Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 20.10.2018: Man United, Chelsea, Barcelona, Real Madrid, Hazard, Mourinho, Martial, Asensio, Leroy Sane

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anaamini kwamba Hazard ataisaidia Chelsea kushinda taji la ligi ya Uingereza msimu huu. (Daily Star)

Mshambuliaji wa man United Anthony Martial ,22, ambaye hana kandarasi na klabu hiyo mwisho wa msimu huu analenga kuondoka katika klabu hiyo. (Mirror)

Mchezaji anayelengwa na Tottenham na Juventus Anthony Martial amekataa ofa kadhaa za kuandikisha kandarasi mpya na United. (RMC Sport via Calciomercato)

Anthony Martial

Nahodha wa klabu ya Juventus Giorgio Chiellini, 34, amemwambia kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, kwamba anakaribishwa tena katika klabu hiyo ya Itali.. (Mirror)

Chelsea itajaribu kumsaini mshambuliaji mpya mnamo mwezi Januari baada ya kupoteza subira na mshambuliaji Alvaro Morata, 25. (Sun)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa mchezaji wa Borussia Dortmund na Uingereza kinda Jadon Sancho huenda asirejee katika klabu hiyo katika kipindi chake cha ukufunzi. (Manchester Evening News)

Manchester City imeanza mazungumzo na winga Leroy Sane, 22, kuhusu kumuongezea kandarasi yake , licha ya kwamba raia huyo wa Ujerumani ana takriban miaka miwili na nusu iliosalia katika kandarasi (Telegraph)

Winga Leroy Sane

Arsenal iko katika nafasi nzuri ya kumsaini mshambuliaji wa Roma na Uturuki Cengiz Under ,21, ambaye amehusishwa na uhamisho wa klabu ya Bayern Munich. (Forza Roma via Daily Express)

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri amemwambia nyota wa klabu hiyo Eden Hazard, 27, anaweza kushinda kila kitu, ikiwemo Ballon d'Or - iwapo atasalia Stamford Bridge. (Talksport)

Maurizio Sarri anasema kuwa hana hamu ya matamshi ya babake beki Andreas Christensen kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa ,22, huenda atandoka katika klabu hiyo iwapo hakuna hakikisho la yeye kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha timu(Times - subscription required)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anaamini rekodi nzuri ya ulinzi ya timu hiyo imekumbwa na changamoto kutokana na mchezo wa kushambulia wa klabu hiyo.. (Guardian)

Marco Asensio

Real Madrid imejiandaa kumuuza Marco Asensio, anayelengwa na Liverpool na Chelsea. (Marca via Sun)

Chelsea inataka mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 25, kuchukua mahala pake Alvaro Morata, 25, huku mchezaji wa AC Milan Patrick Cutrone, 20, akitajwa kuwa mchezaji mbadala anayeuzwa kwa bei nafuu. (Sun)

Beki wa Juventus Alex Sandro, 27, ambaye alihusishwa na uhamisho wa kuelekea Paris St-Germain na Manchester United msimu huu , bado hajaongeza kandarasi yake na klabu hiyo ya Itali kutokana na tofauti kuhusu mshahara. (Calciomercato)

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa amekerwa na shutuma za hivi karibuni ambazo amekuwa akipokea na timu yake (Sky Sports)

Eric Abidal

Murugenzi wa klabu ya Barcelona Eric Abidal anaandaa kununua beki wa muda iwapo beki wa Ufransa Samuel Umtiti, 24, hatoweza kuzuia upasuaji katika goti (Marca)

Mchezaji wa Uingereza England Ben Chilwell, 21, anaendelea na majadiliano ya kuweka kandarasi mpya na klabu ya Leicester City . (Leicester Mercury)

Nahodha wa zamani wa timu ya Uingereza Wayne Rooney anaamini kwamba angesalia kuwa mchezaji wa Everton iwapo angeendelea kucheza kama mshambuliaji msimu uliopita. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa Newcastle United Rafael Benitez anasema kuwa haogopi kufutwa kazi , licha ya klabu hiyo kuwa chini ya (Telegraph)

Winga wa zamani wa Newcastle Chris Waddle anasema kuwa mashabiki wa klabu hiyo hawatamlaumu mkufunzi Rafael Benitez kuondoka katika klabu hiyo kwa ukosefu wa. (Newcastle Chronicle)

Tetesi za soka Ijumaa 19.10.2018

Alexis Sanchez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexis Sanchez alijiunga na Manchester United akitokea Arsenal Januari, naye Henrikh Mkhitaryan akahamia Arsenal

Alexis Sanchez anatafakari kuihama Manchester United miezi tisa baada ya mchezaji huyo wa kiungo cha mbele mwenye umri wa miaka 29 kuwasili kutoka Arsenal. (Mail)

Real Madrid imewasiliana na aliyekuwa meneja wa Chelsea Antonio Conte kuhusu kupokea jukumu la kusimamia klabu hiyo kutoka kwa Julen Lopetegui, aliyesalia na mechi tatu kuuokoa wadhifa wake licha ya kwamba ameajiriwa msimu huu wa joto. (Corriere dello Sport )

Mshambuliaji wa Liverpool na England Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 29, yu tayari kusaini mkataba kuongeza muda wake kucheza Anfield. (Sun)

Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United Wes Brown anasema mchezaji wa Chelsea Eden Hazard anatumia mbinu sawa na za Cristiano Ronaldo kushinikiza uhamisho kwenda Real Madrid. (Express)

Lakini timu ya the Blues inatumai kuidhinisha mazungumzo ya mkataba na Hazard mwezi ujao kujaribu kumshawishi raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 27 akubali kuahidi mustakabli wake huko Stamford Bridge. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ibrahimovic, anasema atakataa kurudi Manchester United Januari

Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic, aliye na miaka 37, anasema atakataa kurudi Manchester United mwezi Januari wakati msimu ukimalizika wa ligi kuu ya soka. (Sky Sports kupitia Metro)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Man United raia wa Ufaransa, Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 22, amekataa mapendekezo kadhaa ya mkataba mpya kutoka klabu hiyo.(RMC Sport)

Kikosi cha Barcelona kinaweza kumkaribisha mchezaji wa kiungo cha mbele wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, mwenye umri wa miaka 26, katika klabu hiyo tena iwapo ataamua kurudi tena katika timu hiyo ya mabingwa wa Uhispania kutoka Paris St-Germain. (Mundo Deportivo )

Chelsea imekosa subira na mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, mwenye umri wa miaka 25, na itajaribu kupata mchezaji mwingine wa kuichukua nafasi yake Januari. (Sun)

Arsenal ina hamu kumsajili beki wa shoto wa Liverpool Alberto Moreno, huku timu hiyo ya the Reds ikikubali kumpoteza mchezaji huyo wa Uhispania mwenye miaka 26 kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Image caption Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Liverpool Divock Origi

Liverpool itaomba kitita cha zaidi ya £ milioni 20 kwa mchezaji wa kiungo cha mbele Divock Origi, mwenye miaka 23, iwapo raia huyo wa Ubelgiji ataondoka Januari. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, ambaye kwa sasa amechukuliwa na AC Milan kwa mkopo, anasema alilazimishwa kuondoka Juventus ili kutoa nafasi kwa ujio wa Cristiano Ronaldo. (Gazzetta dello Sport )

Tazama pia hii:

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez ameambiwa hatopewa fedha zaidi kununua wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho Januari. (Chronicle)

Aliyekuwa beki wa kati wa Manchester United Gary Pallister amemshutumu Romelu Lukaku baada ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji kusema anatumai kucheza katika Serie A huku kukiwepo fununu zinazomhusisha na uhamisho kwenda Juventus. (Star)

Bosi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema hana majuto kuhusu klabu hiyo kutomsajili mchezaji yoyote msimu wa joto. (Telegraph)

Bora kutoka Alhamisi

Nyota wa Brazil Neymar, 26, anajutia uamuzi wake wa kuondoka Barcelona na kujiunga na Paris St-Germain na kwamba yuka radhi kurejea Nou Camp mwisho wa msimu huu. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Wachezaji mahiri wa Ufaransa katika klabu ya Barcelona wanamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, kujiunga na klabu hiyo. (Mail)

Andreas Pereira, 22, wa Manchester United amethibitisha majibizano makali kati ya Pogba na meneja wake Jose Mourinho yalitokana na tofauti kuhusiana na video katika mtando wa kijamii wa Instagram. (Manchester Evening News)

Mfaransa mwenzake katika klabu hiyo, Hugo Lloris anasema kuwa Pogba anahukumiwa kimakosa kwa sababu ya thamani yake ya euro milioni 89m. (Mirror)

Manchester United na Liverpool wanamfuatilia winga wa PSV Steven Bergwijn wa miaka 21. (De Telegraaf, via Sun)

Arsenal ni klabu ya hivi punde kuhusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Italia na Cagliari, Nicolo Barella, 21. (Gazetta dello Sport, via Football London)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meneja wa Everton Marco Silva

Meneja wa Everton Marco Silva amesema "Manahodha wangu wawili" Phil Jagielka, 36, na Leighton Baines, 33, bado wana majukumu muhimu ya kufanya katika klabu hiyo- na kusisitiza kuwa mashauriano kuhusu kandarasi mpya ziwekwe kando kwa ajili ya siku zijazo. (Liverpool Echo)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii