getty Images

Mahakama Kuu mjini Kigali imeamua kumuachilia huru kwa dhamana mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara na mamake na watafuatiliwa wakiwa nje ya gereza.

Jaji wa mahakama kuu mjini Kigali ametangaza kwamba maombi yao ya dhamana yamekubaliwa lakini wakawekewa masharti ya kukabidhi pasipoti zao kwa mwendesha mashitaka.

Aidha wametakiwa kutovuka mipaka ya jiji la Kigali bila kibali maalumu.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema baada ya uwamuzi huo umati wa jamaa zao umeimba na kusherehekea mahakamani huku wakimsifu Mwenyezi Mungu kwa uamuzi huo.

Wawili hao walikuwa kizuizini tangu mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

Walikanusha madai hayo wakisema wakisema yana misingi ya kisiasa.

Mashtaka yanayomkabili

Bi Rwigara na mtetezi maarufu wa haki za wanawake nchini Rwanda na familia yake inasema matatizo yake yalianza wakati aliamua kuwania urais.

Hakufaulu kuwania na alipigwa maruku baada ya uchunguzi kubaini kuwa Bi Rwigara alikuwa amekiuka sheria kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono kugombea kwake.

Bi Rigwara alikamatwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara Septemba 2017 nyumbani kwake kwenye mji mkuu Kigali.

Kagame: Afrika iache kutegemea nchi za Magharibi

Rwanda yaunda gari lake la kwanza

Mama yake naye anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea mapinduzi ya serikali.

Image caption Diana Rwigara na mamake wakiwa mahakamani leo

Rais Kagame alishinda uchaguzi wa mwaka uliopita kwa asilimia 98.63 ya kura.

Amesifiwa kwa kuleta mafanikio ya kuichumi nchini humo tangu yafanyike mauaji ya kimbari mwaka 1994.