Msafiri Zawose: Mwanamuziki Mtanzania anayevuma Ulaya na Marekani licha ya kutumia ala ya asili

Msafiri Zawose: Mwanamuziki Mtanzania anayevuma Ulaya na Marekani licha ya kutumia ala ya asili

Muziki wa asili nchini Tanzania haufurukuti mbele ya muziki wa kizazi kipya ambao unapatiwa muda wa kutosha katika vyombo vya habari na hata wasanii wake kupata nafasi ya kushiriki matamasha makubwa nje na ndani ya Tanzania.

Licha ya muziki huo kutokutamba, Zawose amekuwa ni msanii anayefanya matamasha mengi Ulaya na hivi karibuni wimbo wa ushirikiano na msanii Feiertag_Music uitwao Trepidation umejumuishwa katika nyimbo 122 zitakazotumika katika Game la Fifa.

Msafiri Zawose ambaye ni msanii wa muziki wa Asili toka Tanzania amejijengea jina kubwa katika mataifa ya bara Ulaya na Marekani kwa aina ya muziki anao ufanya

Msafiri ambaye hutumia ala za asili kama vile zeze na marimba katika Muziki wake ana amini kwamba ipo siku Muziki huu wa asili utapata heshima nchini Tanzania na kwingineko barani Afrika

Mtayarishi: Eagan Salla