Kutoweka kwa Jamal Khashoggi: Mkuu wa UN ataka 'ukweli' kuhusu kutoweka kwake

Jamal Khashoggi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jamal Khashoggi mwanahabari wa gazeti la Marekani la Washington Post aliyetoweka

Taarifa za kutoweka kwa mwanahabari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi na madai ya kwamba huenda ameuawa zimeendelea kugonga vichwa vya habari kote duniani

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres sasa anasema kuwa ''anataka ukweli'' kuhusiana na kutoweka kwa mwanahabari Jamal Khashoggi.

Bwana Guterres ameimbia BBC kuwa anahofia visa vya kutoweka kwa watu kama vile mwanahabari Jamal Khashoggi huenda ikawa "Jambo la kawaida''.

Khashoggi, ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia alitoweka Oktoba 2 katika mazingira ya kutatanisha baada ya kutembelea ubalozi wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamfalme Mohammed bin Salman amekosolewa kuhusiana na kutoweka kwa mwanahabari Jamal Khashoggi

Saudi Arabia imekanusha madai kwamba ilitoa amri ya kuawa kwa mwanahabari ikisema madai hayo ni ya "uwongo".

Waziri wa uslama wa kitaifa ya wa Saudi Arabia, mwana mfalme Abdulaziz bin Saud bin Naif bin Abdulaziz, amenukuliwa na shirika la habari la Saudia akisema kuwa ufalme huo pia unataka kubaini ukweli kuhusiana na kisa cha kutoweka kwa mwanahabari Khashoggi.

Vianzo vya habari kutoka idara ya usalama nchi Uturuki vimeiambia BBC kwamba maafisa nchini wana kanda ya sauti na video kuthibitisha kuwa bwana Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul.

Guterres amesema nini?

Haki miliki ya picha Google
Image caption Antonio Gutteres Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

Akizungumza katika mkutano wa shirika la fedha duniani mjini Bali Guterres amesema,''Tunahitaji kuambiwa ukweli kuhusiana na kisa hiki, tunahitaji kujua nini hasa kilifanyika''.

Gutteres pia amesema mfumo wa kisheria unahitajika ili waliohusika wawajibishwe kisheria.

Bwana Guterres ametoa wito kwa Saudi Arabia kujibu madai kwamba ilihusika na kutoweka kwa mwanahabari Khashoggi kwa njia inayotakikana.

Saudi Arabia itakua mwenyeji wa kongamano la uwekezaji mjini Riyadh mwezi huu lakini badhi ya wadau wakuu wametangaza kujiondoa katika mpango wa kuhudhuria mkutano huo.

Mkuu wa Benki ya Dunia ,Jim Kim, tayari amjiondoa katika mkutano huo, huku Sir Richard Branson, mkuu wa shiria la Virgin, akisema kuwa amesitisha wajibu wake katika miradi miwili ya utalii.

Siku ya Jumamosi mkuu wa, shirika la kimataifa la fedha duniani Christine Lagarde ameelezea kugutushwa kwake na ripoti kutoka Uturuki lakini atahudhuria kongamano la uwekezaji nchini Saudi Arabia.

Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Hatice Cengiz, Mchumba wa mwanahabari Khashoggi anasema alimsubiri nje ya ubalozi kwa saa 11 lakini hakurejea

Jamal Khashoggi ni nani?

  • Bwana Khashoggi ni mwandishi wa habari mashuhuri ambaye amewahi kuangazia, taarifa za jinsi Sovieti ilivyovamia Afghanistan na kuibuka kwa Osama Bin Laden.
  • Amefanya kazi katika mashirika kadhaa ya habari nchini Saudi Arabia.
  • Aliwahi kuwa afisaa wa ngazi ya juu wa Saudi Arabia, lakini baadaye akatofautiana na serikali.
  • Mwaka jana alikimbilia uhamishoni nchini Marekani ambako amekuwa akiandika makala ya kila mwezi katika gazeti la Washington Post.
  • Katika makala yake ya kwanza ya gazeti hilo, Bw Khashoggi alisema kuwa anagopa kukamatwa kwa kukosoa wazi wazi utawala wa nchini Saudi Arabia.
  • Siku tatu kabla ya kutoweka kwake Khashoggi, aliambia BBC kuwa "Watu wanao kamatwa si wapinzani wa serikali na kwamba wana uhuru wa kujielezabali wanajieleza.

Matukio kuelekea kutekwa kwaKhashoggi Oktoba 2

Haki miliki ya picha Image copyrightGETTY IMAGES

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Uturuki:

03:28: Ndege ya kwanza ya kibinafsi iliyokuwa imebeba maagenti wanaoshukiwa kuwa wa Saudia iliwasili uwanja wa ndege wa Istanbul.

05:05: Maajenti hao walichukua chumba cha malazi katika hoteli moja karibu na jengo la ubalozi .

12:13: Magari kadhaa ya kidiplomasia yanayodaiwa kuwabeba baadhi ya maagenti hao yanaswa katika video yakiwasili ubalozi huo wa Saudia

13:14: Bwana Khashoggi anaonekana akiingia jengo la ubalozi.

15:08: Magari ya yanaondoka jengo la ubalozi yanachukuliwa video yakiwasilia makaazi ya balozi karibu na hapo.

17:15: Ndege ya pili iliyobeba maafisa wanaoshukiwa kuwa wa Saudi Arabia inatua Istanbul.

17:33: Mchumba wa Khashoggi, Hatice Cengiz, anaonekana katika picha za CCTV akisubiri nje ya ubalozi.

18:20: Moja y andege ya kibinafsi anaondoka uwanja wa ndege wa Istanbul airport.

21:00: Muda ambao ndege ya pili iliondoka

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii