Kanye West adai kofia ya Trump imempa nguvu za Superman, akosoa shule za siku hizi

Kanye West Haki miliki ya picha Reuters

Si jambo la kushangaza kusikia Kanye West mmoja kati ya wasanii maarufu zaidi duniani katika miondoko ya kufoka foka amekutana na Rais wa Marekani Donald Trump.

Kwa muda mrefu sasa amekuwa akionyesha hisia zake wazi wazi za kumsifu Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter na mahojiano mbali mbali.

Hata hivyo amekuwa akiwakosoa wanaomkemea kwa kuwataka wamwache awe na uhuru wa mawazo yake.

Kanye West alialikwa katika ikulu ya Marekani kwa ajili ya chakula cha mchana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mageuzi katika magereza, ajira na masuala ya wamarekani weusi.

Ni mjadala uliojaa vioja vingi kutokana na ukweli kwamba Trump na Kanye wote ni wazungumzaji sana na hutumia zaidi mtandao kuweka wazi hisia zao.

Hata hivyo uongeaji wa Kanye West pia ulitengeneza habari.

Katika majadiliano hayo yaliyolenga siasa, mageuzi na uzalishaji, West alinukuliwa akisema "wamejaribu kunitisha, marafiki zangu kuhusu kuvaa hii kofia, lakini hii kofia inanipa nguvu".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kanye West aliweka wazi hisia zake za kumkubali sana Rais wa Marekani

Kanye alienda mbali zaidi na kusema kofia hiyo iliyoandikwa "Make America great again" maneno yanayowakilisha kauli mbiu ya utawala wa donald Trump inamfanya anajionea fahari sana na anajiona kama Superman na aliongeza kuwa Trump ametengeneza kofia shujaa kwa ajili yake.

Haki miliki ya picha ShaunKing
Image caption Hata hivyo kauli za Kanye hazikupokelewa vizuri na baadhi ya watu

Shule hazivutii

Hata hivyo alitoa hoja zake mbali mbali ikiwemo kwa sasa shule zina upweke zaidi na sio kama simu

"Mara nyingine watu wanasema mtoto huyu hana uwezo wa kusikiliza kwa makini, Hauna huo ugonjwa, shule imejaa upweke, sio ya kufurahisha kama hii," anasema Kanye huku akionyesha simu yake ya mkononi.

Pia alimtaka Rais Trump ajenge viwanda katika mji alipozaliwa wa Chicago na alimpongeza Donald kwa kufanikiwa kusimamisha vita na Korea kaskazini.

"Umesitisha vita, tumetatua tatizo letu kubwa zaidi," Kanye alimwambia Trump.

Taarifa za Kanye kukutana na Trump zilisambaa sana huku zikiwa zimeambatana na video mbalimbali zinazo mwonyesha Kanye akimkumbatia Rais huyo wa marekani.

Lakini pia baadhi ya video hizo zimemwonyesha akiwa katika mazungumzo ambapo alisikika akimsifia sana Rais huyo wa Marekani kuwa anampenda.

Hata hivyo mkutano huo umekuwa gumzo mtandaoni huku watu mbali mbali wakionyesha kukerwa na kitendo cha Kanye West kukutana na Trump lakini pia maneno aliyozungumza.

Haki miliki ya picha Pool

Baadhi ya wasanii maarufu ambao awali pia walikuwa ni marafiki wa Kanye west wameonyesha kukerwa na kitendo hicho cha Kanye.

Huku baadhi wakitamka wazi wazi kuwa Kanye anaitia aibu jamii ya wamarekani weusi.

Kupitia kurasa mbali mbali za mitandao ya kijamii, wasanii hao wamerusha madongo yao wazi wazi akiwemo P. Didy, TI, 50 Cent na wengine wengi.

Haki miliki ya picha Diddy
Image caption Hii ni mara ya kwanza kwa Kanye West kutembelea Ikulu ya Marekani

Kanye West aliwahi kumtembelea Donald Trump huko Manhattan mwaka 2016 mwezi mmoja baada ya Trump kushinda, lakini hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutembelea ikulu ya Marekani.

Mke wake Kim Kardahian amewahi kwenda mara mbili katika Ikulu hiyo maarufu kama White House.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii