Kondomu zinazojilainisha zilizoundwa kupunguza maambukizi

condom Haki miliki ya picha Getty Images

Wanasayansi wanasema wamegundua njia ya kutengeneza kondomu zinazojilainisha zinazoteleza tu zinapovaliwa.

Ni kutokana na kilainishi cha kudumu kinachosalia wakati wote wa tendo la ndoa, kinasema kikosi , kilichoungwa mkono na wakfu wa Bill na Melinda Gates Foundation.

Wanatarajiwa itazifanya kondomu kuvutia katika matumizi na hivyobasi kufanikiwa kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na uja uzito.

Mtelezo wa kutosha ni muhimu katika tendo la ndoa, na usipokuwepo, wahusika hupata maumivu na mara nyingine kondomu hupasuka au kuvuka.

Inapotumika vizuri, kondomu hutumika kama njia ya kupanga uzazi inayofanya kazi, lakini sio kila mtu anazipendelea.

Kwa mara nyingi kondomu huwa zimewekwa mtelezo kurahisisha matumizi, lakini mara nyingine huwa haitoshi.

Watu huweza kutumia vitelezo au vilainishi vinavyouzwa madukani ila hutapakaa, mara nyingine mtu hulazimika kuongeza mara kwa mara , na kutatiza shughuli inayoendelea kwa wakati huo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Watafiti wanasema kondomu hiyo ya kujilainisha, huendalikatatuwa matatizo hayo.

Inaweza kuhimili shughuli nzima bila kupoteza mtelezo kwa mujibu wa Jarida la sayansi la Royal Society Open.

Wakati ilipofanyiwa majaribio, kondomu za kawaida zilizotumika kwa vilainishi vya dukani, zilikuwa laini awali ya matumizi lakini baadaye hupoteza mtelezo huo katika tendo la ndoa.

Kundi la watu waliojitolea waliombwa kugusa na kuziorodhesha kondomu zote, kwa misingi ya urahisi wa kuvaa na mtelezo wake.

Makosa ya kawaida yanayofanywa na watumizi kondomu

  • Bidhaa za mafuta, zikiwemo krimu za mkononi, zinaweza kuharibu mpira wa kondomu kwahiyo ni muhimu kuepuka kuzitumia.
  • Usitumie Kondomu zaidi ya mara moja
  • Tahadhari namna unavyozihifadhi kondomu zako kwasababu zinaweza kuharibika haraka, hususan kama umeziweka kwenye pochi au begi.
  • Tazama tarehe ya mwisho ya matumizi
  • Unapovaa kondomu, ni muhimu ufinye mwisho wa mpira huo ili utoe hewa yoyote, usipofanya hivyo, huenda ikapasuka.

Kati ya kundi hilo la watu waliojitolea katika majaribio ya kondomu, wanaume na wanawake 33 waliridhishwa zaidi na kondomu hizo zinazojilainisha.

Watafiti wanasema utafiti zaidi unahitajika kulinganisha utendaji wa kondomu hizo zinazojilainisha, dhidi ya aina nyingine za kondomu kwa uhalisi.

Kampuni moja sasa kutoka chuo kikuu inapanga kutengeneza kondomu hizo za kuuzwa sokoni, iwapo itapata idhini kisheria.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii