John Terry: Kapteni wa zamani wa England na Chelsea astaafu soka

John Terry Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Terry alilinyanyua taji la ligi ya England alipokuwa kapteni wa Chelsea katika msimu wake wa mwisho Stamford Bridge

Aliyekuwa kapteni wa timu ya taifa ya England na Chelsea John Terry amestaafu katika soka.

Terry, mwenye umri wa miaka 37, hajaichezea klabu yoyote tangu aondoke timu ya mabingwa Aston Villa msimu wa joto.

Mlinzi huyo alitoa tangazo hilo kwenye akaunti yake ya Instagram, akisema: "Baada ya miaka 23 kama mchezaji wa soka, nimeamua sasa ndio muda muafaka kwangu mimi kustaafu kutoka mchezo wa soka."

Terry, aliyejinyakulia mataji 78 England, aliondoka Chelsea mnamo 2017 baadaya kuichezea klabu hiyo ya Londona kwa miongo miwili.

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu 08.10.20118

Alishinda mataji matano katika lingi ya England , matano ya FA , taji la Mabingwa alipokuwa , na kuwa mchezo aliyethaminiwa zaidi katika klabu hiyo .

Beki huyo wa kati alifanikiwa kushinda mataji matano ya ligi na la Europa katika mechi alizowahi kushiriki mara 700 za Chelsea.

Terry aliutumia msimu wa 2017-18 akiichezea Aston Villa na mechi yake ya mwisho kama mchezaji soka wa kulipwa iliishia kwa 1-0 dhidi ya Fulham mnamo Mei katika mechi ya marudio kwenye fainali ya ligi ya mabingwa.

Kiungo wa Arsenal ashindwa kwenda Azerbaijan

Aliondoka Villa Park wakati makataba wake wa mwaka ulipomalizika na alikataa ombi la uhamisho kwenda Spartak Moscow mwezi uliopita, licha ya kuarifiwa kufanyiwa ukaguzi wa akiafya, akisema kwamba haitokuwa sawa kwa familia yake.

Haki miliki ya picha .
Image caption Chelsea ilitoa heshima kwa kapteni wake wa zamani

Kupanda na kushuka milima

Terry aliingia katika soka akiwa na miaka 17 alipocheza dhidi ya Aston Villa katika League Cup mnamo Oktoba 1998, na alilifunga bao lake la kwanza kwa klabu hiyo katika mechi ya FA dhidi ya Gillingham mnamo 2000.

Hatahivyo mwaka uliofuata, Terry alikuwa mojawapo ya wachezajiw a Chelsea waliotozwa faini ya mishahara ya wiki mbili na klabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu katika hoteli moja kufuatia shambulio la kigaidi la Septemba 11 nchini Marekani.

Alikuwa kiungo muhimu katika ushidni wa Blues katika kunyakuja taji la England au Primia na kombe la FA kati ya 2009-10, na kuwahi kucheza zaidi ya mara 50 wakati Chelsea ilipokuwa klabuya saba pekee kufanikiwa kupata ushindi wa mataji mawili mtawalia.

Nyota wa Liverpool alazwa baada ya kuumia uwanjani

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 05.10.2018

Hatahivyo alivulia ukapteni wa timu ya taifa ya England, kabla ya kupigwa marufuku kucheza mechi nne na kutozwa faini ya £220,000 kwa kutoa matamshi ya ubaguzi dhidi ya mlinzi wa QPR Anton Ferdinand.

Alikosa kucheza fainali ya ligi ya mabingwa pia mnamo 2012 ambapo the Blues aliifunga Bayern Munich kwa mikwaju ya penalti, kutokana na kwamba alikuwa amesimamaishwa kucheza.

Terry alifunga mabao 4 goals katika mechi 35 za ligi wakati Chelsea iliponyakua taji la ligi ya Englanda kati ya 2014-15, lakini imekuwa vigumu kucheza kikamilifu chini ya ukufunzi wa Antonio Conte.

Alijiunga na Aston Villa kwa mkataba wa mwaka mmoja na kuichezea mechi 36, alifunga bao moja, katika msimu wa mwisho kama mcheza soka wakati imu hiyo ya Birmingham ilipomaliza katika nafasi ya nne kwenye ubingwa kabla ya kushindwa katika mechi ya marudio kwenye fainali.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kwaheri kutoka kwa Terry

Katika ujumbe kwenye mtandao wa Instagram, Terry aliishukuru familia yake kwa kumuunga mkono.

Aliandika: "Nikiwa na miaka 14 nilifanya maamuzi makubwa na muhimu: kujiunga na klabu ya Chelsea. Maneno hayatoshi kuonyesha uzito wa kila mmoja katika klabu, hususan mashabiki.

"Tangu mwanzo, wameniunga mkono kikamilifu ndani na nje ya uwanja , nina uhusiano mkubwa nao.

"Tumekuwa na kumbukumbu nyingi nzuri na nisingefanikiwa bila ya nyinyi. Kwangu mimi nyinyi ni mashabiki bora duniani. Nataraji nimewapa ufahari kwa kuvaa shati na mpira mkononi.

"Kazi yangu katika klabu na moyo wangu daima uni wa Chelsea, lakini ninashukuru kwa muda wangu wa mkopo huko Nottingham Forest mnamo 1999, ambao ulinisaidia pakubwa kujiendeleza kama mchezaji chipukizi.

"Na nataka pia nitoe shukrani kubwa kwa Aston Villa kwa kunipa fursa kucheza katika klabu kubwa na kuwa kapteni kwa msimu mzima wa 2017-18.

"Ilikuwa ni heshima kubwa kuwakilisha timu kubwa yenye sifa ya soka na mashabiki wake.

"Natazamia ukurasa mpya katika maisha yangu na changamto zinazokuja mbele."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii