Jamal Khashoggi: Mwandishi wa Saudia aliyepotea aliyemjua Osama bin Laden

A man holds a poster of Saudi journalist Jamal Khashoggi during a protest in Istanbul,organised in front of the Saudi consulate. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jamal Khashoggi alikwenda kwenye ubalozi wa Saudia mjini Istanbul kupata nyaraka za udhibitisho wa talaka aliyompa aliyekuwa mke wake

Polisi nchini Uturuki wanaochunguza tuhuma za mauaji ya mwandishi habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi wamepanua uchunguzi, taarifa zinasema.

Maafisa wa Uturuki ambao hawajatajwa wanasema mwili wake huenda umetupwa katika msitu ulio karibu au katika shamba.

Khashoggi alitoweka baada ya kuingia katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul mnamo Oktoba 2 , sehemu ambayo maafisa wa Uturuki wanatuhumu aliuawa.

Saudi Arabia inakana kuwa na ufahamu wowote wa kilichomkabili.

Sampuli zilizochukuliwa kutoka ubalozi na makaazi ya balozi wakati wa upekuzi wiki hii zinafanyiwa majaribio kwa kulinganishwa na chembe chembe za vina saba au DNA ya Khashiggi.

Uturuki imewahi kusema ina ushahidi wa kanda ya sauti na video ya mauaji ya Khashoggi, lakini hazijafichuliwa wazi, licha ya Marekani kuitaka Uturuki itoe ushahidi huo.

Mkasa huu umesababisha mvutano mkubwa kati ya Riyadh na washirika wake wa mataifa ya magharibi.

Jamal Khashoggi ni nani?

Jamal Khashoggi ni mwandishi maarufu aliyeangazia taarifa kubwa kwa mashirika tofuati nchini Saudia.

Aliunda urafiki na Osama bin Laden katika miaka yake ya kwanza alipoanza kuwa mwandishi habari na alifahamika kama mzaliwa maarufu wa Saudia aliyelazimika kutoroka nchi hiyo.

Kabla ya kutoweka kwake katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, uhamisho wa kibinfasi wa Khashoggi ulimlazimu kuishi baina ya Marekani, Uingereza na Uturuki.

Aliondoka Saudi Arabia mnamo Septemba 2017, baada ya kukosana na maafisa katika ufalme wa nchi hiyo.

Akiwa uhamishoni, alikuwa akiandikia gazeti la Washington Post Marekani nakala kali za kuukosoa utawala wa Saudia, na pia katika akunti yake ya Twitter ambako alikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 1.6.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jamal Khashoggi alisafiri sana kwenda Afghanistan, kumhoji Osama bin Laden

Usafiri kwenda Afghanistan

Mwandishi huyo mwenye miaka 59 aliianza kazi Saudi Arabia baada ya kuhitimu shahada kutoka chuo kikuu nchini Marekani mnamo 1985.

Alipokuwa akifanya kazi katika gazeti la al-Madina katika miaka ya 1990s, aliandika pakubwa kuhusu wanamgambo wa kiislamu nchini Afghanistan waliokwenda kupigana katika uvamizi wa USovieti.

Alifanya mahojiano mengi tu na raia wa Saudia, Osama bin Laden, ambaye anaarifiwa kumfahamu tangu ujana wake nchini Saudi Arabia.

Bin Laden kwa wakati huo alikuwa bado hajakuwa mtu anayefahamika sana katika mataifa ya magharibi kama kiongozi wa kundi la al-Qaeda.

Khashoggi alimtembelea katika mpango kwenye milima ya Tora Bora, na pia aliwahi kumhoji nchini Sudan pia mnamo 1995.

Khashoggi mwenyewe aliwahi kuhojiwa na gazeti la Ujerumani, Der Spiegel mnamo 2011 kuhusu uhusiano wake na Osama bin Laden.

Khashoggi alikiri kwamba anakubaliana na mitazamo ya bin Laden' katika siku za nyuma kuhusu kutumia mbinu zisizo za kidemokrasia kama kupenya katika mfumo wa kisiasa au kutumia mbinu za ghasia kuziondosha tawala fisadi katika mataifa ya kiarabu.

Kutetea mageuzi

Lakini tangu hapo, Mwandishi huyo aligeuka kuwa mojawapo ya watu waliozungumza wazi kuhusu maendeleo wa nchi hiyo, aliyenukuliwa na vyombo vya habari vya mataifa ya magharibi kama mtaalamu kuhusu masuala ya itikadi kali katika dini ya kiislamu.

Alionekana kama mtu aliye karibu na watawala wa Saudia, aliyekutana mara kwa mara na familia ya ufalme nchini humo.

Alishikilia nyadhifa tofuati na alifanya kazi na vituo kadhaa vya TV akinza kama mwandishi wa masuala ya nje ya nchi, hadi kuwa mhariri mkuu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hatice Cengiz, mchumba wa Jamal Khashoggi, raia wa Uturuki aliyefahamisha maafisa kwamba alitoweka

Kupasuka kwa wimbi la maandamano katika nchi za kiarabu

Kituo cha Al-Arab kilionekana kuwa mpinzani kwa shirika la utangazaji la Al-Jazeera, linalofadhiliwa na Qatar.

Lakini muda mfupi baada ya kuzinduliwa, kituo hicho cha televisheni kilichokuwa chini ya usiamamizi wa Khashoggi kilifungwa kwa kupeperusha mahojiano na kiongozi wa upinzani wa Bahraini.

Khashoggi kwa wakati huo pia alikuwa akihojiwa na vyombo vya habari vya mataifa ya nje, akishutumu ufalme wa Saudi Arabia, sakieleza kwamba kuna haja ya kuwa na mfumo wa kidemokrasia kuhakikisha utulivu wa nchi hiyo katika miaka ijayo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Polisi Uturuki wanashuku huenda mwandishi huyo aliuawa , tuhuma ambayo Saudia inakana vikali

Wakati maandamano ya machipuko katika nchi za kiarabu yalipoanza, kudai mabadiliko ya uongozi Khashoggi alikubaliana na upinzani uliotaka mabadiliko nchni Misri na Tunisia.

Msimamo wake ulikuwa kinyume na sera rasmi ya ufalme wa Saudia, uliotazama maandamano hayo kama tishio kwa uwepo wake.

Kukosana kuhusu Trump

Mnamo Desemba 2016, wakati mwanamfalme wa Saudia alipokuwa akijenga uhusiano na rais mpya wa Marekani Donald Trump, Khashoggi anaarifiwa kushutumu uhusiano huo.

Vyombo vya habari Arabuni vinaashiria uandishi wake kuhusu suala hilo ulipigwa marufuku kwa sababu hii.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Khashoggi alikuwa na wafuasi milioni 1.6 kwenye Twitter

Khashoggi pia alikosoa uamuzi wa serikali ya Saudia kuvunja uhusiano na Qatar, akiuomba uflame ushirikiane na Turkey kuhusu masuala ya kieneo, nchi ambayoni mshirika wa karibu na Qatar.

Mwandishi huyo wa zamani aliondoka Marekani mnamo Septemba 2017, akimshutumu kiongozi wa kudumu wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, kwa kulenga upinzani.

'Kujifanya kama Putin'

"Nimeondoka nyumbani kwangu, nimeiacha familia yangu na kazi yangu na ninapaza sauti yangu," alisema "kufanya jambo jingine lolote itakuwa ni kuwasaliti wanaoteseka gerezani. Naweza kuzungumza wakati wengi hawawezi."

"Naweza kusema Mohammed bin Salman anajifanya kama Putin. anatenda haki ki ubaguzi," aliandika katika nakala kwenye gazeti la Washington Post.

Aliendelea na shutuma zake dhidi ya kiongozi wa Saudia hadi alipoingia katika ubalozi huo mjini Istanbul.

Ndio mara ya mwisho alipoonekana.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii