Diane Reeves: Baada ya mpenzi wangu kuniambukiza HIV - hivi ndivyo nilivyopata haki

Haki miliki ya picha Diana Reeves

Diane Reeve hakutarajia kwamba atapata mpenzi tena baada ya ndoa yake ya miaka 18 kuvunjika.

Lakini mwaka 2002 , akiwa katika umri wa miaka 50 alifanikiwa. Aligundua kwamba mpenzi wake mpya Phillipe Padieu alikuwa akilala na wapenzi wengine na alikuwa amemuambukiza virusi vya HIV.

Nilikuwa nimetupilia mbali swala la mapenzi , lakini baadhi ya marafiki zangu walinishawishi kwamba nilikuwa mchanga sana kuchukua hatua hiyo na kusema kuwa ni muhimu kurudi katika soko- wakinipendekezea kuanza uhusiano wa mtandaoni.

Ilikuwa vigumu na nilikaribia kuachana na mpango huo wakati Phillipe aliponiulizia.

Ilikuwa kwa ufupi sana: Napenda picha yako na ningependa kukutana nawe, lakini nilivutiwa .

Alikuwa raia wa Ufaransa na alikuwa mwenye umbo zuri , na nikafikiria sawa kwa mara ya mwisho.

Tulikutana naye katika shule ya sanaa ya kijeshi na baadaye tukaelekea katika mgahawa mmoja na kupata kinywaji na kuketi hapo kwa saa moja tukizungumza.

Nilivutiwa sana na nadhani pia yeye. Alikuwa na hadithi nzuri na aliniambia mambo mengi kumuhusu, lakini sikuweza kujua iwapo pia yeye alikuwa akihisi nilivyohisi. Aliniambia neno moja la mapenzi na nikasema ''sawa' anahisi ninavyohisi'' na kuanzia wakati huo tukaanza na uhusiano wetu wa kimapenzi.

Haki miliki ya picha ALYSSA VINCENT PHOTOGRAPHY

Philippe alikuwa mchanganuzi wa maswala ya usalama katika kampuni moja kubwa lakini alifutwa kazi baada ya mwaka mmoja wa uhusiano wetu.

Wakati alipokuwa akitafuta kazi mpya nilimwambia anisaidie katika shule. Wakati alipokuwa akifunza kwa niaba yangu tulikuwa tukienda kujiburudisha baada ya kazi nyakati za usiku tukiwa pamoja.

Tulikuwa tukionana mara tata ama hata nne kwa wiki na muda mwengine wote nilikuwa nikifanya kazi shuleni.

Alifurahi sana nami pia nilifurahia sana na tulikuwa pamoja kwa miaka minne na nusu.

Mwaka 2006 mwanangu wa kike alikuwa akifunga ndoa na tulifanya sherehe nzuri ya kufana.

Phillipe alikuwepo-alipiga video ya sherehe hiyo kuu na baadaye tukaenda kula chakula cha usiku kama familia. lakini baadaye alinipigia simu yake ya rununu na kusema kuwa hajihisi vyema.

Haki miliki ya picha DIANE REEVE

Hakupiga simu kwa kutumia simu yake ya nyumbani, swala lililonifanya kuwa na wasiwasi na nilikasirika sana kwa sababu chakula kile cha usiku kilikuwa muhimu sana kwangu.

Nilienda peke yangu lakini nikiwa njiani nilifikiria kwamba ninaenda kwa mtu ambaye ameshindwa kuhudhuria chakula cha usiku cha harusi ya mwanangu.

Mlango ulikuwa umefungwa , nyumba ilikuwa imejaa giza na gari lake halikuwepo. Nilikaa karibu na njia iliokuwa ikielekea katika nyumba yake na kulia sana , na baadaye nikaanza kukasirika.

Kwa sabbau nilikuwa nikilipia simu yake nilikuwa na uwezo wa kupata jumbe za sauti yake . Wanawake wawili tofauti walikuwa wamemwachia ujumbe na ilikuwa wazi kutoka kwa sauti zao kwamba hawa ni wanawake aliokuwa na mipango nao.

Nilisubiri kwa takriban saa moja na nusu ama hata zaidi na baadaye nilimuona akitokezea kwa kona akija.

Wakati alipoona gari langu aliharakisha na kutoroka-aligundua kuna kitu kilichokuwa kikiendelea-hivyobasi nilimfuata hadi katika barabara za mji huo hadi alipoingia katika barabara kuu.

Alikuwa akiendesha kwa kasi ya mita 90 kwa saa na nilikuwa nyuma yake. ''Nilidhani kwamba ninaweza kukufukuza usiku kucha , gari langu lilikuwa limejaa mafuta ya kutosha''.

Hatimaye alisimamisha gari. Nilimpigia kelele na kumshutumu kwa kunidanganya na wapenzi wengine. Alisema, usingeingia na kusoma ujumbe wangu wa barua pepe.

Alikasirika sana na kuanza kulipiga gari hatua ilioniogopesha sana. Hivyobasi niliamua kwamba hapo ndio mwisho wetu.

Tuliachana siku ya Jumamosi .Jumatatu iliokuja nilifanyiwa ukaguzi na matokeo yalipotokea kulikuwa na utata katika seli zangu za uzazi.

Waliniambia kwamba ulikuwa ugonjwa wa HPV au Human Papiloma Virus .

Sikuwa nimewahi kusikia ugonjwa kama huo awali hivyobasi nilijua kwamba ameniambukiza. Hilo lilinishangaza na kunifanya kuwa na hofu- nililazimika kufanyiwa upasuaji ili kuondoa seli hizo zisizo za kawaida na sikujua kwamba huenda zikasababisha saratani au la.

Nilifikiria iwapo nilitakiwa kuwaonya wanawake wengine wawili . Nilipitia rekodi za simu za muda wa kipindi cha miezi tisa za Phillipe, nikijaribu kuzitafuta tena jumbe hizo.

Nilipiga simu na kila mara mwanamke alipojibu , nilimuuliza je una uhusiano wa kimapenzi na Phillipe Padieu? na iwapo wangesema ndio ningewaambia ningependa kuzungumza nawe kidogo.

Niligundua kulikuwa na wanawake wengine tisa ambao walikuwa wakishiriki naye kimapenzi.

Wengine walikasirika, wengine walizima simu zao huku wengine wakivutiwa sana na kutaka kujua zaidi nilichokuwa nikiwaelezea huku wengine wakinishukuru-nilipata majibu tofauti.

Mwanamke mmoja ambaye alikuwa katika uhusiano na Phillipe ambaye aliishi karibu naye alikasirika sana na akaamua kukutana na wanawake wengine . Tulikuwa na mkutano mzuri tukijadiliana na kupiga picha tukiwa pamoja na na baadaye kumtumia.

Kulikuwa na mwanamke mwengine ambaye niliwasiliana naye baadaye . Tulikutana katika kilabu kimoja cha muziki wa Jazz, alikuwa akikutana na Pillipe mara tatu kwa wiki kwa takriban mwaka mmoja na nusu.

Hakuwa na uhusiano wake na Phillipe pekee, lakini alikuwa akisubiri hilo litokee, nafikiria. Aliniambia kila kitu kilichotokea -vile mapenzi yao yalivyonoga kwa miaka kadhaa vile walivyokuwa wakijenga nyumba pamoja lakini wakaachana.

Nilimwambia kuhusu ugonjwa wa HPV na kwamba nilikuwa nikiendelea kupata ,matatizo ya kiafya.

Alisikiza kwa makini kile nilichomwambia. Nilimwambia kwamba huu ni uamuzi wako na iwapo unataka kuendelea na uhusiano wako naye ni uamuzi wake, na nilifikiria kwamba hiyo ndio mara ya mwisho tutazungumza.

Miezi mitatu baadaye nilipokea simu kutoka idara ya afya iliosema kuwa nilitakiwa kufanyiwa vipimo.

Nilijawa na wasiwasi kwa sababu nilikuwa nikikumbwa na matatizo tofauti ya kiafya mbali na seli za uzazi zisizo za kawaida.

Niliihifadhi simu ya Phillipe iwapo kuna mtu mwengine angelipiga. Niliaangalia tena baada ya kuwasiliana na idara ya afya na kugundua kwamba mtu wa mwisho kupiga simu alikuwa mwanamke niliyekutana naye katika kilabu cha pombe.

Nimpigia simu na kusema, Nilipokea simu kutoka kwa idara ya afya , je unaweza kuniambia nini kuhusu hilo? Aliniambia maneno manne ambayo sitasahau: Tunahitaji kuzungumza.

Aliendelea kuwasiliana na Phillipe baada ya sisi kukutana lakini akaamua kusitisha uhusiano wake naye. Alianza kuwa na wasiwasi kuhusu magonjwa ya zinaa na akaamua kwenda kupimwa.

Daktari wake alimpigia simu na kumwambia alikuwa akiishi na virusi vya HIV. Siku iliofuatia nilikutana na mkunga na wakachukua damu yangu.

Siku ya pili waliniita na matokeo. 'Diana pole una virusi''. Niliangusha simu na kuanguka kwa magoti .

Nilidhani nitaaga dunia. Sikuwa nimefuatilia ugonjwa wa HIV -nakumbuka kulikuwa hakuna tiba, na nilijua kulikuwa na dawa sasa, lakini sikujua athari yake-na nilijua kwamba mimi ninaugua sana.

Haki miliki ya picha ALYSSA VINCENT

Hiyo ilikuwa mwezi Januari 2007. Niliporudi kufanyiwa uchunguzi niligundua kwamba nilikuwa nimeambukizwa virusi vya Ukimwi. Hiyo inamaanisha kwamba kinga yako ya mwilki imeharibika hali ya kwamba mara kwa mara unaugua maambukizi. Mwili wako hauna nguvu za kukabiliana na virusi hivyo kwa kuwa kinga yake tayari imeharibika.

Hiyo ilikuwa mwaka 2007 mwezi Januari. Mara tu baada ya kupokea matokeo hayo alienda kwa watalaam wa kutoa ushauri nasaha.

Nilihitaji usaidizi ili kuelewa vitu. Nilikumbwa na msongo wa mawazo , nilijawa na hofu. Niliamua kuzungumza tena na mwanamke niliyekutana naye katika kilabu cha Jaz.

Tulilia pamoja na kukasirika pamoja. Alipopata matokeo yake angemwita Phillipe na kumuelezea. Naye alijibu ''hakuna la ajabu kila mtu hufariki kutokana na sababu fulani'' .

Kwa nini usiachane nami na kundelea na maisha yako? yalikuwa majibu mabaya kutoka kwa mtu ambaye alitarajiwa kupigwa na bumbuazi.

Tulishuku kwamba Phillipe alituambukiza sote wawili na tukafikiria kwamba lazima tuwe na kitu tutakachokifanya.

Tulifanya uchunguzi na katika majuma kadhaa tuliamua kuwasilisha ripoti kwa poilisi. Tuliwataka maafisa wa polisi kumzuia .

Tulitaka wafanya uchunguzi kubaini iwapo ni kweli alikuwa akibeba virusi hivyo na tulitaka kujua iwapo kuna kitu tunaweza kufanya ili kumzuia kuwaumiza wanawake wengine.

Maafisa wa polisi walituonea huruma na kutuelewa na kusema kwamba kwasababu ilikuwa sisi wawili pekee walituambia kwamba hatukuweza kuthibitisha.

Lakini iwapo wanawake wanne ama watano wangejitokeza wanasema ilikuwa rahisi kwa wao kupata wakili ili kuwasimamia. Tulirudi katika simu .

Haki miliki ya picha Diane Reeves

Mtu wa kwanza kumpigia alikuwa mwanamke aliyekuwa jirani wa Phillipe ambaye nilikutana naye mapema.

Alifanyiwa vipimo na kupatikana ana virusi vya HIV. Alitusaidia kwa kutazama nyumba hiyo na kuandika baadhi ya nambari za magari zilizokuwa zikiingia na kutoka katika nyumba ya Phillipe usiku kucha.

Tulikuwa na kazi nyingi kwa sababu alikuwa akikutana na wanawake tofauti kila siku lilikuwa jambo la kushangaza.

Nilikuwa na rafiki ambaye alikuwa na uwezo wa kubaini wamiliki wa magari hayo na kuweza kupata majina yao wanakoishi na tulipopata tulienda kuwatembelea.

Kwa jumla tulipata wanawake 13 ambao walipatikana na virusi vya HIV. Nilikasirika kwamba hili lilikuwa likiendelea kwa kipindi cha muda mrefu . Nilikuwa na uhusiano na Phillipe tangu 2002, lakini baadhi ya wanawake niliozungumza nao walikutana nami pamoja na wale waliokuwa wakiingia katika nyumba ya Phillipe kila usiku.

Huku kesi hiyo ikiendelea, idara ya polisi ilianza kushirikishwa. Ili kujaribu kuthibitisha kwamba Phillipe alijua kwamba alikuwa na virusi vya ugonjwa wa HIV , polisi ilitega kile ilichokitaja kuwa simu ya kuthibitisha kwamba ni kweli ana virusi vya ugonjwa huo.

Niliketi katika kituo cha polisi na kumpigia simu ili kujaribu kumfanya akiri kwamba alikuwa anajua kwamba alikuwa anaishi na virusi vya HIV .

Simu hiyo haikupata majibu ya kufurahisha.

Alisema , ulipataje nambari hii na hapo akaendelea kunijibu kwa kutumia matamshi machafu.

Nilimwambia, vipi, nilisikia kwamba ulikuwa hujisikii vyema na nilikuwa nakupigia simu nikujulie hali - akanikatia simu.

Kulikuwa na mwanamke katika idara ya afya ambaye alikuwa akitusaidia kuwatafuta wanawake hao . Nilimuuliza Je umewahi kumuona mwanamume huyu? lakini sikupata jibu lolote.

Baadaye nilikumbuka kwamba Phillipe mara nyengine hutumia jina Phil White, na akakumbuka jina hilo.

Ilikuwa mwaka 2005 takriban mwaka mmoja na nusu kabla ya uhusiano wetu kuvunjika . Alienda kwa daktari na kufamnyiwa vipimo. Nilimlipia matibabu aliyopewa hivyobasi nilitoa hundi na kuzipeleka hadi kwa wikili wa serikali-na hiyo ndio mara ya kwanza nilimuona akitabasamu.

Hundi hizo zilimpatia sababu ya kuweka notisi ya rekodi za matibabu . Bila notisi hiyo ingekuwa vigumu kuzipata kutokana na sheria za faragha na hivyo ndivyo tulivyothibitisha kwamba alipatikana na virusi vya HIV. Kati ya wanawake 13 waliopatikana na virusi vya ukimwi ni watano pekee waliokuwa kutoa ushahidi mahakamani kutokana na unyanyapaa unaoshirikishwa na virusi hivyo.

Tulianzisha kundi la msaada na tukaweza kukutana katika nyumba yangu mara kwa mara. Sote tuliweza kukabiliana na janga lililokuwa likitukumba.

Lengo muhimu la kuanzisha kundi hilo lilikuwa kuhakikisha kuwa jimbo la Texas litalipia matibabu yanayohitajika kutokana na uhalifu, na walikuwa wakimshtaki Phillipe kwa unyanyasaji wa kutumia kifaa kinachoweza kuuwa.

Ulikuwa mchakato mrefu uliochukua takriban kati ya miezi mitano na sita, kwa sisi kuwatafuta wanawake. Ilikuwa inachosha-bado nilikuwa na ukimwi lakini tulikuwa tukitumia kila njia kumzuia kuambukiza wanawake wengine.

Kesi hiyo hatimaye ilianza 2009, miaka mitatu baada ya uhusiano wangu na ule wa Philippe kuvunjika na miaka miwili baada ya mimi kupatikana na virusi hivyo.

Afisa wa serikali alituonya kwamba tutaingia katika mkaa na kwamba chochote kile kilichojulikana na Phillipe kuwahusu ambacho kilikuwa na uchafu kitatangazwa kwa umma.

Ijapokuwa nilikuwa tayari kukabiliana na lolote lile nilikuwa kizimbani kwa takriban saa moja na baadaye nikasahau.

Baada ya hukumu kutolewa, tulifanya mkutano ulioshirikisha rafiki zetu na jamii zetu pamoja na kusherehekea kwa sababu tulijua hakuweza tena kumuumiza mwanamke mwengine tena.

Phillipe hakujitwika majukumu. Alisema kuwa ni mimi ndiye niliyewaambukiza watu wote hao HIV , licha ya kwamba tulikutana na mwanamke mmoja mjini Michigan ambaye alikuwa amemuambukiza HIV 1997.

Na pia sisi tulifanya vipimo vya DNA ambavyo vilithibitisha kuwa virusi vilivyokuwa ndani yetu vilitoka kwa mtu mmoja na kwamba Phillipe ndiye aliyevisambaza kwetu.

Nashuku kwamba alikuwa akisambaza virusi hivyo kwa wanawake kwa miaka mingi kabla ya kumgundua na kwamba kupatikana kwa ugonjwa huo katika damu yake hakukuwa maya ya kwanza.

Lakini kitu kimoja ambacho Phillipe alinifanyia mimi na wenzangu ni kwamba aliharibu uwezo wetu wa kuamini na hivyobasi inafanya uhusiano kuwa mgumu sana, licha ya kwamba sasa nina uhusiano mzuri na mtu anayenielewa na ananipenda na kunikubali.

Dawa zimekuja kufikia sasa na nalazimika kumeza tembe moja kwa siku.

Virusi nilivyonavyo haviwezi tena kuonekana katika damu yangu. Imebainika kwamba iwapo unaishi na virusi vya ukimwi na virusi hivyo haviwezi kuonekana tena basi hatari ya maambukizi haipo tena.

Phillipe Padieu na silaha yake ya maangamizi aliyokuwa akiitumia alihukumiwa kifungo cha miaka 45 jela

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii