Kimbunga Michael: Majimbo matatu kusini mashariki mwa Marekani yameathirika

Kimbunga Michael kuyakumba maeneo ya majimbo matatu Marekani

Gavana wa jimbo la Florida Rick Scott amesema kuwa kimbunga Michael kimesababisha madhara yasiyo semeka katika maeneo ya pwani jimboni.

"Hivyo maisha ya watu wengi yamebadilika kabisa,familia zimepoteza kila kitu."

Maeneo ya kaskazini mashariki yameharibiwa vibaya,nyumba zimechimbuka na kuanguka kutoka kwenye misingi yake,miti mikubwa imeangukia nyumba,mfumo wa umeme umeharibika kabisa.

Kimbunga Michael siku ya jumatano kililikumba eneo hilo kwa kasi kubwa ya kilomita 250 kwa saa.

Zaidi ya watu 370,000 Florida waliamriwa kuondoka,japo kuwa inaonyesha wengi wao walikaidi.

Gvana wa jimbo la Florida Rick Scott, amekielezea kimbunga hicho kuwa ni hatari Zaidi.

Kutokana na hali hiyo majimbo ya Alabama, Florida na Georgia yametangaza hali ya hatari,ambapo Alabama maeneo 92 watu wake wanatakiwa kupisha madhara ya kimbunga hicho Michael kusini mwa jimbo la Georgia na maeneo 35 ya jimbo la Gergioa kimbuka hicho kinatarajiwa kuyafikia.

Naye Gavana wa Jimbo la Carolina ya Kaskazini Roy Cooper ameonya kwamba watu wake kwamba wanatakiwa kuchukua tahadhali kwani huenda madhara ya kimbunga hiki yakawa makubwa Zaidi ya Kimbunga Florence kilicholikumba eneo hilo mwezi uliopita.

Mada zinazohusiana