''Nilijikuta niko chini, ni  kama mtu kapigwa ngwara''
Huwezi kusikiliza tena

Alphonse Augustino Cherehani: Injinia aliyenusurika baada ya kuzama MV Nyerere

Jina la Injinia Augustino Cherehani lilianza kuvuma katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania siku tatu baada ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake katika ziwa Victoria kati ya kisiwa cha Ukerewe na Ukara. Injinia Augustine Cherehani katika kile kilichowaacha wengi vinywa wazi aliokolewa wakati tumaini la kupata walio hai likiwa limesha malizika. Amemsimulia mpiga picha wa BBC Swahili Eagan Salla