Kwa nini huwa vigumu kwa Waafrika kuzuru mataifa ya Afrika wakilinganishwa na Wazungu na raia wa nchi za nje

paspoti ya Mali Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wasafiri wengi wa Afrika wanasema hati ya usafiri katika bara hili huwa ni ghali sana

Mfanyibiashara tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote, amesema kuwa anahitaji hati 38 za kusafiria mataifa tofauti barani akitumia pasipoti yake ya Nigeria.

Licha ya hayo raia wengi wa mataifa ya bara Ulaya wanaruhusiwa kuzuru mataifa ya Afrika bila hati ya usafiri, yaani visa.

Mataifa ya Kiafrika yalitakiwa kufutilia mbali masharti ya visa kwa wananchi wote wa Afrika kufikia mwaka 2018.

Hii ilikuwa sehemu muhimu ya makubaliano na ushirikiano wa mataifa ya Umoja wa Afrika (AU) iliyopitishwa na wanachama wote mwaka 2013.

Hadi wa leo Ushelisheli ndilo taifa la pekee barani Afrika ambalo limeweka huru masharti ya usafiri kwa Waafrika wote na raia wa mataifa hayo

Ripoti ya hivi karibuni ya Muungano wa Afrika AU imebaini kuwa waafrika wanaweza kutembelea 22% ya mataifa mengine ya Afrika bila visa.

Hili ni suala nyeti katika baadhi ya mataifa tajiri barani Afrika kutokana na kadhia ya wenyeji kuwabagua wageni kwa kuhofia kupoteza nafasi zao za kazi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfanyibiashara Aliko Dangote anataka usafiri urahisishwe ndani ya barani Afrika sawa na ilivyo barani Ulaya

Watunga sera kutoka Cape hadi Cairo wamekuwa na wakati mgumu kuwahamasisha watu umuhimu wa uhuru wa kutangamana wakisisitiza ni kiungo muhimu kwa ustawi wa uchumi.

Katchie Nzama, mwanablogu wa masuala ya utalii nchini kutoka Afrika Kusini ambaye ametembelea mataifa 35 barani Afrika anasema "Viongozi wetu wanafanya kila wawezalo kuhifadhi na kulinda mipaka ya kikoloni,"

Muungano wa Afrika AU huenda unapigania bara lililo na mipaka huru ambapo watu wake takriban bilioni 1.2 wanaweza kutangamana katika mataifa tofauti kama wenzao wa muungano wa bara Ulaya lakini inakabiliwa na vizuizi vya kila aina.

Kwa mfano maafisa wa uhamiaji nchini Burkina Faso kuwatoza wasafiri ada dola 200 kupata visa wanapowasili nchini humo, au Tanzania kuwakamata na kuwarudisha makwao raia wa mataifa ya Afrika Mashariki wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria. Tunisia pia imeripotiwa kuwanyima visa wasafiri wa kiafrika waliyokwama katika uwanja wa ndege baada ya ndege ya yao kufutiliwa mbali.

Hii yote ni ishara wazi ya jinsi mataifa ya bara afrika yanavyoangaliana kwa jicho la kutoaminiana.

Ni mapendeleo?

Afrika Kusini imetajwa kuwa moja ya mataifa ya Afrika ambayo imefungia mlango Waafrika wenzake huku ikiweka wazi sera ya mlango wazi kwa mataifa mengine duniani.

Ni mataifa 15 pekee ya Afrka ambayo raia wake wanaruhusiwa kuzuru Afrika Kusini bila visa huku ikiwapatia fursa raia wa mataifa 28 ya Ulaya kuingia nchini humo bila visa bora wawe na paspoti ya muungano wa Ulaya.

Msemaji wa Idara ya masuala ya ndani wa nchi hiyo Thabo Mokgola ameitetea vikali sera hiyo.

Ameiambia BBC kuwa "Hiyo ni dhana potofu -makubaliano kuhusu hati ya usafiri inategemea uhusiano kati yetu na mataifa husika. Kwa sasa tuko katika harakati ya kukamilisha mpango huo kwa baadhi ya mataifa ya Afrika".

Hata hivyo msingi wa makubaliano hayo haijawekwa wazi ni wa aina gani.

Kenya, kwa mfano inawapatia raia wa Afrika Kusini Visa wanapowasili nchini humo lakini wakenya sharti waombe hati ya usafiri ya nchi hiyo kabla ya kulipa ada na baadaye kusubiri kwa siku tano kabla ya kuidhinishwa kwa hati hiyo.

Tangu mwa 2015, miaka miwili baada ya Muungano wa Afrika kuyataka mataifa kutekeleza hitaji la kufutilia mbali hati ya usafiri kwa mataifa yote ya Afrika kufikia mwisho wa mwaka 2018, Afrika Kusini ilienda kinyume na agizo hilo kwa kuweka masharti magumu zaidi ambayo yameendelea kulaaniwa vikali.

Baada ya kukumbwa na kudorora kwa uchumi na kushuka kwa idadi ya watalii wanaozuru taifa hilo, Afrika Kusini imelazimika kubadili msimamo na kulegeza baadhi ya masharti ya usafiri.

Haki miliki ya picha Corbis/Getty Images
Image caption Ufukwe wa bahari ya atlantic nchini Senegal

Paspoti ya Afrika

Mataifa ya Namibia, Mauritius, Ghana, Rwanda, Benin na Kenya zimelegeza masharti ya usafiri kwa raia wa mataifa ya bara Afrika kwa kuwapatia visa wanapowasili nchini humo au kuwarusu wazuri mataifa hayo kwa hadi siku 90 kwa kutumia paspoti zao.

Hata hivyo bado raia wa mataifa ya Afrika wanahitaji hati ya usafiri uzuru zaidi ya nusu ya mataifa 54 barani ambayo yanalinda mipaka uliyoorodheshwa wakoloni wao zaidi ya mwango mmoja uliyopita.

Mfanyibishara bilionea wa Nigeria Aliko Dangote anasema ''Mtu kama mimi licha ya kuwa na kampuni nyingi nahitaji kuwa na hadi visa 38 ili kuniwezesha kuzuru bara Afrika''

Bwana Dangote ameripotiwa kuwa mmoja kati ya watu watakaopewa paspoti ya Afrika iliyozinduliwa mwaka 2016

Stakabadhi hiyo inastahili kuchukua nafasi ya paspoti ya kila nchi lakini kwa sasa inamilikiwa na baadhi ya viongozi wa nchi, wanadiplomasia na maafisa wa ngazi ya juu wa muungano wa AU.

Haki miliki ya picha AFP/BBC
Image caption Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenyekiti wa zamani wa muungano wa Afrika Idriss Déby walipewa paspoti ya kwanza ya AU mwaka 2016

Ushirikiano wa mataifa kikanda baini ya mataifa ya Jumuiya ya Afrika mashariki, Afrika magharibi , Afrika Kusini na Afrika ya Kati iunakabiliwa na changamoto kwasababu ya masharti ya usafiri kutoka eneo moja hadi jingine..

Gharama ya usafiri

Kikwazo kingine ni cha gharama ya usafiri ndani ya bara la Afrika .

Ni ndege chache sana za kibiashara kutoka eneo moja hadi nyingine na zole zilizopo zinatoza nauli ya hali ya juu.

Winnie Rioba, mwanablogu wa Kenya anaeangazia masuala ya usafiri anasema "Bei ya usafiri kutoka Kenya hadi Namibia ni sawa na kusafiri kuenda Thailand, na gharama ya usafiri kutoka Nairobi kuenda Dubai ni bei nafuu kuliko kuenda Morocco," .

Na hii ni kando na gharama ya kupata visa.

Bi Rioba alitozwa ada ya dola 90 kupata visa ya Djibouti, hii ikiwa ni ada ya juu ikilinganishwa na dola 75 aliyotozwa kupata visa ya Schengen ambayo ilimwezesha kuzuru mataifa 26 ya bara Ulaya.

"Nimetumia pesa nyingi kuomba hati ya usafiri kuliko gharama ya usafiri katika ziara yangu ya mataifa ya Afrika," anasema bi Nzama mwana blogu wa Afrika Kusini ambaye anakubaliana naye.

Ili kuwasaidi raia wa Nigeria kukabiliana na masuala ya usafiri barani Afrika, mfanyibiashara Funmi Oyatogun amebuni ramani inayoangazia ni mataifa yapi yaliyo na masharti rahisi kuzuru

Funmi Oyatogun, anasema " Lengo letu ni kurahisisha usafiri kote barani Afrika,"

Anaamini juhudi zake ni sehemu muhimu itakayochangia kuunganisha watu katika bara hilo.

Watu wengi wanaunga mkono kufutiliwa mbali kwa masharti ya usafiri kwa waafrika wanaosafiri ndani ya Bara la Afrika.

Huku muda wa mwisho wa kutekeleza agizo lililotolewa na AU, kuhusiana na suala hilo ukikaribia kukamilika ni watu wachache wanaamini mpango huo utafikiwa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii