Daraja la Hong Kong-Zhuhai: Daraja refu zaidi duniani kwa picha

Daraja refu zaidi duniani ambalo lina umbali wa 55km (maili 34), linalofahamika kama daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macau limefunguliwa rasmi.

Daraja hilo linapatikana katika mlango wa Mto Pearl na linasifiwa kama ufanisi mkubwa wa kihandisi.

Stretch of the Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha Getty Images

Daraja hilo lina pia njia ya chini kwa chini na linaunganisha visiwa vya Hong Kong na China bara kupitia Macau.

Daraja la Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha Reuters

Kutoka mwanzo wake hadi mwisho wake, ukishirikisha pia barabara mbili zinazoliunganisha, daraja hilo urefu wake ni mara 20 zaidi ya daraja maarufu la Golden Gate linalopatikana San Francisco.

Stretch of the Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha Reuters

Daraja hilo limejengwa kuhimili mitetemeko ya ardhi na vimbunga ambavyo mara kwa mara hukumba eneo hilo.

Limejengwa pia kuhimili kugongwa na meli iwapo ajali kama hiyo itatokea.

View from the shore of the bridge as it becomes an under-sea tunnel Haki miliki ya picha AFP

Ili kuziwezesha meli kupitia mlango huo wa mto, daraja hilo linafikia wakati na kuingia chini ya maji, na kuwa barabara ya chini kwa chini ya urefu wa 6.7km, kupitia visiwa viwili bandia, kwa maana kwamba visiwa hivyo ni vya kujengwa na si asilia.

Stretch of the Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha Reuters

Mradi huo wa ujenzi unapitia katika eneo ambalo hupitia ndege zikipaa na zikienda kutua katika uwanja wa kimataifa wa Hong Kong.

Hii iliwalazimu wahandisi kuhakikisha kwamba daraja hilo haliendi juu sana.

Stretch of the Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha Reuters

Ujenzi wa mradi huo ulianza mwaka 2009 lakini ulicheleweshwa mara kwa mara na pia kukawa na wasiwasi kuhusu usalama wake.

Aidha, gharama yake ya ujenzi imekuwa ikipanda mara kwa mara na kwa jumla sasa inakadiriwa limegharimu zaidi ya $20bn (£15.3bn).

Toll booths at the Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha AFP

Mwanzoni ilitarajiwa daraja hilo lingefunguliwa rasmi mwaka 2016 lakini hata tarehe kamili ya uzinduzi wake mwezi huu haikuwa imethibitishwa, hadi ilipobainishwa jana kwamba lingezinduliwa leo.

Stretch of the Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha Reuters

Sio tu kwamba ujenzi wa daraja hilo umepita bajeti pia na muda uliokadiriwa kutumika kulijenga bali pia limegharimu maisha ya watu.

Maafisa wa Hong Kong na China wanasema kwamba wajenzi tisa walifariki wakati wa ujenzi wa daraja hilo.

Stretch of the Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha AFP

Daraja hili linaunganisha maeneo matatu ya China - mawili ni ya utawala maalum ya Makau na Hong Kong na eneo la tatu ni China bara.

Hii ina maana kwmaba daraja hili linapitia maeneo yenye mifumo tofauti ya kisheria na kisiasa.

Stretch of the Hong Kong Macau bridge Haki miliki ya picha Reuters

Mabasi na magari ya kibiashara yatasafirisha abiria na mizigo kupitia daraja hilo.

Teksi hata hivyo haziruhusiwi na ni magari machache sana ya kibinafsi ambayo yataruhusiwa kupita.

Signs in an empty immigration hall in Hong Kong Haki miliki ya picha EPA

Mtu anapokuwa anasafiri kati ya Hong Kong na China bara huhitajika kuwa na visa. Vituo viwili vya uhamiaji vimejengwa kuwahudumia watu watakaokuwa wanatumia daraja hilo kusafiria.

Tunnel entrance at Hong Kong Macau expressway Haki miliki ya picha Reuters

Nini sababu ya kulijenga daraja hili? Kuokoa muda. Safari kupitia mlango huo wa mto huchukua zaidi ya saa nne. Sasa kwa kutumia daraja hilo, safari hiyo itachukua dakika 30 pekee.

Night view of the Hong Kong-Macau-Zhuhai bridge Haki miliki ya picha Reuters

Lakini baadhi ya wakazi Hong Kong wamekosoa nia ya kujengwa kwa daraja hilo, wakisema hakuna anayelihitaji sana.

Wanasema zaidi ni jaribio la kuiunganisha zaidi Hong Kong na China bara kikamilifu.

Hong Kong ni eneo linalojitawala ambalo lilikuwa koloni ya Uingereza hadi lilipokabidhiwa tena kwa China mwaka 1997.

Unaweza kusoma pia:

Picha zote zina hakimiliki

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii