Bahati nasibu nchini Marekani yaweka historia mpya ya dola bilioni 1.6

A store selling Mega Millions lottery tickets in Washington DC Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bahati nasibu nchini Marekani yaweka historia mpya ya dola bilioni 1.6

Bahati nasibu nchini Marekani imefika rekodi mpya ya dola bilioni 1.6 baada ya wale wanaocheza kukosa kupata tikiti kwenye droo ya Mega Millions ya dola biloni 1.

Shindano hilo ambalo watu 15 walishinda dola milioni moja kila mmoja lilishuhudia milolongo kwenye vituo kote nchini siku ya Ijumaa kununua tikiti.

Sasa droo nyingine itafanyika siku ya Jumanne. Tikiti hizo zinazouzwa kwenye majimbo 44 nchini Marekani hazijapata mshindi tangu mwezi Julai.

Shindano hilo lilibuniwa mwaka 2002.

Baadhi ya Ushindi wa fedha nyingi Marekani

  • $1.58bn: Ushindi wa Powerball mwaka 2016. Fedha hizo ziligawanwa mara tatu kati ya washindi waliokuwa na tikiti kutoka California, Florida na Tennessee
  • $758.7m: Ushindi wa mwaka 2017 na mama wa watoto wawili Mavis Wanczyk kutoka Massachusetts.
  • $656m: Ushindi wa Mega Millions mwaka 2012, uliogawanwa kati ya washindi watatu kutoka Maryland, Kansas na Illinois
  • $648m: Ushindi mwingine wa Mega Millions mwaka 2013 na watu wawili; mwanamke kutoka Georgia na mwanamume kutoka California
  • $590.5m: Ushindi wa Powerball jackpot ulioshindwa na mwanamke mwenye miaka 84 kutoka Florida

Mada zinazohusiana