Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 06.10.2018: Mourinho, Neymar, Pogba, Loftus-Cheek, Fabregas, Cahill

Image caption Jose Mourinho,Kocha wa Machester United

Habari za ndani toka Machester United zinasema kocha Jose Mourinho atatimuliwa kazi kwenye mapumziko haya ya mwishoni mwa juma kama timu yake itapata matokeo mabaya dhidi ya Newcastle United ( Daily Mirror)

Image caption Mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris St-Germain na timu ya taifa ya Brazil Neymar

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris St-Germain na timu ya taifa ya Brazil Neymar amefanya mazungumzo na kiungo wa Manchester United Paul Pogba kumshawishi kujiunga na mabingwa hao wa League 1 baada ya kutokua na mustakabali mzuri wa baadae kwa kiungo huyu mwenye miaka 25. (Goal)

Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson amesema timu yake inaweza kumsajili kiungo wa Chelsea Roben Loftus-Cheek,ambaye alicheza kwa mkopo kwenye timu hiyo msimu uliopita (Talksport)

Timu ya Arsenal itamsajili kiungo raia wa Paraguay mwenye umri wa miaka 24 anaichezea timu ya Atlanta United Miguel Almiron,Hayo yamesema na Rais wa timu hiyo ya Marekani Darren Eales (Fox Deportes USA, in Spain)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa Chelsea na timu ya Taifa ya Hispania Cesc Fabregas 31 katikati

Kiungo wa Chelsea na timu ya Taifa ya Hispania Cesc Fabregas 31,anatarajiwa kupewa mkataba mpya na Blues kwa sababu mkataba wake unatarajia kuisha mwishoni mwa msimu huu kwenye majira ya kiangazi (Guardian)

Mlinzi wa kati wa timu ya Chelsea na England Gary Cahill ,32, amesema anajianda kukaa kwenye timu hiyo ya Stamford Bridge hadi mwishoni mwa msimu huu ingawa kulikuwa na taarifa zikisema alikuwa na mpango wa kuondoka kwenye timu hiyo wakati wa dirisha dogo la uhamisho mwezi Januari (Evening Standard).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gary Cahill

Wakati huo huo Southampton inataka kumsajili Cahill pale mkataba wake utakapomalizika kwenye majira ya usajili yajayo ya kiangazi.

James Rodriguez,27,amekasirishwa mno na kitendo cha kuwekwa nje kwenye kikosi cha kwanza cha Bayern Munich na sasa anafikiria kuihama timu hiyo.

Nyota huyo wa Colombia anacheza kwenye timu hiyo kwa mkopo toka Real Madrid upande wa Ujerumani (Bild-in German)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Niko Kovac amekanusha kuwa na tofauti na Rodriguez

Kocha wa Bayern Munich Niko Kovac amekanusha kuwa na tofauti na Rodriguez. (AS)

Kocha wa Brentford Dean Smith amekanusha uvumi ulioenea kuwa anataka kuihama timu hiyo baada ya kuhusishwa na mpango wa kupewa kazi ya kuinoa Aston Vill na kusema hana mpango ( Birmingham Mail)

Kocha wa timu ya Everton Marco Silva amesema hatofikilia kufanya usajili mwezi Januari hadi akitathimini kikosi chake chote ( Liverpool Echo)

Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ujerumani Ilkay Gundogan ,27, amesema timu yake haitakutana na mchezo mgumu msimu huu zaidi ya mchezo wa ugenini kesho dhidi ya Liverpool. (ESPN)

Image caption Mwamamuziki Noel Gallagher

Mwamamuziki Noel Gallagher ambaye ni shabiki wa Manchester City amenukuliwa akisema kocha wa Manchester United Jose Mourinho anafanya kazi nzuri (Talksport)

Akiwa safarini kusaini mkataba na Manchester City,kiungo Bernardo Silva, 24,amewaambia mashabiki wa Manchester United kuwa alifanya uamuzi sahihi kwenda Old Trafford kabla hajajumuika na mashetani wekundu.(Sun)

Mada zinazohusiana