Jamal Khashoggi: Wafahamu watu wanaodaiwa kumuua mwanahabari Khashoggi

CCTV pictures made available through the Turkish newspaper Sabah allegedly showing Saudi citizens who Turkish police suspect of involvement in the disappearance of Jamal Khashoggi (2 October 2018) Haki miliki ya picha EPA

Vyombo vya habari nchini Uturuki vimewaorodhesha raia 15 wa Saudi Arabia ambao mamlaka nchini humo zinawashuku kuhusika katika mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.

Khashoggi raia wa Saudia alikuwa mkosoaji kinara wa sera za Mwanamfalme Mohammed Bin Salman mara ya mwisho alionekana akiingia ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2 na kuuawa akiwa ndani.

Awali Saudia walidai kuwa mwanahabari huyo ambaye alikuwa akiishi Marekani alitoka ndani ya ubalozi wake. Baada ya shinikizo wakasema kuwa aliuawa alipojaribu kupambana na baadaye wakakiri kuwa aliuawa katika opersheni isiyo rasmi na ambayo haikubarikiwa na Bin Salman.

Wengi wa washukiwa hao 15 waliingia Uturuki saa chache kabla ya Khashoggi kuingia kwenye ofisi za ubalozi kufuatilia nyaraka kuhusu ndoa yake na kuondoka Uturuki siku hiyo hiyo wakitumia ndege binafsi za kukodi.

Mamlaka za Uturuki zinaamini kuwa washukiwa hao ni maafisa wa uslama na majasusi wa serikali ya Saudia, tuhuma amabazo zinathibitika kwa vyanzo vya kiupelelezi vilivyowazi.

Washukiwa hao ni wafuatao;

Salah Muhammed A Tubaigy, 47

Haki miliki ya picha AFP

Dkt Tubaigy ni daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa ya binadamu ikiwemo uchunguzi wa sababu za vifo. Daktari huyo alipata shahada yake ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Glasgow, Uskochi na mwaka 2015 alifanya kazi kwa miezi mitatu katika kituo cha uchunguzi wa kitabibu cha Victorian nchini Australia.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Tubaigy anajitambulisha kama mkuu wa Baraza la Wachunguzi wa Matibabu wa Saudia. Ukurasa huo unauhusiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia.

Maafisa wa Uturuki wananadai kuwa Dkt Tubaigy alitua katika uwanja wa ndege wa Istanbul akiwa na msumeno. Daktari huyo aliingia Uturuki alfajiri ya Oktoba 2, na kufikia hoteli ya Movenpick iliyopo mita 500 kutoka katika ofisi za ubalozi wa Saudia. Aliondoka Uturuki siku hiyo hiyo saa 5 kasoro dakika nne usiku.

Inadaiwa sauti ya daktari huyo inasikika katika mkanda wa sauti ulionasa tukio la kuteswa kisha kuuawa kinyama kwa Khashoggi. Yanaiwa sauti ya mtu anayetambulika kama daktari ilikuwa ikiwaita wengine wasikilize muziki wakati akimkata Khasoggi vipande vipande.

Dkt Tubaigy hajazungumza kitu mpaka sasa, lakini bwana mmoja aliyejitambulisha kama mjomba wake ameandika katika mitandaoni kuwa daktari huyo hawezi kushiriki unyama kama huo.

Maher Abdulaziz M Mutreb, 47

Haki miliki ya picha AFP

Mutreb inaaminiwa kuwa alifanya kazi kwa miaka miwili katika Ubalozi wa Saudia jijini London.

Chanzo kimoja cha mambo ya ujasusi kimeiambia BBC kuwa bwana huyo ni afisa usalama Saudia na alikutana naye mwaka 2011 alipomfunza matumizi ya teknolojia ya ujasusi iitwayo spyware.

CNN pia wamemnukuu mtoa taarifa wao mmoja ambaye amemtaja Mutreb kuwa Kanali wa kikosi cha ujasusi cha Saudia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maher Mutreb anaonekana kushoto mwa picha hii (aliyekunja mikono) alipoambatana na Mwanamfalme Mohammed Bin Salman alipotembelea chuo cha Massachusetts Institute of Technology, Marekani mwezi Machi.

Picha mbali mbali zinaonesha aliambatana na Bin Salman katika matukio matatu tofauti mwezi Machi mwaka huu kitu kinachoashiria kuwa alikuwa sehemu ya ulinzi wa Mwanamfalme huyo.

Gazeti lililoupande wa serikali ya Uturuki la Sabah limetoa picha za CCTV zinazoonesha kuwa Mutreb aliingia ofisi ndogo za ubalozi Istanbul saa 4:55 asubuhi ikiwa ni takriban saa tatu kabla ya Khashoggi kuingia katika ofisi hizo.

Mutreb anaaminika kuingia Uturuki akitumia ndege moja na Dkt Tubaigy yenye namba ya usajili HZSK2 na alifikia Movenpick pia, Aliondoka na ndege nyengine ya kukodi ya HZSK1 SAA 12:40 jioni ya siku hiyo hiyo.

Abdulaziz Mohammed M Alhawsawi, 31

Haki miliki ya picha AFP

Gazeti la New York Times limemtaja jasusi mmoja wa Ufaransa ambaye amewahi kufanya kazi na familia ya Kifalme ya Saudia ambaye amemtambua Alhawsawsi kuwa moja ya walinzi wanaombatana na Bin Salman.

Alhawsawi aliingia Istanbul kwa kutumia ndege ya abiria usiku wa saa 7:43 na akafikia katika hoteli ya Wyndham Grand Istanbul Levant iliyopo kilometa 1 kutoka ubalozi wa Saudia. Aliondoka Istanbul kwa ndege ya HZSK2 pamoja na Dkt Tubaigy.

Thaar Ghaleb T Alharbi, 39

Haki miliki ya picha AFP

Mwezi Oktoba mwaka jana, mtu mwenye jina kama hilo ambaye alikuwa akifanya kazi katika kikosi cha ulinzi wa familia ya kifalme alipandishwa cheo kwa ushujaa wake katika kumlinda mwanamfalme Bin Salman. Katika tukio hilo mtu mwenye silaha aliwauwa walinzi wawili kabla ya kuuawa.

Alharbi aliingia Uturuki na ndege ya HZSK2 na kufikia Mövenpick, kisha akaondoka na ndege ya HZSK1.

Mohammed Saad H Alzahrani, 30

Haki miliki ya picha AFP

Mlinzi aliyevalia magwanda yenye jina kama hilo alipigwa picha na kurekodiwa akiwa na Bin Salman mwaka 2007 kwamujibu wa mwanaharakati Iyad el-Baghdadi.

Alzahrani aliingia Istanbul kwa kutumia ndege ya kukodi na kufikia hoteli ya Wyndham Grand na kuondoka kutumia ndege ya HZSK2.

Khalid Aedh G Alotaibi, 30

Haki miliki ya picha AFP

Gazeti la Washington Post linaripoti kuwa raia wa Saudia mwenye jina kama hilo aliingia nchini mara tatu pamoja na wanafamila ya kifalme ya nchi hiyo.

Aliingia na kutoka Istanbul kwa kutumia ndege za abiria siku hiyo hiyo. Naye pia alifikia katika hoteli ya Wyndham Grand.

Naif Hassan S Alarifi, 32

Haki miliki ya picha AFP

Ukurasa wa Facebook wa mtu mwenye jina kama hilo unamuonesha akiw amevaa magwanda ya kikosi maalum cha kijeshi cha Saudia.

Aliingia Istanbul kwa kutumia ndege ya abiria na kufikia hoteli ya Wyndham Grand na kuondoka na ndege ya HZSK2.

Mustafa Mohammed M Almadani, 57

Haki miliki ya picha AFP

Almadani anasadikiwa kuwa jasusi wa Suadia na aliingia Istanbul kutumia ndege ya HZSK2 na kufikia hoteli ya Mövenpick. Aliondoka Istanbul kwa kutumia ndege ya abiria siku hiyohiyo.

Meshal Saad M Albostani, 31

Haki miliki ya picha AFP

Albostani anasadikiwa luteni katika jeshi la anga la Saudia.

Aliingia Istanbul kutumia ndege ya abiria na kufikia hoteli ya Wyndham Grand. Aliondoka na ndege ya HZSK2.

Tarehe 18 Oktoba, gazeti la Uturuki la Yeni Safak liliripoti kuwa Albostani alifariki katika ajali ya gari yenye utata jijini Riyadh lakini hawakutoa maelezo zaidi.

Waleed Abdullah M Alsehri, 38

Haki miliki ya picha AFP

Mtu mwenye jina kama hilo alipandishwa cheo katika jeshi la anga na Bin Salman mwaka jana, vyombo vya habari vya Saudia viliandika.

Alsehri aliingia Istanbul kwa ndege ya HZSK2 na kufikia Mövenpick, aliondoka na HZSK1.

Mansour Othman M Abahussain, 46

Haki miliki ya picha AFP

Mtu mwenye jina kama hilo alinukuliwa kama kanali katika kurugenzi ya ulinzi wa raia nchini Saudia na moja ya magaazeti ya nchi hiyo mwaka 2014.

Abahussein aliingia Istanbul kwa kutumia ndege ya abiria na kufikia hoteli ya Wyndham Grand na kuondoka na ndege ya HZSK2.

Fahad Shabib A Albalawi, 33

Haki miliki ya picha AFP

Mr Albalawi ni jasusi wa Saudia na liingia na moja ya ndege za kukodi na kufikia Mövenpick. Aliondoka na ndege ya HZSK1.

Badr Lafi M Alotaibi, 45

Haki miliki ya picha AFP

Alotaibi aliingia Istanbul kwa HZSK2 na kufikia Mövenpick, aliondoka kwa HZSK1.

Saif Saad Q Alqahtani, 45

Haki miliki ya picha AFP

Alqahtani kwamujibu wa Washington Post anafanya kazi na Bin Salman. Aliimgia Uturuki na HZSK2 na kufikia Movenpick na kuondoka na ndege ya abiria.

Turki Muserref M Alsehri, 36

Haki miliki ya picha AFP

Alsehri aliingia Istanbul kwa HZSK2 na kufikia Mövenpick, aliondoka kwa HZSK1.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii