Sabarimala: Mungu asiyetaka wanawake katika hekalu lake

Mungu wa kihindi
Image caption Wanawake wawili wanajaribu kuingia hekaluni

Kwa mara ya kwanza, hekalu la Sabarimala lililopo katika mji wa Kerala kusini mwa India wiki hii limefungua milango yake kwa wanawake wa kila rika baada ya uamuzi wa kihistoria wa Mahakama kuu.

Hata hivyo hakuna mwanamke yoyote aliyeingia kwani waandamanaji wenye kuzusha wenye fujo wamezuia njia.

Wanawake wawili, mwandishi Kavitha Jagdal na mwanaharakati wa masuala ya kijamii, Rehana Fathima walifanikiwa kufika katika eneo la hekalu hilo siku ya Alhamisi.

Polisi zaidi ya 100 waliwalinda kuzuia mawe waliyokua wanatupiwa na waandamanaji walipokuwa wakitembea kilomita tano sawa na maili tatu kuelekea kwenye hekalu hilo.

Lakini iliwalazimu kurudi baada ya kusimamishwa na wafuasi wa hekalu hilo mita chache kutoka kwenye hekalu hilo.

Waandamanaji pia wamejumuisha wanawake wengi ambao wameshiriki katika migomo, kuziba barabara na kukagua magari yanayo kwenda hekaluni yakiwa yamebeba mwanamke yoyote yule aliye kati ya umri wa kupata hedhi ya kila mwezi. Wakizingatia zaidi umri wa miaka 10 mpaka 50.

Hekalu hilo linavutia mamilioni ya wafuasi kutoka pembe zote za nchi ya India.

Kwanini wanaandamanaji wamekasirika?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Baadhi ya wanawake wanaona ni upendeleo kunyimwa kuingia hekaluni

Baadhi ya wapinzani wanaopinga kwa nguvu zote maagizo ya mahakama kuu kufutilia mbali sheria ya kuzuia wanawake kuingia katika hekalu hilo, ni kwasababu waandamanaji wanaamini kuwa agizo hilo linakwenda kinyume na matakwa ya mungu Ayappa mwenyewe.

Waumini wa dini ya Kihindu wanawachukulia wanawake wanaopata hedhi kuwa ni najisi na huwazuia kushiriki katika shughuli za kidini.

Wakati mahekalu mengi ya Wahindu yanawaruhusu wanawake kuingia ilimradi wakiwa hawapo katika hedhi, hekalu la Sabarimala ni moja kati ya mahekalu machache ambayo huwazuia kabisa wanawake walio katika umri wa kupata hedhi kuingia hekaluni.

Wafuasi wa dini ya Kihindu wanasema marufuku ya wanawake kuingia katika hekalu hilo si kwasababu ya hedhi pekee, ni kwasababu ya kutii matakwa ya Mungu wao ambaye inaaminika kuwa aliweka wazi taratibu za kufuata ili kupata baraka zake.

Haki miliki ya picha Kaviyoor Santhosh
Image caption Kuna sababu mbali mbali za kuzuia wanawake kuingia hekaluni ikiwemo hedhi

Kila mwaka mamilioni ya wafuasi wa kiume wanatembea kupanda katika kilima bila kuvaa viatu mpaka juu ili kuliona kaburi. Lakini pia hufunga - funga kavu - kwa siku 41 na kuepuka kabisa kuvuta sigara, pombe, nyama, ngono na kuwasiliana na wanawake walio katika hedhi kabla ya kuanza safari.

Hekaya ya mungubwana Ayappa

Kila mungu katika imani ya Kihindu ana haiba yake na upekee wa visa vyake mwenyewe, na mungu Ayappa hana tofauti.

Kwa mujibu wa kisa cha hekalu, mungu Ayyappa hana mahusiano kwani amechukua kiapo cha useja, yaani kutoishi na mwanamke.

Kuna visa kadhaa kuhusu suala hilo, kwa mujibu wa hadithi, Ayappa alizaliwa baada ya muungano kati ya miungu wawili wa kiume ambao wamempa nguvu na uwezo wa kumshinda pepo wakike ambaye alikuwa akisumbua hadi wakati huo.

Juu ya kumshinda, ilifunuliwa kwamba alikuwa ni binti mdogo ambaye alilaaniwa kuishi maisha ya pepo.

Pepo hilo lilimpenda kimapenzi mungu Ayappa na kumuomba amuoe, lakini Ayappa alikataa na kusema kuwa yeye amekusudiwa kwenda msituni na kujibu maombi ya wafuasi wake.

Kwa nini kutekwa kwa MO kumeacha kishindo?

Pepo hilo la kike liliendelea kumbembeleza, akamjibu kuwa atamuoa siku ambayo wafuasi wapya wataacha kwenda kufuata baraka zake. Siku ambayo haija wahi kutokea.

Hadithi zinasema kwamba anamsubiria katika hekalu la pili ambalo lipo njiani kuelekea kwenye kaburi kuu la Sabarimala.

Wanawake hawaendi kwenye mahekalu hayo, kwa imani kwamba wakifanya hivyo watakuwa wanatukana mungu na kujitoa kwa mwanamke aliyempenda.

Kwa mujibu wa hadithi nyingine, Bwana Ayappa alikuwa mwana mfalme ambaye alikomboa ufalme wake kutoka kwa mvamizi wa kiarabu aliyeitwa Vavar.

Baada ya mapigano, Vavar akawa mfuasi mtiifu wa mwanamfalme. Pia kuna kaburi ambalo lina wakfu wake karibu na hekalu la Sabarimala. Inasemekana yeye huwalinda wahamiaji wanaokuja kuomba baraka zake.

Katika toleo hili, bwana Ayappa hatimaye aliweka nadhiri kujibu maombi ya kila mfuasi ambaye alikuja kwake, na alijiondolea kabisa hamu yote ya kidunia ikiwa ni pamoja na mahusiano na wanawake, ambapo ndio moja ya sababu ya kwa nini wanawake hawaruhusiwi ndani ya hekalu lake.

Inaweza pia kukawa na historia nyingine zinazohusiana na mungu Ayappa na kwa nini wanawake hawaruhusiwi ndani ya hekalu lake.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Baadhi ya wafuasi wanasema hawatarudi kwenye hekalu hilo kama uamuzi wa mahakama utatekelezwa

Waandamanaji wanasema nini?

"Hakuna shangwe miongoni mwa wanawake ambao ni wafuasi wa imani ya Kihindu, kwani wamefadhaika sana," ameandika Vineetha Menon katika jarida la Organiser.

Menon anajenga hoja kuwa wanawake wasiingie hekaluni ni "kutimiza nia ya mungu Bhava"

Baadhi ya wafuasi wanaume wanasema kwamba hawata rudi katika hekalu hilo kama maamuzi ya mahakama yatatekelezwa.

"Tumekuwa tukija katika hekalu hili kwa miaka 30 sasa. Lakini tunaweza tusirudi hapa kwasababu wanawake kuingia hekaluni ni kuharibu mfumo wa imani yetu na kanuni takatifu, Murugan, mfuasi alimwambia mwandishi wa BBC India Imram Qureshi.

Hata hivyo maamuzi hayo ya mahakama yamewagawanya mahakimu waliotoa hukumu hiyo.

Mgahawa ambapo wateja hulipa kwa njia ya Bitcoin Kenya

Indu Malhotra, hakimu pekee wa kike alipinga hukumu iliyotolewa.

"Maswala ya ndani ya kidini kwa kawaida hayatakiwi kuingiliwa na mahakama, na hata dhana ya usawa haiwezi kuibuliwa katika mambo ya kidini," alisema kwa maoni yake.

Wanawake wamekuwa wakidai kuingia katika hekalu hilo kwa miongo kadhaa sasa. Lakini mwaka 2016 taarifa ya utata kutoka kwa chifu wa hekalu hilo iliibua maandamano upya.

Prayar Gopalakrishnan anasema kuwa ataruhusu wanawake kuingia endapo itagundulika mashine ambayo inaweza onyesha kama mwanamke yupo kwenye hedhi au la.

Saudia yabanwa mbavu mauaji ya Khashoggi

Waendesha mashtaka walitumia na kunakili kauli hiyo kama mfano na kusema kuwa miongozo ya hekalu hilo ina vunja usawa ulio hakikishwa kwa wahindi wote kupitia katiba ya nchi. Waliongeza kuwa ilikuwa ni upendeleo na kuwanyima wanawake haki yao ya kuabudu.

Waandishi wa habari wanasema kuwa mapigano kati ya waandamanaji na polisi yanaweza kuongezeka katika siku zijazo kwani wanawake zaidi wanatarajiwa kujaribu kuingia hekaluni.

Mada zinazohusiana