Harusi ya Facebook: 'Kwa nini tuliigiza harusi yetu Kinshasa'

Jean-Félix Mwema Ngandu na Arlene Agneroh Haki miliki ya picha Christian Shabantu Mpenga
Image caption Jean-Félix Mwema Ngandu na Arlene Agneroh

Marafiki na familia yake wanaona kuwa Arlène Agneroh amefinikiwa karibu kila kitu alichotaka maishani.

Amepata ufanisi mkubwa maishani na anavutia. Wanamuita kiongozi kwa sababu huwa anawafundisha wajasiriamali somo la kujiendeleza maishani.

Lakini wanasema kitu pekee alichokikosa ni mume wakumuoa.

Hivi karibuni Arlène alikutana na kisa kilimkumbusha jinsi jamii inavyowapa presha vijana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuoa au kuolewa

Akiwa na miaka 33 alialikwa harusi ya mmoja ya marafiki zake katika mji mkuu wa Kinshasa - ilikuwa mwaliko wa 30 aliyopokea katika mwaka huo pekee.

Kama ilivyo kawaida ya harusi ya wakongo, wageni walioalikwa na bibi harusi huvalia nguo zinazofanana naye, huku wale waliyoalikwa na bwana harusi nao huvalia mtindo tofauti.

Wakati wa sherehe hiyo ya harusi, Bi Agneroh alikuwa ameketi na rafiki yake wa karibu, Jean-Félix Mwema Ngandu.

'Ilikuwa kitu cha kushangaza sana'

Kama illivyo kawaida, mmoja wa rafki yao aliwapiga picha wakiwa pamoja harusini.

Bada ya hapo akaiweka picha hiyo katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Dakika tano baada ya kufanya hivyo, simu yake ikaanza kuita na kupewa pongezi. Akaanza kucheka.

Bi Agneroh, anakumbuka kumuuliza "Kuna nini?"

Akanijibu,"Kila mmoja anafikiria nyinyi wawili mmeoana!".

Haki miliki ya picha Larissa Diakanua
Image caption Marafiki wao wa zamani walisema kuwa wanataka kuhudhuria harusi yao baada ya picha ya pili kutumwa Facebook

Agneroh aliiambia BBC "Sikuamini kabisa. Muda mfupi baada ya hapo baadhi ya watu wakaanza kunitumia ujumbe wa kunipongeza ,"

Marafiki wake wawili wilifurahishwa na suala hilo wakaamua kuliendeleza gumzo hilo na hapo hapo wakaamua kutuma picha nyingine inayowaonyesha wakiwa wameketi katika sehemu maalum ambapo pametengewa maharusi.

Mara hii, walisubiri kwa saa kadhaa baada ya kushare picha hiyo katika ukurasa wa Facebook ya rafiki yao mwingine ili kuona watu watasema nini.

"Nilipoamka asubuhi ya siku iliyofuatia, nilipata nimepigiwa karibu simu mia moja, pamoja na ujumbe wa WhatsApp na Facebook," .

Bi Agneroh anasema kuwa "Baadhi ya wale walionipigia simu na kunitumia ujumbe ni watu ambao hatukuwa tumezungumza kwa kati ya maika 10, na 15 years. Hata sijui watu hao walipata wapi namba yangu ya simu."

'Watu wanaamini kila kitu wanachosoma mtandaoni'

Image caption Arlène Agneroh

Agneroh pia anasema "Tukio hilo lilimfanya kusikitika kwa sababu mtu hufikia mahali maishani akajiona kuwa ameridhika, lakini jamii humshinikiza kujiona kuwa bado kuna kitu ambacho hakijatimia."

Bwana Mwema Ngandu, 32, anaafiki kuwa walijua hatua yao "ingelizua gumzo ", aliambia BBC kuwa walijiandaa walipopiga picha ya pili.

"Zama hizi za taarifa ghushi, watu huamini kila kitu wanachoona na kusoma mitandaoni,"

Mwema Ngandu anatoa wito kwa watu kuwa kuwa makini kuhusiana na vitu wanavyosoma katika mitandao ya kijamii.

"Wakati mwingine ni mambo ya kufurahisha lakini pia huenda ikawa mabo ya kusikitisha ambayo yanaweza kuwaathiri wahusika kwa njia moja au nyingine."

Image caption Kanisa Katoliki lina waumini wengi nchini DR Congo

'Bado niko kwenye soko'

Wakati mmoja wa marafiki zake walimwambia kuwa wanajiandaa kuja Kinshasa kwa "harusi"

Bi Agneroh aliamua kuwaambia ukweli wa mambo katika ukurasa wake wa Facebook. Katika maelezo yake refu aliwaambia marafiki za: "Picha hizi zinaonyesha vijana wawili waliopigwa picha na marafiki zao, bila maoni au mwelekeo wa ndoa lakini nyote mkaamua kutafsiri mlivyochagua.

"Bila hata kuuliza maswali yoyote, mkaamua kusambaza picha hizi na kuunda hadithi zenu wenyewe.

Shukrani kwenu nyote, nimeanza kukusanya orodha ya wageni kwa ajili ya harusi yangu.

Image caption Arlène Agneroh anaonyesha kwa simu yake, ndiyo picha iliyosambazwa mitandaoni

"Lakini kwa sasa, wale ambao wamekuwa wakitaka kunitongoza lakini wakawa na hofu, Huu hapa ni ujumbe wangu: Mimi bado niko kwenye soko lakini sijakusudia kutafuta mume.

Kwa hiyo, subira ... Somo la kujifunza ni kutafakari kabla ya kutenda jambo .Ni vyema pia kuangalia mazingira.

Picha peke yake sio ishara ya hadithi kamili."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii