Khashoggi: Saudi Arabia kuwachunguza wahusika wa mauaji ya Khashoggi

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema kuwa washukiwa wote wa mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi, mashtaka yao yatasikilizwa nchini Saudi Arabia.

Katika kikao mjini Bahrain, Adel al-Jubeir amevishutumu vyombo vya habari vya magharibi kwa kuongeza chumvi katika kuripoti taarifa ya kesi hiyo.

Kauli yake imekuja siku moja baada ya serikali ya Uturuki kutaka kuwaamisha washukiwa 18 waliohusika na mauaji hayo.

Mwandishi huo aliuwawa nchini Saudi Arabia mjini Istanbul wiki tatu zilizopita.

Mchumba wa Jamal,Riyadh imekanusha madai ya kuhusishwa kwa familia ya kifalme katika mauaji hayo na badala yake imelaumu watu iliyowataja kuwa''maajenti wakatili''

Awali Saudi Arabia ilikana kuhusika kwa lolote dhidi ya mwandishi huo lakini mwendesha mashtaka wa serikali sasa ameweza kueleza jinsi mauaji hayo yalivyotokea.

Chanzo cha picha, EPA

Khashoggi ambaye alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa mwana mfalme wa Saudia na viongozi wa Saudia.

Suala la kwamba washtakiwa ni raia wa Saudi ,hivyo inabidi Saudi Arabia iendelee kuchunguzwa kwa kina na washtakiwa hao watashitakiwa Saudi Arabia.

Haifahamiki kama Uturuki na Saudi Arabia wamefikia makubaliano ya kuwaamisha washitakiwa.

Hofu juu ya wapi mauaji hayo yalifanyika bado imetanda

Wasaudi Arabia wanaleza kuwa mauaji ya Khashoggi ni janga kubwa ambalo limetokea tangu shambulizi la kigaidi lililotokea mwaka 2001.

________________________________________

Wamarekani wanasema nini juu ya mauaji haya?

Marekani inasema kwamba bado itaendelea kuwashinikiza wasaudia kuelezea ukweli wa kifo cha mwandishi huyo kilivyotokea.

Wanasema kifo cha Khashoggi kinapaswa kuwagusa kila mmoja na hivyo Marekani haitakaa kimya kwa kitendo hiki cha kinyama alichofanyiwa mwandishi kwa vurugu.

Trump amesema: "Walikuwa na wazo duni sana, na wakalitekeleza vibaya mno, na kiufupi harakati zao za kuuminya ukweli ndio mbovu zaidi katika historia ya kujaribu kuficha ukweli."

"Naamini aliyekuja na wazo lile yupo katika matatizo makubwa hivi sasa. Na wanatakiwa kuwa kwenye matatizo," amesisitiza Trump.

Nchi yeyote inayoshindwa kuzingatia sheria na kanuni za kimataifa imeshindwa.

Lakini pia rais Trump alisisitiza kuwa kuna uwezekano kuwa mfalme hafahamu mauaji hayo yalitokea vipi.

Chanzo cha picha, EPA

Mchumba wa mwandishi Khashoggi anasemaje?

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Riyadh ,aliyekuwa mchumba wa Jamal

Mchumba wa mwanahabari wa Saudia aliyeuawa Jamal Khashoggi anasema amesusia mwaliko wa rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House kwa madai kiongozi huyo wa haijaonesha nia ya kutaka kujua ukweli kuhusu mauaji hayo ya kikatili.

Hatice Cengiz amekiambia kituo kimoja cha Televisheni nchini Uturuki kwamba mwaliko huo unalenga kubadili maoni ya Wamarekani

Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul wiki tatu zilizopita.

Mataifa mengine wanazungumziaje suala hilo?

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, alisema kuwa mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi yalipangwa siku kadhaa kabla ya kutekelezwa.

Erdogan alisema hayo alipokua akiwahutubia wabunge chama tawala nchini Uturuki.

Alisema Uturuki ina ushahidi mkubwa wa kuthibitisha kuwa mauaji ya Khashoggi yalikuwa yamepangwa na kutekelezwa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2.

Erdogan sasa anataka washukiwa wa mauaji hayo wafunguliwe mashtaka mjini Istanbul Uturuki.