Uganda: Ndoa mbili zisizo za kweli kufanyika nchini Uganda ili kukusanya ada ya chuo

Uganda

Chanzo cha picha, TWITTER

Maelezo ya picha,

Harusi batili ya mtangazaji wa redio Uganda kwa ajili ya kumsaidia Lulu Jeremiah

Mtangazaji mmoja nchini Uganda ameamua kufanya harusi isiyo ya kweli na rafiki yake siku ya ijumaa ambapo wageni wote watatakiwa kulipia harusi hiyo ili waweze kuhudhuria.

Sababu iliyompelekea kufanya maamuzi hayo ni baada ya mwandishi nchini humo Lulu Jemimah kuamua kujioa ili apate ada ya kwenda kusoma chuo kikuu cha Oxford.

Lulu mwenye umri wa miaka 32, aligonga vichwa vya habari siku za hivi karibuni alipoamua kujioa mwenyewe akiwa amevalia shera.

Unaweza ukajiuliza kwanini Lulu alijioa mwenyewe?

Lulu anasema kuwa yeye anafikiria zaidi kwenda kujiendeleza kielimu kuliko kutulia nyumbani na kuanza maisha ya ndoa.

"Nikiwa na umri wa miaka 21 au 22, watu walianza kuniuliza kuwa ni lini nitaingia katika maisha ya ndoa wakati mimi naona nina mambo mengi ya kufanya, kama kwenda kusoma na kupata elimu ya juu zaidi", aliiambia BBC.

Chanzo cha picha, Lulu Jemimah

aliongeza pia kuwa..."Nikiwa na miaka 16 baba yangu aliandika hotuba yake kwa ajili ya kuisoma siku ya harusi yangu. Kila nilipokuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa mama yangu alikuwa akiniombea, na kwa miaka ya karibuni maombi yake yalikuwa pamoja na kupata mume bora, ambaye atanifaa," amesema Bi Jemimah.

Aidha Lulu anadai kuwa msisitizo wa yeye kuolewa ulikuwa unatoka nje ya familia zaidi, watu wengi walimwambia anawezaje kutegemea kwenda nje ya Uganda huku hajapata mume, kwanini asiolewe kwanza ndio aondoke.

Anasema alitaka kuonyesha namna ambavyo hali ya ndoa ilivyo, wakati huo huo alipanga kuongeza kiasi ya pesa kilichokuwa kimesalia cha yeye kwenda kusoma shahada yake ambapo alikuwa anahitaji dola 12,000 ili aweze kuendelea na masomo kwani alikuwa amekosa ufadhili au kudhaminiwa.

Kwanini hii ni ndoa ya pili?

Taarifa ya ndoa hiyo kutangazwa kwenye kipindi cha radio kilichokuwa na mtangazaji Siima K Sabiti ambapo alikuwa na rafiki yake Bernard Mukasa walisema inabidi waoane ili kuweza kumsaidia pia.

"Ni lini utawaambia wazazi wako kuhusu ndoa hiyo? Hilo ni swali ambalo mara zote huulizwa," Bi.Sabiti aliiambia BBC.

Walipanga kufanya harusi kubwa, huku tiketi za kuingilia alipewa Lulu kwa ajiri ya kuwapa watu watakao mchangia kuongeza fedha zitakazomsaidia kwenda kusoma nje ya Uganda katika masomo yake ya ubunifu katika uandikaji katika chuo cha Oxford.

"Tunategemea kufanya kitu tofauti, tunatumia hela ya Uganda ambapo Lulu anahitaji kupata fedha kwa njia ya Pound ambayo inatumiwa nchini Uingereza,

nina mawazo chanya kuwa tunaweza kumsaidia kupata kiasi cha fedha ambazo anazitaka ambapo itamfanya kwenda kusoma kitu anachokipenda na kukitaka," Sabiti aliiambia BBC.

"Wasichana wengi wanashindwa kuhimili shinikizo la jamii katika mambo mengi tu, ambapo mwanawake kama Lulu aliweza kushikiria elimu yake na utaalamu wake katika kumiliki biashara yake mwenyewe na kuweza kufanya mambo kama hayo.

"utaratibu huu unaanza kidogo kidogo na badae wataelewa na kukubali jambo hili."

Maandalizi ya harusi isiyo ya kweli yalifanyika ambapo watumbuizaji pia walikuwa tayari kuigiza ili waweza kumsaidia Lulu aongeze fedha anazozihitaji kwenda kusoma shahada yake.

Mtangazaji Sabiti aliongoza mipango na harusi hiyo isiyo ya kweli na rafiki yake Bernard Mukasa baada ya kusikia kuwa Lulu Jemimah, mwandishi nchini Uganda anahitaji kwenda kusoma Zaidi katika fani yake ya ubunifu katika uandikaje.