Abiy Ahmed: Wanajeshi waliokuwa wakiandamana walitaka kuniua, niliwafanyisha mazoezi nikiwa sina raha moyoni

Picha ya waziri mkuu akifanya mazoezi ya Press-ups Haki miliki ya picha Walta TV
Image caption Abiy Ahmed anasema kuwa aliwaamrisha wanajeshi waliokuwa wakiandamana kuhusu mshahara kufanya zoezi la maungo ili kupunguza wasiwasi uliokuwepo.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema kwamba baadhi ya wanajeshi walioingia katika eneo la afisi yake wiki iliopita walitaka kumuaa.

Wakati huo, aliondoa wasiwasi uliokuwepo kwa kuwaamrisha kufanya press-ups[mazoezi ya maungo}.

Bwana Abiy na wanajeshi hao walionekana wakicheka lakini aliambia bunge kwamba 'ndani yangu sikuwa na furaha'.

Katika kipindi cha miezi sita iliopita amekuwa akifanya mabadiliko muhimu na anasema kuwa baadhi ya wanajeshi wake walitaka kuzuia mabadiliko hayo.

"Maandamano hayo ya baadhi ya wananjeshi hao katika afisi ya waziri mkuu yalikuwa kinyume na sheria na hatari , kwa sababu lengo lilikuwa kusitisha mabadiliko yaliokuwa yakiendelea, bwana Abiy aliambia wabunge wakati ambapo waziri mkuu anajibu maswali bungeni.

Wakati huohuo baada ya hali hiyo kudhibitiwa , baadhi ya wanajeshi walisikika wakisema: Alitoroka kabla ya sisi kiumuua.

Haki miliki ya picha Reuters

Wengi wameshangazwa na matamshi ya waziri huyo wiki hii ambapo wiki iliopita alijibu tofauti alipoulizwa kuhusu swaa hilo.

Baadaye alionekana akicheka na kutabasamu, lakini amefichua katika bunge kwamba alikuwa amekasirika na kukerwa sana.

Anasema kwamba alihofia kwamba mgogoro ungezuka kwa kuwa vijana wadogo walikuwa wakielekea mjini Addis Ababa ili kiushiriki katika vita.

Kwengineko kuna hamasisho kwamba kuna baadhi ya watu wasiofurahikia mabadiliko yake.

Waziri mkuu huyo hapo awali amewataja wanajeshi wasiokubaliana naye kuhusu mabadiiko anayofanya.

Alitumia neno hilo kuhusu jaribio jingine la mapinduzi ya maisha yake alipozungumzia mlipuko wa ghasia za kikabila katika maeneo tofauti ya taifa hilo.

Hali ya kutisha

Mnamo tarehe 10 mwezi Oktoba , takriban wanajeshi 100 waliokuwa wakiandamana , wengine wao wakiwa wamejihami walienda kumuona waziri mkuu -ili kuitisha nyongeza ya mishahara.

Hali hiyo ilizua hali ya hatari na kusababisha barabara kufungwa katika eneo hilo huku mtandao ukizimwa kwa saa kadhaa.

Akizungumza na wabunge siku ya Alhamisi , bwana Abiy alisema kuwa bila amri ya kufanya press ups swala lote zima lingeongezeka na kuzua wasiwasi mkubwa .. watu wengine wanaona press-ups tulizofanya kuwa za kawaida. Lakini, tulitumia kuondoa hali ya hatari iliokuwepo.

"Katika jeshi, push-ups ama kufanya mazoezi ama hata kuzungumza kwa sauti ya juu ni baadhi ya hatua zinazotumika kupunguza hisia ama huzuni.

Tangu achukue mamlaka mnamo mwezi Aprili , bwana Abiy amefanya mabadiliko -ikiwemo kuwaachilia huru maelfu ya wafungwa wa kisiasa , kutopiga marufuku makundi yaliopigwa marufuku na kuleta amani kati yake na taifa la Eritrea.

Mwezi uliopita , viongozi wa mashtaka wa Ethiopia waliwashtaki washukiwa watano na ugaidi kufuatia jaribio la kutaka kumuua bwana Abiy katika shambulio la gurunedi katika mkutano mnamo mwezi Juni.

Alifanikiwa kutoroka na hakujeruhiwa na kulitaja shambulio hilo kuwa lilitekelezwa na wanajeshi wasiotaka kuona taifa la Ethiopia likiwa limeungana.

Harakati za mabadiliko ya bwana Abiy

Haki miliki ya picha AFP
Image caption watu walisherehekea wakati eneo la mpakani kati ya Eritrea na Ethiopia lilipofunguliwa
  • 2 Aprili- Alikuwa waziri mkuu baada ya kujiuzulu kwa ghafla kwa Hailemariam Desalegn
  • 19 Aprili - Alimbadilisha mkuu wa polisi na usalama wa ndani
  • Mei - Aliwaachilia huru maelfu ya wafungwa wa kisiasa , ikiwemo kiongozi wa upinzani Andargachew Tsege
  • 5 Juni - Aondoa hali ya hatari miezi miwili kabla muda wake kukamilika
  • 5 Juni - Akubali uamuzi wa ulioipatia Eritrea eneo la mpakani.
  • 9 Julai - Akiwa pamoja na rais wa Eritrea walkitangaza kumalizika kwa vita kati ya mataifa hayo mawili
  • 11 Septemba - Alifungua eneo la mpakani na Eritrea
  • 16 Oktoba - Awachagua wanawake kushikilia nusu ya nyadhfa za uwaziri.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii