Mabadiliko ya tabia nchi: Njia tano za kupunguza ongezeko la joto duniani

Picha ya dunia inayoonyesha sehemu ya mabara Haki miliki ya picha Getty Images

Ni ombi la mwisho, wanasayansi wanatoa kuhusiana na hatari ya kuongezeka kwa viwango vya joto duniani.

Ripoti yao inayosisitizia mataifa kudhibiti viwango vya joto chini ya nyuzi joto 1.5 sasa inasema hali inaendelea kuwa mbaya ikizingatia kule tunakoelekea.

Kudhibiti viwango vya joto hadi vipimo vinavyohitajika vya nyusi joto 1.5 inaamnisha jamii inastahili kupunguza kwa kiwango kikubwa shughuli zake za viwanda na shughuli zingine za mazingira ambazo zinchangia kupanda kwa viwango vya joto duniani

Ili kufikia hatua hiyo itagharimu washika dau gharama kubwa lakini bado kuna matumaini.

Haki miliki ya picha SOPA IMAGES

Baada ya miaka mitatu ya utafiti na kujadiliana pamoja na majadiliano wiki nzima kati ya wanasayansi na maafisa wa serikali, katika mkutano wa mazingira nchini Korea Kusini, Jopo kazi la mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa limetoa ripoti maalum kuhusu umuhimu wa kuhakikisha viwango vya joto duniani visalia kuwa chini ya nyuzi joto 1.5

Watunga sera walikuwa na wakati mgumu kuafikiana na watafiti kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ikizingatiwa madhara yake kiuchumi na viwango vya maisha.

Licha ya midahalo mingi kuhusu madhara ya kuongezeka kwa viwango vya joto duniani kuna mambo muhimu yanayojitokeza wazi kuhusiana na suala hilo.

Prof Jim Skea, mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika jopo mataifa kuhusu mazingira anasema, ''Jambo muhimu kwanza ni kupunguza gesi ya viwango vya joto kwa digiri 1.5 hatua hiyo pekee itakuwa na umuhimu mkubwa katika mabadiliko ya hali ya hewa''.

Bwana Skea pia ameongeza kuwa "Jambo la pili ambalo si la kawaida ni mabadiliko ambayo yanayo hitajika ikiwa tunapunguza joto kwa 1.5C

Hii ni pamoja na mabadiliko ya mifumo ya nishati, mabadiliko ya njia tunayotumia ardhi, na mabadiliko ya mfumo wa usafiri."

Kaisa Kosonen, kutoka shirika la Greenpeace na ambaye alikua mwangalizi wa mashauriano hayo anasema ,"Wanasayansi wanataka kuandika kwa herufi kubwa , 'TEKELEZENI SASA MABADILIKO HAYA , lakini kwanza wanastahili kuonyesha bayana hali ni mbaya kiasi gani,"

Watafiti wametumia ukweli huo na baadhi ya mifano mingine kwa kupiga picha inayoashiria jinsi ya dunia inakabiliwa na hatari kubwa, inayosababishwa na wanadamu.

Tulikuwa tukifikiria kuwa tunaweza kurudisha joto chini ya nyuzi joto mbili karne hii, lakini hayo si mabadiliko ambayo tunanaweza kudhibiti.

Utafiti huu unasema kuwa kupitisha kiwango cha joto duniani kwa nyuzi joto 1.5 inamaaanisha kuwa viumbe hai dunia wanaelekea kuangamia.

Hali hiyo isipotiliwa maanani tunaelekea kuvuka viwango vilivyopendekezwa ifikapo mwaka 2030, miaka 12 kuanzia sasa.

Sorry, your browser cannot display this map

Sasa tufanye nini?

Ripoti hiyo inapendekeza lazima iwe na mabadiliko makubwa na muhimu katika mifumo minne ya kimataifa

Mifumo hiyo ni pamoja na Kawi ,matumizi ya ardhi, makaazi na viwanda

Lakini inaongeza kuwa ulimwengu hauwezi kufikia lengo lake bila mabadiliko ya watu binafsi.

Wanasayansi wanahimiza watukubadilisha mtindo wao wa maisha kwa mfano kutumia teknolojia ya mawasiliano badala ya kusafiri kwa ndege.

Pia wanapendekeza watu kutumia kamba kuanika nguo juani badala ya kutumia mashini kuzikausha miongoni mwa vitu vingine vitakavyopunguza hewa ya carbon.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchina hutoa kiasi kikubwa zaidi duniani cha gesi yenye madhara makubwa ya CO2, ambayo husababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.

Hatua tano muhimu za kufikia nyuzi joto 1.5

  1. Uzalishaji wa hewa ya CO2 ulimwenguni unahitaji kupunguzwa kwa 45% ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2010 kufikia mwaka wa 2030
  2. Kutumia kawi mbadala kwa 85% badala ya kuzalisha umeme ifikapo mwaka 2050
  3. Kupunguza uzalishaji wa mkaa ya mawe kabisa
  4. Karibu eneo la kilomita milioni saba litahitajika kuzalisha ya nishati
  5. Kupunguza viwango vya kimataifa vya joto duniani ifikapo mwaka 2050
Image caption Viwanda vinatajwa kwa kiwango kikubwa kuchangia mabadiliko ya hali ya hewa

Itagharimu pesa ngapi kufikia hayo?

Wataalamu wanasema haitakuwa rahisi lakini kudhibiti viwango vya joto duniani wa kwa digiri 1.5 kunahitaji uwekezaji wa karibu dola trilioni 2.4 katika mfumo wa kawi kati ya mwaka 2016 na 2035.

Wanasema fedha hizo zinahitaji kufadhili miradi itakayochangia kufikiwa kwa mpango huo muhimu duniani.

Dr Stephen Cornelius, mwanachama wa zamani wa uangallizi wa masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa anasema"ndio gharama ni kubwa lakini ni uwekezaji wa siku za usoni''

Anasema ni vyema kudhibiti uzalishaji wa gesi chafu kuliko madhara ya gesi hiyo kwa mazingira karne ijayo.

Image caption Athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Nini kitafanyika hatua isipochukuliwa?

Watafiti wa masuala ya mazingira wanasema mataifa yakishindwa kudhibiti viwango vya joto chini yanyuzi joto 1.5, ulimwengu utakuwa mahali hatari zaidi kutokana na mabadiliko yatakayoshuhudiwa

Viwango vya maji katika bahari vitapanda kwa nchi nne hali ambayo itasbabisha mafuriko yatakayoathiri karibu watu milioni 10.

Pia kuna athari kubwa kupanda kwa kiwango cha joto la bahari na asidi hali ambayo itaathiri viumbe hai majini

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii