DesertWheelRace2018: Mashindano ya walemavu Isiolo Kenya

#DesertWheelRace2018

Mashindano makubwa ya watu wanaoishi na ulemavu yanafanyika nchini Kenya.

Zaidi ya walemavu 100 kutoka jamii za wafugaji wanashiriki katika mashindano yaliopewa jina #DesertWheelRace2018 yanayofanyika kila mwaka kwa walemavu walio kwenye viti vya magurudumu mjini Isiolo mashariki mwa Kenya.

Dhamira kuu ya michezo ya leo ni kushinikiza kampeni inayonuiwa kupambana na unyanyapaa dhidi ya watu walio na ulemavu katika jamii.

Ujumbe uliopo ni kwamba kuwa mlemavu hakupaswi kumzuia mtu kufanya kitu chochote. Na kwamba kila mmoja ana uwezo ya kutimiza ndoto yake.

Kauli mbiu ya mwaka huu, 'Tume fursa mtoto atembee' imenuiwa kuhamasisha umuhimu wa kutoa mafunzo kwa watoto walemavu.

Changamoto kubwa katika baadhi ya jamii nchini ni kutotambua umuhimu wa kuwapa elimu watoto wenye ulemavu, na kwa mujibu wa wanaharakati wengi wao husihia kutengwa na kunyimwa haki msingi maishni, ikiwemo hiyo ya elimu.

Waziri wa ugatuzi nchini Kenya, Eugene Wamalwa ametoa hakikishi kwa washika dau katika warsha ya kitaifa ya walemavu nchini kwamba serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa sheria inaendelea kutekelezwa katika uwakilishi wa walemavu kwenye taasisi mbali mbali za serikali.

Kifungu cha 54 cha sheria nchini Kenya kinahimiza uwepo wa angalau 5% ya walemavu katika taasisi zote za umma, ima ni kwa kuchaguliwa au kuteuliwa.

Nini kinabaini umri wa wavulana kubaleghe?

Ndege ya Air India yagonga ukuta

Kwa mujibu wa benki kuu ya dunia, changamoto kubwa inayotajwa ya uwakilishi kamili katika masuala ya kijamii na kiuchumi ni pamoja na :

  • Kutoweza kufikia mazingira stahiki na usafiri
  • Ukosefu wa vifaa na teknolojia za kuwasiadia
  • Vyanzo vya kuzoeleka vya mawasiliano
  • Pengo katika uwasilishaji wa huduma,
  • Ubaguzi
  • Upendeleo
  • Unyanyapaa katika jamii

Shirika la afya duniani na benki kuu ya dunia linakadaria kwamba takriban watu bilioni 1 au 15% ya watu duniani, wanaishi na ulemavu wa aina fulani.

Kati ya idadi hiyo, inatajwa kwamba kati ya milioni 93 to 150 ni watoto.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii