Je upinzani katika Afrika Mashariki na kati bado uko hai?

Bobi Wine amesema kwa muda mrefu demokrasia katika Afrika imekuwa ikiminywa na watawala Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mpinzani Uganda Bobi Wine amesema 'kwa muda mrefu demokrasia katika Afrika imekuwa ikiminywa na watawala'

BBC Idhaa ya Kiswahili inaanza Makala maalum za kuangalia na kutathmini hali pamoja na uhai wa vyama vya kisaiasa vya upinzani katika eneo la Afrika Mshariki.

Hapa swala kuu ni, je vyama vya Upinzani katika Afrika Mashariki na kati bado viko hai?

Mbunge wa Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine akihutubia mkutano wa kisiasa wa hadhara Mjini Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa juma hili alisikitishwa sana na hali ya kisiasa katika bara la Afrika na hasa Afrika Mashariki.

Alisema kwa muda mrefu demokrasia katika Afrika imekuwa ikiminywa na watawala hivyo kuzima sauti na uwezo wa vijana huku ufisadi, mapendeleo na uongozi mbaya ukikithiri.

Ndio maana katika ziara hiyo yake ncini Kenya Bobi Wine aliungana na Mbunge chipukizi wa Kenya Babu Owino pamoja na Wabunge wengine kuanzisha vuguvugu jipya la vijana "Youth For Africa Movement"

Huwezi kusikiliza tena
Ni ipi nguvu ya upinzani katika mataifa ya Afrika?

Katika mikutano miwili mikubwa ya kisasa Jijini Nairobi Bobi Wine na wabunge wenzake chipukizi kutoka Kenya walisema vuguvugu hilo jipya la Vijana lina lengo la kupanua demokrasia , kuwapa vijana wa bara la afrika sauti na uwezo kuhusu maswala ya uongozi na usimamizi ili kuboresha maisha yao.

" Tumekuja hapa sio kuomba bunduki, sisi hatuna haja ya kumuuwa yeyote hatutaki umwagikaji wa damu . Tumekuja kutafuta urafiki na kuungana na nyinyi ili tupiganie uhuru wa mamilioni ya wanaonyanyaswa barani Afrika ambao wengi wao ni vijana ." alisema katika mojawapo ya mikutano hiyo Jijini Nairobi.

" Pakiwa na maonevu na uongozi wa kiimla nchini Uganda , hii inaathiri sio waganda tu . Ikiwa jambo lolote baya litafanyika nchini Kenya ,hii pia inaiathiri Uganda na kadhalika", alisema huku akishangiliwa.

Ili kuunganisha viongozi vijana barani Afrika viongozi wa vuguvugu hilo jipya la vijana wamepanga kuwa na mkutano mwenge mkubwa wa hadhara jijini Nairobi mwezi wa Novemba ambao utahudhuriwa na viongozi wengine chipukizi kama vile Julius Malema wa Afrika kusini, Nelson Chamisa aliyeogombea urais wa Zimbabwe katika uchaguzi mkuu hivi karibuni.

Upinzani Tanzania

Nchini Tanzania nako kumekuwa na malalamiko kuwa demokrasia imekuwa ikiminywa huku mambo mengine yakifanyika kana kwamna nchini hiyo ni ya chama kimoja ilhali kuna vyama vingi vya kisiasa.

Huwezi kusikiliza tena
Freeman Mbowe: Chanzo cha wabunge 20 wa upinzani kukamatwa Tanzania ni uchaguzi mdogo

Freeman Mbowe ni kiongozi wa chama cha upoinzani cha CHADEMA " Tunakuwa na vyama vingi katika maneno na katika karatasi lakini katika matendo tunatengeneza mfumo wa chama kimoja , nchi hii itazama."

Lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini Tanzania mambo hayakuwa hivi. Kulionekana kuwa na ushindani mkubwa wa kisiasa na wa wazi ncini humo.

Na tarehe 29 Oktoba ,2015 Rais John Pombe Magufuli alipotangazwa mshindi kwa kura 8,882,935 wengi wadadisi wengi wa kisasa walibashiri kwamba Bwana Edward Lowassa aliyeibuka wa pili kwa kura 6,072,848 angeliihangaisha serikali hiyo mpya na kuwa mkosoaji wake mkubwa. Hata hivyo mambo hayakuwa hivyo.

Mapema mwezi Januari mwaka 2018 Bwana Lowassa alizuru Ikulu kukutana na Rais Magufuli na baada ya ugeni huo katika hutuba yake alimsifu sana rais wa Tanzania.

"Kwanza nimepata faraja sana kuja ikulu. Mimepata nafasi nzuri ya kuzungumza nae. Kwanza nikupongeza kwa kazi nzuri anayoifanya.afanya kazi nzuri nchini, anahitaji kutiwa moyo".

Kusalimiana kwa Raila na Uhuru Kenya

Na kuvuka nchini Kenya mambo sio tofauti sana .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Uhuru na kiongozi wa Raila Odinga wamekubaliana kuunda mpango wa pamoja wa kuangazia utekelezaji wa malengo ya pamoja

Tarehe 9 mwezi Machi mwaka huu wa 2018 kiongozi wa upinzani Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta walikutana na kufanya mazungumzo marefu katika ofisini rasmi ya Rais. Mwishowe wakachomoza na kupena mikoni ya urafiki na kuahidi kufanya kazi pamoja.

Tufauti na uhasama mkubwa wa kisiasa ulidumu kwa miaka na hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 ambapo Upande wa serikali ikiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta nad Upinzani mkuu chini ya Raila Odinga baada ya mkutano huo wa tarehe 9 mwezi Machi wawili hao walionekana wakizungumza lugha moja na hata kuitana "Ndugu yangu".

" Tumekuja pamoja na bdugu yangu Uhuru Kenyatta tumeongea kwa kirefu na tumekubaliana ya kwamba tunataka kuunganisha Kenya iwe taifa moja".

Kutona na matamshi hayo ya Bwana Raila Odinga achanganuzi wengi na hata raiya wa kawaida walisema sasa upinzani umekufa nchini Kenya.

Ingabire hampi homa Kagame

Image caption Victoire Ingabire Umuhoza kiongozi wa upinzani Rwanda aliyeachiwa huru na rais Kagame mwezi jana

Rwanda nako upinzani wa kisasa wa haja nikama hakuna.

Wadadisi wengi walidhana pengine wanasiasa Victoire Ingabire Umuhoza na mwanasiasa mwengine wa hivi majuzi tu Bi Diane Rwigara wangelimtia Rais Paul Kagame homa ya kisasa lakini mambo yalikuwa kinyume.

Bi Ingabire alikamatwa na hatimae kufungwa jela mwaka 15 kwa makosa ya ugaidi pamoja na kuhatarisha usalama wa kitaifa . Hata hivo sasa yuko huru baada ya kupewa msamaha na Rais Kagame.

Nae Mwanadada Diane Rwigara alianzsha kampeni za kutaka kumuondo Rais Kagame Uongozini lakini juhudi zake hazikufika mbali. Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda ilimzuia kushirika kutokana na kutotimiza masharti yaliyohitajika . Baada alikamatwa na kushitakiwa kutokana na makosa kadhaa ya jinai yakiwemo kugushi nyaraka.

Mwanzo wa kifo cha upinzani Burundi

Image caption Agathon Rwasa amesema wapinzani nchini Burundi kwanza watapaswa kuimarisha vyama vyao kabla ya kuungana kwa ajili ya uchaguzi wa 2020.

Burundi nako kwa sasa hakuna upinzani wakumsumbua Rais Pierre Nkurunziza kisaiasa.

Kwa wengi ishara zimekuwepo tangu kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa kuchaguliwa na kuwa Naibu spika wa Bunge la Burundi.

Pia wakati chama chake Rwasa cha National Liberation Forces (NLF) kuamua kumtimua kiongozi huyo, na halafu viongozi wapya wakaamua kumuunga mkono Rais Nkukunziza, ilionekana kuwa mwanzo wa kifo cha upinzani .

Wabunge wa upinzani Burundi walipochaguliwa na kujiunga na baraza la mawaziri, ilikatisha wengi tamaa ya kuwa na upinzani wa nguvu wa kisiasa nchini humo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii