Je, utumiaji wa kompyuta unaweza kuwapatia wanawake wafungwa nchini Kenya fursa mpya?

hatua ya kuwapa fursa mpya ili nao kujitafutia uchumi ambao utawanufaisha hapo badae".
Image caption Kujifunza teknolojia ni fursa mpya kwa wafungwa ili wajikomboe kiuchumi hapo badae

Dorcus mwenye umri wa miaka 44, anatabasamu huku akichukua mashine moja ya tarakilishi , akiwaelelezea wanafunzi wapya kuhusu matumizi ya kila kifaa cha kilektroniki cha kompyuta.

'Sasa naweza kufanya kila kitu.Naweza hata kukutengenezea tarakilishi,' anaongezea.

Dorcus ni miongoni mwa wafungwa 500 katika gereza la lanagata ambalo ndio gereza pekee ya wanawake katika mji mkuu wa Kenya,Nairobi.

Wakati mwingine wafungwa huwa wanafungwa hapo vifungo hadi vya miaka miwili kwa makosa ya uchuuzi, kuuza vitu kama njugu au matunda kandokando ya barabara.

Wengine wanahudumia vifungo vya maisha jela kwa makosa makubwa zaidi, kama vile mauaji, au utumiaji wa nguvu. Licha ya aina hiyo ya uhalifu, takwimu za magareza ya Kenya kutoka mwaka 2014 zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya wafungwa wote nchini humo watarudia makosa na kufungwa tena jela.

Image caption Aggrey Mokaya ni mwanzilishi wa Change Hub, mpango wa urekebishaji wa kiteknolojia

Aggrey Mokaya mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mwanzilishi wa Change Hub, mpango wa urekebishaji wa kiteknolojia na muhadhiri wa chuo kikuu cha Jomo Kenyatta, anasema "Ni hatua ya kuwapa fursa mpya ili nao kujitafutia uchumi ambao utawanufaisha hapo badae".

Change Hub inawafundisha wanawake hawa kila kitu katika teknolojia na mitindo ya tovuti hadi kurekebisha tarakilishi.

Aggrey anaamini kwamba ni kupitia kuwawezesha watu kutumia teknolojia ndio kutakaosaidia kupunguza idadi kubwa ya watu wanaofanya makosa kwa mara ya pili.

'Mfungwa wa zamani na mtu ambaye hajafanya makosa ya uhalifu mbele ya sheria wote ni sawa, kwa hivyo nadhani wote wanafaa kuwa sawa kwa maswala ya uchumi na mbele ya ujasiriamali au fursa zozote.

Baada ya kuhudumu nusu ya kifungo chake cha miaka mitatu kwa udanganyifu Dorcus ataachiwa huru mwezi Oktoba 2018

"Nina watoto watano na mimi ni mjane hivyobasi kukutanishwa tena na wanangu ni jambo muhimu kwangu ", Dorcus anasema.

Dorcus tayari ametengeza tovuti kwa biashara yake ya kushona nguo ambayo anatarajia kuzindua atakapotoka jela.

'Sitaweza kuzunguka na kupata vumbi miguuni kwa sababu sina gari', analezea.

Iwapo watanyimwa fursa kama hizo ili kuweza kuingia mahali wanapoweza kujipatia kitu tunawatayarisha mazingira ya kushindwa'.

'Itabadili maisha yangu, Nitakuwa nikihifadhi muda na fedha'.

Mfumo wa haki nchini Kenya ,unaangazia sana adhabu badala ya urekebishaji, na suala hili ndilo linalopaswa kubadilika, kulingana na wakili wa mahakama kuu Achieng Orero.

'Sidhani kwamba kuna juhudi za pamoja zinazofanywa ili kuwarekebisha wafungwa', anasema.

'Ni muhimu sana kushirikisha urekebishaji ama kuwacha fikra za kutoa adhabu kwa sababu mwisho wake, wakati mfungwa huyo anapomaliza kifungo chake hio ndio njia ya pekee kuwawezesha kuwa watu muhimu katika jamii'.

Image caption Rahab Nyawira amekuwa mtaalam wa kuoka keki baada ya kutoka gerezani

Kwa upande mwengine wa mji wa Nairobi, katika jiko moja lenye moto mkali Rahab Nyawira mwenye umri wa miaka 35, anaweka mapambo katika keki kubwa.

Aliachiliwa kutoka jela ya Langata mwaka huu baada ya kuhudumia kifungo cha miaka sita kwa kosa la wizi wa mabavu.

Rahab kwa sasa anamiliki biashara yake ya kuoka keki na ana mipango ya kumshirikisha watoto wake katika biashara hiyo. ''Tovuti yangu ninaweza kusema ndio nguvu zangu , anaelezea huku akitabasamu.

'Inanisaidia kukutana na wateja wapya mtandaoni kila mahali nchini Kenya'.

Alitengeneza tovuti yake wakati alipokuwa jela. 'Nilijifunza mambo mengi kupitia Change Hub. Niliweza kjifunza kuhusu HTML, CSS na Javascript. Kwa tovuti yangu nilijitengezea kila kitu mwenyewe.

Mwanangu wa kike anaponiona sasa, najivunia sana'.

Agrey anaamini kwamba ni uwezo huu wa kutumia teknolojia unaoweza kubadilisha maisha ya wafungwa wanawake wanapoachiliwa huru.

'Kuna upendeleo wa kijinsia katika utumizi wa teknolojia', anasema, akielezea kwa nini yeye huwazingatia wafungwa wanawake.

Iwapo ninaweza kubadili maisha ya mwanamke mmoja inamaanisha kuwa kuna matokeo mazuri. Ni fursa kwa watoto wake pia kujifunza programu hiyo mapema .

Aggrey anatafuta ufadhili wa kupanua Change Hub ili kuwafikia takriban wafungwa 8,000 wa kike katika jela za kenya

Image caption Gereza pekee la wanawake jijini Nairobi,lanagata

Kufikia sasa wafungwa 21 katika jela ya Langata wamepitia masomo ya programu hiyo

Ana mipango ya kuifanya program yake kujimudu kupitia kushirikiana na makampuni ambayo yatawalipa wafungwa kusomea teknolojia na kuunda vitu kwa kutumia mashine za printa za 3D na

baadaye, ndoto yake ni kuipeleka Change Hub katika kila gereza nchini Kenya.

'Unajua unapozungumzia kuhusu kutaka kufanya mradi wa kiteknolojia, kila mtu anasema kwa nini usiende katika jela za wanaume ama zile za wafungwa vijana?'

'Nafikiria kuhusu hilo na kusema kuwa ni kweli ni muhimu lakini ni kitu cha baadaye. Tutafikiria hilo iwapo tutafanikiwa katika jela za wanawake.'

Kipindi hiki cha BBC kiliandaliwa kupitia ufadhili wa wakfu wa Bill & Melinda Gates

Mada zinazohusiana